Hammaz
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 6,607
- 14,076
Hutujui, sishangai ukitoa majumuisho hayo!Kwa hiyo akizingua sheikh mnamkataa lakini akizingua mchungaji wa wakristo mnajumuisha wakristo wote kwamba makafir
Kuna kafiri na ukafiri.
Ukafiri ni kuficha:Kwa upande wa uislamu kitendo cha hali ya kuficha haki ya muumba kwa namna moja ama nyengine inaitwa ukafiri. Kwa mtendaji atakayetenda hiyo hali ataitwa kafir.
Na kama hujui kilugha hata wakulima kuficha mbegu kwenye upandaji chini ya ardhi istilahi ya maneno yatakayo tumika ni hayo hayo! Ka-fa-r
Uislam unamtaka muislam auchukie ukafiri kwa sababu hata yeye mwenyewe anaweza akatumbukia humo! Kwa sababu ukafiri ni kitendo.
Uislam haumtaki muislam amchukie anayefanya kitendo cha ukafir kwa tafsiri nyengine kafiri. Kwa sababu wewe ni kiumbe cha Mungu na yeye Mungu ndiye anajua nini cha kufanya kwa viumbe wake. Na mwisho wa siku nijipe magonjwa ya moyo ya nini? Hivyo tunaishi kwenye msemo wa "Ikiwa unampenda Mungu, basi heshimu viumbe vyake"
Dini ya kiislamu inaendeshwa kwa elimu na elimu ndiyo dini yenyewe. Kwa msingi huo, si kila muislamu ni msomi. Kwa namna hiyo, usiuhukumu uislamu kwa matendo ya muislam!