Hekima na busara za mwanadamu hazipo kwenye kutokukosea bali ni kujifunza kulingana na makosa.....
Katika safari ya maisha ya kimahusiano kujikwaa ni jambo la kawaaida kwani tunaishi katika ulimwengu uliojaa wanafiki, waongo na walaghai...na ni vigumu kuikwepa mitego yao.....
Mara nyingine unaweza ukajikuta upo kwenye mikono ya shetani huku ukizani kuwa ni malaika.....na wakati mwingine ukajikuta upi kwenye mikono ya malaika wewe ukidhani ni shetani........
Kama ilivyo ngumu kuitofautisha ladha ya pepsi na Azam cola....ndivyo ilivyo ngumu kumtambua mnafiki na msema kweli kwani wote wanakuja katika sura na maumbo yaliyofanana......