Mtoa post sijui ulidhamilia nn ila nikuombe ufahamu single mothers sio wote ni watu wabaya! Na sio wote hawafai kupewa nafasi ya kuwa mke! Japo wapo wachache wanasababisha kuharibiwa kwa sifa za hawa watu na hii huwa ipo hata katika upande wa wanawake ambao ni non single mothers sio wote wanafaa kuolewa pia!
Kuna sababu nyingi zinapelekea mtu kuwa single mother including kifo cha mwenza,usaliti wa wanaume, kuachwa na wapenz au waume,kupata mimba wakiwa shule n.k kuna wadada wengine nao huamua kwa dhat ya mioyo yao kuamua kuwa hivyo walivyo! Kwaiyo siamini kama single mothers ni watu wabaya kama wengine wanavyojadili hapa! Kikubwa ni kujua Huyo mtu uliyenae ni muaminifu kiasi gani, mvumilivu kiasi gani !!
Tuwapumzishe Single mothers kwa kuwapa shutuma mbaya kwa kila kitu tuwapongeze kwa ujasiri wao wa kulea watoto wao pamoja na changamoto wanazopitia kuna watu wengi tu huoa single mother sio lazima uwe wewe unaeshinda kumkandia humu.