Kwanini baadhi ya wazazi hawapendi watoto wao kuoa 'single mother'?

Ahahahah waambie shougger
 
Ulichokisema ni sawa kabisa mi nafikiria wengi wa hawa single mum n mateso ambayo wanayapata kutok kwa hao baba mtoto ndio mana wanasema wacha nifanye mwenyewe sometime it's better letting go than holding on on something that keeps on bring you down like everyday
Wise word ladyaj
 
Mimi nilioa single mum zaidi ya miaka ishirini iliyopita na mbaya zaidi nikaoa bara [mimi ni nina asili ya zbar lkni nimezaliwa kariako] Mila zetu na dini ilikuwa ni tofauti [mimi ni muislam wkti yeye ni mkristu] alisilimu kwa hiari yake [kwenye suala la imani huwa sipendi kumlazimisha mtu]
Uhusiano wangu ulipingwa mama, dada zangu na ndugu karibu wote ila baba yangu tu.
Kwa vile mimi na mwenzangu tulishaamua suala hili[yeye alikuwa jasiri kuliko mimi maana yake kwao kazi ilikuwa ngumu zaidi] tulioana kiislamu[ingawa kwangu hata bomani ingekuwa sawa tu kwa wakati huo]
Katika kipindi chote cha ndoa hadi leo hii, mapenzi ya mke wangu kwangu nami kwake hayajapungua na wale watoto ambao nimewalea ni wakubwa sasa na wananithamini na kunipenda zaidi ya wale ambao tumezaa kwenye ndoa yetu.
Hivi sasa mke wangu ndiye amekuwa kipenzi cha ukoo wetu na watoto wa ndugu zangu wote wakiwa na matatizo kwenye ndoa zao basi mshauri wao mkubwa ni yeye.
Ninachosisitiza hapa ni kwamba tuache kuzungumza kiumjumla mambo nyeti kama haya.
 
Nielewe Mkuu,
Nilikuwa tayari nina nyumba yangu sio kwamba ninaishi kwa wazazi la hasha ila sikuwa napenda kulala nje kwanza isingekuwa mfano mzuri kwa wadogo zangu.
Halafu sikuwa napendelea kwenda lodge kwa sababu zangu binafsi.
Ila kama huo ni ujinga wacha nikubali kuwa mjinga ila nilichunga heshima yangu nyumbani kwangu maana baba ukiwavunjia heshima waliochini yako basi jua hata wao watakuvunjia heshima.
 
Shukran sana mkuu na hongera kwa hili jambo la kiujasiri zaid na upendo
Napata picha yawezekena n mtu na mtu na sio wrote wenye tabia zile wazazi wanazozifikir heshima kwako mkuu mawazo mazur na yenye hekim
 
Abunwasi kama umesoma vizuri hoja yangu sikusema wote bali nimesema wengi wao ndio wenye hizo hulka. Ukibahatika kumpata wa aina hiyo ni vizuri zaidi kwa sababu wengine wanakuwa wameshatendwa na hao wazazi wenzao kwa hiyo wanakuwa na upendo wa dhati hasa ukionesha kumjali yeye na mtoto wake.
Ila kwa upande wangu nilipata bahati mbaya kama hivyo.
 
Well said mkuu sio wote ila wengi wao wako hivo
 
Kunasababu nyingi za kuachana na mzazi mwenzio.Na hamna anayependa kulea mtoto mwenyew ila inabidi kutokana n mazingira.Nibora kuwa single mother kuliko kuendelea n mateso ndan ya moyo.Tulizaa ndio ila tunashukuru Mungu tumeolewa na maisha yanaendelea
 
Suala siyo hulka ila how do you click together [this is most important].
 
Hivi hao single mothers walidondoka Kutoka mbinguni?...

Wanaume ndio mnaowazalisha mabinti kisha kuwatelekeza au kuwasaliti, kisha ninyi ndio mnaongoza kwa kuwananga humu kila uchao...

Wengine mnajisifia kabisa "Nimemzalisha lakini sitomuoa" akaolewe na nani?

Wengine mama zenu ni 'single mothers',wamewalea wenyewe baada ya baba zenu kuwasaliti, na kuna thread humu jamvini mlikuwa mnawapongeza sana mama zenu kwa bidii waliyofanya kuwalea mpaka leo 'mmekuwa watu' lakini mnawasakama mpaka mnawasababishia usumbufu wa kisaikolojia..

Kuweni na staha japo kidogo.
 
Kachukue soda kwa mangi
 
Asante mzee mwenzangu.
 
Umenena dada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…