Tatizo ni generalisation ya topic. Huwezi kuwafagia single mothers wote, kuwazoa kwa kizoleo kimoja na wote kuwatupa jalalani.
Sababu ya wao kuwa single mothers ni nyingi, pengine walizaa kabla ya ndoa wakatoswa, waliachana au walifiwa na waume /partners wao, nk.
Kuna single mothers wamekuza watoto ambao sasa wamefanikiwa kimaisha kuliko hata wale waliotunzwa na wazazi wote wawili.
Tujitahidi ku avoid generalisation, kwani mara kwa mara tuki generalize vitu, tunaishia kuwa BIASED.
Cha maana mtoto atunzwe katika mazingira yenye upendo, apewe malazi, chakula na mahitaji yote muhimu. Mtoto huyu apewe pia elimu dunia pamoja na elimu ya kiroho, amche Mungu na ajue kwamba sisi sote tupo safarini hivyo hatuna budi tupendane, ikishindikana kupendana basi tuvumiliane.
Declaration: A happily married man for 25 years now.