Kwanini Biblia ilituficha kuhusu uzao wa majitu/Wanefili?

Kwanini Biblia ilituficha kuhusu uzao wa majitu/Wanefili?

ambi
Tangu mwanzo hadi ufunuo sijawahi ona biblia imetamka wazi kuwa manefili yalitokana na uzao wa mtu fulani sijawahi ona hilo andiko.Badala yake maandiko yanakuwa yanaibuka ghafla tu na kuwataja wanefili.

Sote tuna soma mwanzo 6 hadi9 na kuona ya kwamba Mungu aliingamiza dunia na viumbe vyake vyote isipokuwa waliokuwa ndani ya safina pekee yaani kwa upande wa binadamu ni familia ya Nuhu pekee ndiyo ilipona.

Sasa baada ya gharika hawa wanefili walitokea wapi tena ili hali biblia ina sema....

Mwanzo 7:23 Mungu akaangamiza kila kiumbe kilichokuwa hai duniani: Binadamu, wanyama, viumbe vitambaavyo na ndege wa angani. Vyote viliangamizwa duniani. Noa tu ndiye aliyesalimika na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina. 24Maji hayo yalidumu katika nchi siku 150.

Hivyo ni wazi kuwa kila chenye uhai kiliangamizwa kabisa kabisa.

Swali

Hawa wanefili baada ya gharika walitokea wapi tena?.

KARIBUNI
Ambiente Guru msaada tutani
 
baadhi wali survive kwenye galika
 
Acheni kusoma biblia kama novel, someni biblia kwa msaada wa roho mtakatifu ndio mtafunuliwa siri zake. Umeshiba zako ugali unakuja kusoma biblia kama unasoma novel hutaelewa
Wewe uliyeelewa maandiko pamoja na huyo roho mtakatifu wako leteni majibu hapa yasiyo na logical Contradictions yeyote ile.
 
Kama umewajua kupitia Biblia, iweje sasa useme Biblia inakuficha? Vitabu vingine vya mathematics, chemistry, physics etc mbona husemi vinakuficha kuhusu majitu hayo?
Ebu soma hapa
Mwanzo 5;
Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya;
2 mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.
3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.
4 Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.
5 Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa.
6 Sethi akaishi miaka mia na mitano, akamzaa Enoshi.
7 Sethi akaishi baada ya kumzaa Enoshi miaka mia nane na saba, akazaa wana, waume na wake.
8 Siku zote za Sethi ni miaka mia kenda na kumi na miwili, akafa.
9 Enoshi akaishi miaka tisini, akamzaa Kenani.
10 Enoshi akaishi baada ya kumzaa Kenani miaka mia nane na kumi na mitano, akazaa wana, waume na wake.
11 Siku zote za Enoshi ni miaka mia kenda na mitano, akafa.
12 Kenani akaishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli.
13 Kenani akaishi baada ya kumzaa Mahalaleli miaka mia nane na arobaini, akazaa wana, waume na wake.
14 Siku zote za Kenani ni miaka mia kenda na kumi, akafa.
15 Mahalaleli akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi.
16 Mahalaleli akaishi baada ya kumzaa Yaredi miaka mia nane na thelathini, akazaa wana, waume na wake.
17 Siku zote za Mahalaleli ni miaka mia nane na tisini na mitano, akafa.
18 Yaredi akaishi miaka mia na sitini na miwili, akamzaa Henoko.
19 Yaredi akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.
20 Siku zote za Yaredi ni miaka mia kenda na sitini na miwili, akafa.
21 Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela.
22 Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake.
23 Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano.
24 Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa.
25 Methusela akaishi miaka mia na themanini na saba, akamzaa Lameki.
26 Methusela akaishi baada ya kumzaa Lameki miaka mia saba na themanini na miwili, akazaa wana, waume na wake.
27 Siku zote za Methusela ni miaka mia kenda na sitini na kenda, akafa.
28 Lameki akaishi miaka mia na themanini na miwili, akazaa mwana.
29 Akamwita jina lake Nuhu, akinena, Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani Bwana.
30 Lameki akaishi baada ya kumzaa Nuhu miaka mia na tisini na mitano, akazaa wana, waume na wake.
31 Siku zote za Lameki ni miaka mia saba na sabini na saba, akafa.
32 Nuhu alikuwa mwenye miaka mia tano, Nuhu akawazaa Shemu, na Hamu, na Yafethi.

Kisha nijibu swali langu sasa wanefili walitoka katika uzao wa nani?
https://www.jamiiforums.com/javascript:window.print()
 
Kuna Malaika walipokuwa wakitumwa duniani walikuwa wakitamani Wanawake wazuri hivyo wakaanza kujibadilisha kuvaa miili ya kibinadam na kuzaa na binadamu ndio kikatokea hicho kizazi Cha wanefili
tafadhari lete andiko hilo mkuu
 
Acheni kusoma biblia kama novel, someni biblia kwa msaada wa roho mtakatifu ndio mtafunuliwa siri zake. Umeshiba zako ugali unakuja kusoma biblia kama unasoma novel hutaelewa
Malalamishi yote hayo ya nini mkuu? kama unajua si utwambie tu kuwa wanefili wametokana na uzao wa fulani
 
Back
Top Bottom