Kwanini Chato International Airport na si Omukajunguti international Airport? Kagera inaonewa sana

Mpango wa omukajunguti ni wa Siku nyingi

Je, mnatambua kuwa serikali imeshiriki katika kuudumaza mkoa kagera?
Hivi ndivyo mkoa kagera umeachwa yatima na serikali ya Tanzania,
Tulivyopata Uhuru kagera ilikuwa miongoni mwa mikoa mitatu yenye uchumi imara,

1. Dar es salaam
2. Kagera
3. Kilimanjaro

Lakin ukweli usiopingika Kagera imetelekezwa na serikali vya kutosha bila kujali majanga yaliyoikuta au michango ambayo Kagera imetoa kwa watanzania.

Kila MTU kutokea Kagera atakuwa ana kumbukumbu zinazomfanya kusononeka sana,

SABABU MUHIMU ZILIZOSABABISHA KAGERA KURUDI NYUMA KIMAENDELEO

1. VITA YA KAGERA, 1978/79
Vita ya nchi nzima ilipiganwa kwenye mkoa mmoja na kuharibu miundombinu vya kutosha , na ule ndo ulikuwa uwanja wa vita hasa, lakini hakuna sehemu yoyote kuna strategy za kuujenga upya mkoa, tunaishia kusikia maneno ya kashfa tu tena toka kwa viongozi wakubwa kwa wanakagera eti mmeshindwa kujenga hata chuo kikuu kimoja? Aliuliza Kikwete lakini kasahau kuwa yeye kama mkuu wa serikali hajajenga hata chuo cha kutoa cheti.

2. JANGA LA UKIMWI 1983,
Kama inavyojulikana Kagera iko mpakani mwa Uganda, na UKIMWI umeanzia Uganda, na kwa kuwa wana Kagera wana utaratibu wa kufanya Biashara na Uganda , haikukwepeka kupata UKIMWI, nguvu Kazi kubwa ilipotea sana miaka hiyo na kusababisha uchumi kurudi nyuma,

3. AJALI YA MV BUKOBA
Janga la pili ambalo linafanya kudhoofisha mkoa wa Kagera ni kuwa , watoto wengi yatima wameongezeka , nguvu kazi imepungua kutokana na ajali ile.

4.1998 EL NINO
Hii wengi mnaelewa kuwa imekumba sana ukanda wa kanda ya ziwa kuliko kanda yoyote ile hapa nchini , imeharibu miundombinu na kupoteza wazalishaji Mali,

5. KUSHUKA KWA BEI YA KAHAWA 1998 KWA UZEMBE WA SERIKALI.
Inajulikana Kagera ilitegemea sana Kahawa kama kitega uchumi , kwa uzembe wa serikali hakukuwepo utaratibu wa kuhakikisha Kahawa inabaki na bei ya kuridhisha badala yake ikapuuza mpaka wananchi wakakata mibuni maana haikuwa na maana tena,

6. UBAGUZI ULIOJIFICHA TOKA KWA VIONGOZI ( INDIRECT DISCRIMINATION TOWARDS HAYA TRIBE)
Miaka ya nyuma hakuna ambaye hajui kuwa wahaya waliwekewa mizengwe katika baadhi ya sekta, hata kwenye elimu , walipandishiwa alama za ufaulu ili wachache waendelee na elimu ya juu maana walionekana kuwa wao ndio wanafaulu na kujaza madarasa mengine, lakin ili kuitamka sentensi hii (INAHITAJI UJIFANYE MWENDA WAZIMU KIDOGO)

7. KUTENGWA NA NCHI KIJIOGRAFIA
Kagera iko Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, waliowahi kufika uko ndio wanaelewa namaanisha nini, Kagera imekuwa kama kisiwa maana jinsi ya kufika kule inabidi ukatishe kilometer kadhaa za msitu, ili uingie Kagera, au upite ziwani kwa meli ndio uende mikoa mingineyo ambayo ni ya Tanzania, hivyo basi wana Kagera walikuwa na urahisi wa kufanya Biashara na Uganda kuliko mikoa mingine ya Tanzania, lakini serikali ilikataza biashara hiyo , wakajikuta wamebaki kama kisiwa ndani ya nchi yao wenyewe,

8.KAGERA KIMBILIO LA WAKIMBIZI MAUAJI YA KIMBALI YA RWANDA 1994 NA MACHAFUKO TANAYOENDELEA UKANDA ULE.
Wanyarwanda wameiteka Kagera hasa wilaya ya Karagwe na Muleba na kujichukulia ardhi , pia wamekuwa watekaji wa magari na kudhalilisha wana kagera , kitu amabacho kimerudisha nyuma uchumi wa mkoa, kwa kasi, majambazi wametamalaki na kufanya uharamia ambao umefanya kusiwepo hali ya utulivu na kujenga uchumi, serikali imechelewa kuchukua hatua,

9. KUTOJUMUISHWA KATIKA VIPAUMBELE VYA MAENDELEO KIKANDA
Kila kanda imetengwa katika kanda fulani ya mkakati wa maendeleo lakini kanda ya ziwa ambayo ndipo kuna mkoa Kagera hakuna ilipoainishwa katika mpango wa maendeleo.Kagera Umekuwa ni mkoa wa kujitegemea kwa kila kitu utasikia

Ukumbi wa mkutano unajengwa Arusha, sijui chuo cha utalii Dar, chuo cha ufugaji Tabora.

Chuo cha reli tabora, chuo cha science cha nelson Mandela arusha,
Chuo cha serikali cha ugavi, Chuo cha ushirika Moshi Mara..

Chuo cha mbao Iringa, kwanini Kagera hakuna mipango endelevu, sasa upo wapi uwanja wa Mukajunguti wa ndege na ulishaahidiwa kuwa wa kimataifa na kutengewa bajeti kipindi cha Mkapa?,Rais Magufuli halioni hilo?

Kagera wanekuwa wa kupandia kama daraja, Kikwete kaenda Bukoba katoa ahadi ambayo imerudiwa na Magufuli sana, eti ntawapa meli ,mbona hata mtumbwi haujaweka,

We unayesoma hapa nitajie chuo chochote kilichojengwa na serikali kuazia cheti mpaka degree, imekuwa vipaumbele kujenga Dodoma na mnasahau kuna deni Kagera inadai kwa taifa hili.

Kilichosaidia Kagera ni vishirika vya wazungu tu kama partage, world vision, gses, yaan serikali haijatenda haki huko.

SOMA HII SASA SERIKALI INA KITU KINAITWA SUBJECTIVE AND OBJECTIVE PLANNINGS,(BIG FOUR REGIONS) IKO HIVI

1.KANDA YA KUSINI AU NYANDA ZA JUU KUSINI
Imetengwa kama kanda ya kilimo hapa kuna mikoa
Njombe
Mbeya
Katavi
Ruvuma
Na Iringa .

2.KANDA NYINGINE KANDA YA KASKAZINI
Hii imeahinishwa na kupewa kipaumbele kama kanda ya utalii,
Mikoa ni
Arusha,
Kilimanjaro na Manyara,

3.NYINGINE NI KANDA YA KATI ,
Taasisi za siasa na Elimu ya juu
Mikoa ni
Morogoro,
Dodoma,
Singida,

4. KANDA YA MASHARIKI INEPEWA Kanda ya viwanda na Biashara, mikoa ni
Dar es salaam,
Mtwara
Lindi
Pwani
Tanga

KANDA YA ZIWA ANBAYO KUNA KAGERA IKO WAPI, ?
Sasa inafika hatua tunapaswa kuusema ukweli ,

Mheshimiwa rais huu ulikuwa ninwakati wa Kujenga MUKAJUNGUTI INTERNATIONAL AIRPORT SIYO CHATO. TUNGEPOZWA ANGALAU NA UWANJA UO MAANA TUMESUBIRI NEEMA KWA MIAKA MINGI LAKIN WAPI

Wengi watasema umejenga huko kwakuwa ni kwenu, lakini pia hata KAGERA KARAGWE NI KWENU KWA MZEE MACHALILA, NA JINA LAKO LA KIHAYA NI KATO (wengi hawajui hii), sasa kama ndo sababu ya kujenga nyumbani anza nyumbani ambapo pako kwenye mipango ya Siku nyingi,
Kajunguti International Airport - Wikipedia, the free encyclopedia
This is real you. Now I know
 
Huko ndiyo kulio toa wasomi wengi nchi hii? Elimu kweli haiwezi kumkomboa Mwafrica....

Wanashindwa kutumia elimu yao kujenga mkoa wao??
 
Naona kina mangi mnaendeleza chuki zenu na ukabila. Vuteni subira siku mkipata Rais kutoka huko mtapafanya Dubai.
 
Omukajunguti Airport canceled!!! Tunapanua Bukoba Airport. Kigoma Airport tuwe na subira
 
Tatizo la wahaya ni kudhani ili uonekane mtu wa matawi lazima ukae Dar au Mwanza, wakisoma hawataki kurudi bukoba wanaenda kuzika na kuondoka, sasa hivi wasukuma wanajenga kwao, tizama mji wa katoro kahama na bwanga inakua kwa kasi, leo hii kukuta nyumba ya kisasa kijijini ni jambo la kawaida sana.
Nadhani uwanja wa Omukajunguti ulihujumiwa na wawakilishi waoga au wabinafsi wa Kagera kupitia CCM. Bajeti ilitengwa lakini wafuatiliaji hawakuwepo. Mwishowe pesa wakachukuwa wanaojua matumizi yake. Nasikia ilihamishiwa Katavi kwa Pinda.
 
Rais Magufuli anasema Uwanja wa Mkajunguti hautajengwa labda miaka ya mbele. badala yake atapanua uwanja wa bukoba mjini. Kasema kuna watu hewa zaidi ya elfu mbili. hivyo wananchi wasiache kulima. Waendlee kulima kwani Uwanja hautajengwa.
 
Toeni rais na nyie mpate advantages

Usiombee hawa watu wapate rais, hakuna kabil la kibaguzi hapa Tanzania kama wahaya na wanyambo.....I say never zaidi ya hawa watu, yaani hawafai kabisa...tuwarudishe tu Uganda tena immediately.
 
Ni kweli mkoa wa kagera ni kama umetengwa kagera kuna kila kitu kizuri aridhi yenye lutuba, hali ya hewa nzuri, umeme wa uhakika, na watu wake wameelimika sana, na katika dini wapo vizuri (kuna wakati makanisa makubwa hapa TZ yaani RC na KKKT kwa wakati mmoja yoote yalikuwa yanaongozwa na wahaya)Rugambwa na Dr Mushemba, lkn cha kushangaza ulianzishwa mchakato wa kumtangaza kiongozi wa kisiasa kuwa mwenyeheri akaachwa karidinali wa kwanza mwausi........
....mwenyeheri ni wa kanda hiyo hiyo !
 
Je, mnatambua kuwa serikali imeshiriki katika kuudumaza mkoa kagera?
Hivi ndivyo mkoa kagera umeachwa yatima na serikali ya Tanzania,
Tulivyopata Uhuru kagera ilikuwa miongoni mwa mikoa mitatu yenye uchumi imara,

1. Dar es salaam
2. Kagera
3. Kilimanjaro

Lakin ukweli usiopingika Kagera imetelekezwa na serikali vya kutosha bila kujali majanga yaliyoikuta au michango ambayo Kagera imetoa kwa watanzania.

Kila MTU kutokea Kagera atakuwa ana kumbukumbu zinazomfanya kusononeka sana,

SABABU MUHIMU ZILIZOSABABISHA KAGERA KURUDI NYUMA KIMAENDELEO

1. VITA YA KAGERA, 1978/79
Vita ya nchi nzima ilipiganwa kwenye mkoa mmoja na kuharibu miundombinu vya kutosha , na ule ndo ulikuwa uwanja wa vita hasa, lakini hakuna sehemu yoyote kuna strategy za kuujenga upya mkoa, tunaishia kusikia maneno ya kashfa tu tena toka kwa viongozi wakubwa kwa wanakagera eti mmeshindwa kujenga hata chuo kikuu kimoja? Aliuliza Kikwete lakini kasahau kuwa yeye kama mkuu wa serikali hajajenga hata chuo cha kutoa cheti.

2. JANGA LA UKIMWI 1983,
Kama inavyojulikana Kagera iko mpakani mwa Uganda, na UKIMWI umeanzia Uganda, na kwa kuwa wana Kagera wana utaratibu wa kufanya Biashara na Uganda , haikukwepeka kupata UKIMWI, nguvu Kazi kubwa ilipotea sana miaka hiyo na kusababisha uchumi kurudi nyuma,

3. AJALI YA MV BUKOBA
Janga la pili ambalo linafanya kudhoofisha mkoa wa Kagera ni kuwa , watoto wengi yatima wameongezeka , nguvu kazi imepungua kutokana na ajali ile.

4.1998 EL NINO
Hii wengi mnaelewa kuwa imekumba sana ukanda wa kanda ya ziwa kuliko kanda yoyote ile hapa nchini , imeharibu miundombinu na kupoteza wazalishaji Mali,

5. KUSHUKA KWA BEI YA KAHAWA 1998 KWA UZEMBE WA SERIKALI.
Inajulikana Kagera ilitegemea sana Kahawa kama kitega uchumi , kwa uzembe wa serikali hakukuwepo utaratibu wa kuhakikisha Kahawa inabaki na bei ya kuridhisha badala yake ikapuuza mpaka wananchi wakakata mibuni maana haikuwa na maana tena,

6. UBAGUZI ULIOJIFICHA TOKA KWA VIONGOZI ( INDIRECT DISCRIMINATION TOWARDS HAYA TRIBE)
Miaka ya nyuma hakuna ambaye hajui kuwa wahaya waliwekewa mizengwe katika baadhi ya sekta, hata kwenye elimu , walipandishiwa alama za ufaulu ili wachache waendelee na elimu ya juu maana walionekana kuwa wao ndio wanafaulu na kujaza madarasa mengine, lakin ili kuitamka sentensi hii (INAHITAJI UJIFANYE MWENDA WAZIMU KIDOGO)

7. KUTENGWA NA NCHI KIJIOGRAFIA
Kagera iko Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, waliowahi kufika uko ndio wanaelewa namaanisha nini, Kagera imekuwa kama kisiwa maana jinsi ya kufika kule inabidi ukatishe kilometer kadhaa za msitu, ili uingie Kagera, au upite ziwani kwa meli ndio uende mikoa mingineyo ambayo ni ya Tanzania, hivyo basi wana Kagera walikuwa na urahisi wa kufanya Biashara na Uganda kuliko mikoa mingine ya Tanzania, lakini serikali ilikataza biashara hiyo , wakajikuta wamebaki kama kisiwa ndani ya nchi yao wenyewe,

8.KAGERA KIMBILIO LA WAKIMBIZI MAUAJI YA KIMBALI YA RWANDA 1994 NA MACHAFUKO TANAYOENDELEA UKANDA ULE.
Wanyarwanda wameiteka Kagera hasa wilaya ya Karagwe na Muleba na kujichukulia ardhi , pia wamekuwa watekaji wa magari na kudhalilisha wana kagera , kitu amabacho kimerudisha nyuma uchumi wa mkoa, kwa kasi, majambazi wametamalaki na kufanya uharamia ambao umefanya kusiwepo hali ya utulivu na kujenga uchumi, serikali imechelewa kuchukua hatua,

9. KUTOJUMUISHWA KATIKA VIPAUMBELE VYA MAENDELEO KIKANDA
Kila kanda imetengwa katika kanda fulani ya mkakati wa maendeleo lakini kanda ya ziwa ambayo ndipo kuna mkoa Kagera hakuna ilipoainishwa katika mpango wa maendeleo.Kagera Umekuwa ni mkoa wa kujitegemea kwa kila kitu utasikia

Ukumbi wa mkutano unajengwa Arusha, sijui chuo cha utalii Dar, chuo cha ufugaji Tabora.

Chuo cha reli tabora, chuo cha science cha nelson Mandela arusha,
Chuo cha serikali cha ugavi, Chuo cha ushirika Moshi Mara..

Chuo cha mbao Iringa, kwanini Kagera hakuna mipango endelevu, sasa upo wapi uwanja wa Mukajunguti wa ndege na ulishaahidiwa kuwa wa kimataifa na kutengewa bajeti kipindi cha Mkapa?,Rais Magufuli halioni hilo?

Kagera wanekuwa wa kupandia kama daraja, Kikwete kaenda Bukoba katoa ahadi ambayo imerudiwa na Magufuli sana, eti ntawapa meli ,mbona hata mtumbwi haujaweka,

We unayesoma hapa nitajie chuo chochote kilichojengwa na serikali kuazia cheti mpaka degree, imekuwa vipaumbele kujenga Dodoma na mnasahau kuna deni Kagera inadai kwa taifa hili.

Kilichosaidia Kagera ni vishirika vya wazungu tu kama partage, world vision, gses, yaan serikali haijatenda haki huko.

SOMA HII SASA SERIKALI INA KITU KINAITWA SUBJECTIVE AND OBJECTIVE PLANNINGS,(BIG FOUR REGIONS) IKO HIVI

1.KANDA YA KUSINI AU NYANDA ZA JUU KUSINI
Imetengwa kama kanda ya kilimo hapa kuna mikoa
Njombe
Mbeya
Katavi
Ruvuma
Na Iringa .

2.KANDA NYINGINE KANDA YA KASKAZINI
Hii imeahinishwa na kupewa kipaumbele kama kanda ya utalii,
Mikoa ni
Arusha,
Kilimanjaro na Manyara,

3.NYINGINE NI KANDA YA KATI ,
Taasisi za siasa na Elimu ya juu
Mikoa ni
Morogoro,
Dodoma,
Singida,

4. KANDA YA MASHARIKI INEPEWA Kanda ya viwanda na Biashara, mikoa ni
Dar es salaam,
Mtwara
Lindi
Pwani
Tanga

KANDA YA ZIWA ANBAYO KUNA KAGERA IKO WAPI, ?
Sasa inafika hatua tunapaswa kuusema ukweli ,
 
pmj na yoote wengi wa wana kagera n wavivu hamjitumi kuinua uchumi binafsi,ubunifu wa kiuchumi kwenu n 0% kbs ukiachilia mbali mchango wa serikl
mfano hata tu biashara ya mabasi mneshindwa kubuni hadi watu wa Kilimanjaro wamewaletea mabasi ya kuja kwenu mfano kidia one,Osaka prince muro nk mjitume kwanza kabla ya kuilalamikia serikal
 
pmj na yoote wengi wa wana kagera n wavivu hamjitumi kuinua uchumi binafsi,ubunifu wa kiuchumi kwenu n 0% kbs ukiachilia mbali mchango wa serikl
mfano hata tu biashara ya mabasi mneshindwa kubuni hadi watu wa Kilimanjaro wamewaletea mabasi ya kuja kwenu mfano kidia one,Osaka prince muro nk mjitume kwanza kabla ya kuilalamikia serikal
 
pmj na yoote wengi wa wana kagera n wavivu hamjitumi kuinua uchumi binafsi,ubunifu wa kiuchumi kwenu n 0% kbs ukiachilia mbali mchango wa serikl
mfano hata tu biashara ya mabasi mneshindwa kubuni hadi watu wa Kilimanjaro wamewaletea mabasi ya kuja kwenu mfano kidia one,Osaka prince muro nk mjitume kwanza kabla ya kuilalamikia serikal
 
Usiombee hawa watu wapate rais, hakuna kabil la kibaguzi hapa Tanzania kama wahaya na wanyambo.....I say never zaidi ya hawa watu, yaani hawafai kabisa...tuwarudishe tu Uganda tena immediately.
Wewe ndo hufai na hhujitambui, Africa ni moja ..Uganda, Tanzania, Kenya n.k hiyo ni mipango ya kikoloni kutawala Africa .. kibaya zaidi watu wenye ulemavu wa akili ndo wanaendelea kushabikia mambo ya mipaka ambayo hawakuiweka wao wala mababu zao.
Ukimuuliza Mjaruo utaambiwa alitokea Misri, mwingine Uganda, mwingine Msumbiji n.k. Tumia kichwa chako kujadili mambo ya maana siyo kukifanya kichwa kuwa dumu la kutunzia ubongo.
 
Ukichukua Rugemarila family na Kyaruzi family unapata nusu ya utajiri wa nchi hii waulize kwanini hawawekezi kwao?
hahaha wahaya kwa sifa bwana..

mbona hatuwaoni sasa kwenye forbes hau kina kyaruzi, forbes hata ya afrika tuu
 
..kama mkoa uliozaliwa "unanyimwa" maendeleo hamia ktk mikoa "inayopendelewa."

..kuna kipindi Mwalimu Nyerere alianzisha mpango wa quota system ktk nafasi za masomo ya sekondari.

..mikoa fulani iliremshiwa pass mark za kwenda sekondari, huku mikoa mingine ikiwekewa ugumu zaidi.

..wazazi toka mikoa ile ambayo Mwalimu aliamua "kuibinya" ktk kufaulu kwenda sekondari wakawa wanahamisha watoto wao, wanabadili hata majina, na kwenda kusoma darasa la 7 kwenye mikoa iliyokuwa "ikipendelewa."

..KAMA MKOA WAKO UNANYIMWA MAENDELEO HAMIA MKOA UNAOPENDELEWA.
Hiyo quota system ilikuwa mbaya kabisa!
 
Back
Top Bottom