Kwanini China nchi ya kidikteta ina maendeleo makubwa kuliko Kenya na Zambia?

Kwanini China nchi ya kidikteta ina maendeleo makubwa kuliko Kenya na Zambia?

kwa tafsiri hii china sio nchi ya kidikteta......
wana katiba bora, wana sheria bora, wala neno la Xi sio sheria.......

magharibi ndio wameharibu tafsiri ya dikteta kwa kumwita dikteta kila mtu wanae mchukia
Amekosea kidogo kusema mtu mmoja, kuna
Junta dictatorship,
Party dictatorship,
Theocracy
 
Sababu ni nyingi,
Kwanza lazima ufahamu China wana msingi mkubwa wa uvumbuzi na ubunifu wa miaka mingi, Dira, gunpowder, karatasi na mashine za kale za kuchapa ziligunduliwa China.

Pili udikteta wa China ni udikteta wa mfumo wa meritocracy, sio udikteta kama wa Waafrika wa "unanijua mimi ni nani" au baadhi ya familia kuhodhi utawala wa nchi.

Lingine demokrasia ni muhimu sana lakini haikupi kila kitu, ili demokrasia ikusaidie inahitaji mazingira wezeshi pia ambayo hayako kwa nchi nyingi za Africa.
Mfano ni kutokuwepo utamaduni wa rushwa, nepotism, ukabila, raia wengi wajinga n.k
Nimeipenda hii kwenye bold.
 
Hakuna mahusiano yeyote kati ya maendeleo ya nchi husika na mfumo wake unao iongoza.
Na ndo maana kuna nchi zinazo ongozwa kidemokirasia ni tajiri na kuna nyingine zina uchumi wa kati na kuna nyingine ni masikini kabisa,na upande wa nchi zinazo itwa za kidkiteta ni vilevile.

Taifa lolote linapata maendeleo kwa sababu ya uwajibikaji wa viongozi na jamii ya watu wa nchi hiyo,sasa huku Africa kuanzia viongozi mpaka kwa raia uwajibikaji ni zero.

Ukitaka kujua kuwa waafrica ni jamii ya hovyo ww nenda vyuoni ambavyo ndo vinategemewa kuzalisha viongozi na watumishi wa uma uone mambo yanayo fanyika.
Yaani tunataka tuzalishe viongozi bora kutoka kwenye jamii iliyo oza.
 
Sasa mbona China inaendeshwa tofauti kabisa na hiyo definition yako hiyo?
China ukizingua haijalishi ww ni nani una cheo gani utakula kitanzi na mchakato wao wa kula kitanzi huwa sio mrefu ,hukumu ya kitanzi inatoka leo na inaelelezwa ndani ya wiki.
Kuna udikteta wa aina nyingi China ina udikteta wa kichama lakini hiyo sio kizuizi wao kushughulikia viongozi wenye mawenge
 
kwa tafsiri hii china sio nchi ya kidikteta......
wana katiba bora, wana sheria bora, wala neno la Xi sio sheria.......

magharibi ndio wameharibu tafsiri ya dikteta kwa kumwita dikteta kila mtu wanae mchukia
Kuna udikteta wa kichama na hapo ndipo China alipo Xi anaweza asiwe na nguvu yoyote lakini chama cha kikomunisti kikawa kimehodhi nguvu zote
 
Hakuna mahusiano yeyote kati ya maendeleo ya nchi husika na mfumo wake unao iongoza.
Na ndo maana kuna nchi zinazo ongozwa kidemokirasia ni tajiri na kuna nyingine zina uchumi wa kati na kuna nyingine ni masikini kabisa,na upande wa nchi zinazo itwa za kidkiteta ni vilevile.

Taifa lolote linapata maendeleo kwa sababu ya uwajibikaji wa viongozi na jamii ya watu wa nchi hiyo,sasa huku Africa kuanzia viongozi mpaka kwa raia uwajibikaji ni zero.

Ukitaka kujua kuwa waafrica ni jamii ya hovyo ww nenda vyuoni ambavyo ndo vinategemewa kuzalisha viongozi na watumishi wa uma uone mambo yanayo fanyika.
Yaani tunataka tuzalishe viongozi bora kutoka kwenye jamii iliyo oza.
Nakuelewa
 
China hawacheki na kima ujue. Mfano, jengo lililoporomoka Kariakoo jana; asubuhi ya leo wananchi wangekuwa wamekusanyika viwanja vya Mnazi Mmoja kushuhudia mass execution ya wote walioshiriki ujenzi ule! Mko tayari au ni siasa za kulindana?
👆
Huo ndio wanasema udikteta.Wakati kwa hizi nchi za Africa ndio ilitakiwa iwe namna hiyo ili tutoke kwenye huu mkwamo wa ubinafsi,kulindana na rushwa.
 
Kwanini China nchi yenye udikteta wa chama kimoja ina maendeleo makubwa kwenye nyanza mbalimbali kuliko nchi za kidemokrasia za vyama vingi kama Kenya na Zambia ?
Udikteta unaouona wewe ndio umeifikisha China hapo ilipo,ujamaa ukisha komaa sana baadaye huwa unageuka kuwa kama ubepari,ni kweli walitaabika sana wakati wa kutafuta ila sasa hivi wanawaenzi waasisi wa taifa lao kwa kifua mbele.Nadhani unakumbuka Mwamba Magufuli alivyobeba jina la udikteta na wapi alitufikisha,hakuna maendeleo bila ya jasho,tafakari na chukua hatua...
 
Unamkubali sana Magufuli ?
 
Why do we have a two party system when we were all taught that a country divided cannot stand?
Politics dividing people,separates people from each other,
Politics can't do nothing for you that you can't do for self.
 
Miluzi mingi humpoteza mbwa,kwenye demokrasia watu wanapata muda wa kukosoa kila kitu! Kuna kijiji nilikulia miaka ya tisini kile kijiji kilikuwa kisafi Sana wanakijiji waliishi Kwa ushirikiano Sana,barabara walitengeneza wenyewe Kwa kujitolea,hapo ndio Kiongozi alipatikana Kwa kuangalia mtu anayejitoa Sana kwenye KAZI za kijamii! Ulikuwa kuiangalia mtaa unaweza ona mbele hata kilometer 5 usione hata karatasi! Badae nikaenda baada ya miaka 15 dooh salala! Kijiji kichqfu balaa madiwani wanasema tunashindwa kuwafosi watu kwenye KAZI za maendeleo watakunyima kura
 
Ni issu ya mindset. Ukikosa msukumo ndani yako ya kufanya maendeleo mwenyw. Ndo ile tabia ya kuzoea watu kukupambania haki zao. Viongozi nao wanawaza watakul wapi hawan muda na wananchu
 
Mimi hoja yangu huwa hivi Democracy sio kwamba ni benchmark ya utawala wa dunia nzima kwamba ndio mataifa yote yaufuate.

Kuja kwa Democacy ni katika harakati tu za wanadamu kujaribu jaribu aina ya political ideologies au utawala. Usishangae miaka ya mbele kukaja na mfumo mwingine kabisa

Democracy ni ideology tu ambayo mataifa ya Magharibi waliadopt kutoka kwa wahasisi ambao ni Greece

Walichofanya nchi za Magharibi ni kuforce mataifa mengine duniani yatumie mfumo huo wakati wa vita ya ideology (Cold War) kati ya Democracy na Socialism

Nchi za Magharibi zimeingiza chaka mataifa mengi duniani ku-adopt Democracy wakiamini ndio msingi wa maendeleo lakini mwisho wa siku hakuna maendeleo yoyote.

Mataifa yenyewe ya Magharibi yalijipata kupitia political ideology ya Monarchy walipokuwa wanapora mali za mataifa mengine kipindi cha Feudalism.

Halafu leo wanakuja kuhubiri Democracy inaleta maendeleo WTF! Wameleta Democracy ili waweze kuwatawala kupitia ukoloni mambo leo.

Cha ajabu taifa kama Uingereza kipindi cha Monarchy lilijipata sana ilikuwa taifa kubwa duniani lilikuwa WORKSHOP OF THE WORLD kama tunavyosema leo China ni The World's factory

Uingereza walifanya INVENTIONS kubwa sana kwenye kipindi hicho ila kwenye Democracy taifa hilo limekuwa kituko

Mataifa mengi ya Magharibi yameanza kuwa na democratic election iliyo kamili miaka ya 1960s na 1970s

Miaka ya nyuma ya hapo hakukuwa na democratic election kamili ilikuwa na kasoro nyingi kwa mfano wenye mali na vipato ndio waliruhusiwa kupiga kura, ubaguzi wa jinsia na rangi n.k

My take: ilitakiwa kila taifa lijiamulie mfumo wake wa utawala mbona kabla ya Democracy maisha yaliendelea kama kawaida

Wachina hawajatetereka kwenye kukubali mfumo wa Democracy wao wamejipata kwenye mfumo wao wa
Socialism with Chinese characteristics
 
Back
Top Bottom