Mi mi
JF-Expert Member
- Jul 14, 2024
- 2,748
- 5,112
- Thread starter
- #141
Xi hajafikia power ya Deng Xiaoping, Deng hata alivyo retire bado alikuwa na nguvu ya maamuzi 1992 alionesha power yake.Kwa mtindo wao wa uongozi wa China nafasi aliyokuwa nayo Dieng Xioaping (Paramount leader) ni sawa na raisi tu, kwani baada ya kuondoka kwa Mao yeye ndio alikuwa mbeba maono.
Naona mnanchukulia poa sana Xi ila wachina wanajua ni kwanini wameona yeye ndio anawafaa kuwaongoza kwa maisha yake yote hasa kwenye hizi nyakati ngumu ambapo Kuna battle kubwa sana ya kiuchumi kati yao na Marekani
Si kwamba namdharau Xi hapana ila Mao na Deng walikuwa na nguvu kubwa sana kuna kipindi hata position za kiutwala hawakuwa nazo ila maamuzi yao yalikuwa na nguvu.
Xi ni katibu wa chama cha kikomunisti,Rais, mwenyekiti wa kamati kuu ya kijeshi position zote anazo sasa hii ni tofauti na Deng