Kwanini China nchi ya kidikteta ina maendeleo makubwa kuliko Kenya na Zambia?

Kwa mtindo wao wa uongozi wa China nafasi aliyokuwa nayo Dieng Xioaping (Paramount leader) ni sawa na raisi tu, kwani baada ya kuondoka kwa Mao yeye ndio alikuwa mbeba maono.

Naona mnanchukulia poa sana Xi ila wachina wanajua ni kwanini wameona yeye ndio anawafaa kuwaongoza kwa maisha yake yote hasa kwenye hizi nyakati ngumu ambapo Kuna battle kubwa sana ya kiuchumi kati yao na Marekani
Xi hajafikia power ya Deng Xiaoping, Deng hata alivyo retire bado alikuwa na nguvu ya maamuzi 1992 alionesha power yake.

Si kwamba namdharau Xi hapana ila Mao na Deng walikuwa na nguvu kubwa sana kuna kipindi hata position za kiutwala hawakuwa nazo ila maamuzi yao yalikuwa na nguvu.

Xi ni katibu wa chama cha kikomunisti,Rais, mwenyekiti wa kamati kuu ya kijeshi position zote anazo sasa hii ni tofauti na Deng
 
Udikteta ndio uliofanya Xi abadilishe katiba kwa kupata kura za wajumbe wote wa mkutano mkuu/congress(bunge). Mbunge katika bunge la Marekani anaweza kumtukana hata Biden na asifanywe chochote , Elon Musk anamtukana Biden na chama chake Marekani mara nyingi bila kufanywa chochote. Hakuna Mbunge anaweza kumpinga Xi China bila mkakati mpana na wa muda mrefu. Jack Ma aliyekuwa bilionea namba 1 China alijaribu kukosoa kwa mbali tu CCP wakomunisti wakamchukua wakamficha kwa muda aliporudi akawa anaimba Xi anaupiga mwingi na utajiri wake wakautikisa sasa hivi amepoa na kunywea kabisa.

Deng Xioaping hakubadilisha kwa sababu hakutaka na wakati huo kulikuwa na watu watata sana katika siasa za China kuliko walivyo leo hii. Hata Deng kuyapata madaraka ya China na kuwa mtawala kamili ilikuwa mtiti sio wa kitoto na palichimbika haswa ndani ya chama cha CCP hadi kuwazidi wengine.
Kwanza Deng alikutana na wahafidhina wale walioshiba ukomunisti haswa haswa kitu ambacho Deng alitaka kufanya mabadiliko namna ukomunisti wa China uwe ilikuwa patashika.

Kwa mfano Deng angekuwa Magufuli na mtindo wake wa kutusi na kuwakoromea wazee asingekubalika.

Kazi ilikuwa ngumu ile transition ya kutoka kwenye ukomunisti wa kale na kuja kwenye ukomunisti mpya huu wa wakina Deng Xiaoping alikutana na upinzani mkali humo humo chamani kwao

Hata mambo ya cultural revolution na Gang of four aliuona moto wao

Xi sikwamba hajakuna na changamoto amekutana nazo kama rushwa amejitahidi kusolve hilo ila jangamoto zake hazijafika level ya wakina Mao na Deng ukichanganya na cold war
 
Qatar wana watu wachache, nchi ndogo, na fedha nyingi. Hiyo ndio imewezesha kuwa na maendeleo. Wangekuwa nchi kubwa, na watu wengi, kama Nigeria pasingekalika.
Watu wengi hawaelewei hili, wanafikiria udikteta wa watawala wa nchi zenye mafuta uarabuni ndio umezisaidia sana hizo nchi.
Kinachozibeba familia za Kifalme uarabuni ni kwamba pesa wanazopata za mafuta na gesi ni nyingi sana kiasi kwamba wanajichotea za kwao kuwafanya mabilionea na bado zinabaki nyingi tu za kufanya maendeleo kwa raia.
 
Lakini Nigeria ina mafuta mengi pia hata Sudan
 
Udikteta ndio uliofanya Xi abadilishe katiba kwa kupata kura za wajumbe wote wa mkutano mkuu/congress(bunge). Mbunge katika bunge la Marekani anaweza kumtukana hata Biden na asifanywe chochote , Elon Musk anamtukana Biden na chama chake Marekani mara nyingi bila kufanywa chochote. Hakuna Mbunge anaweza kumpinga Xi China bila mkakati mpana na wa muda mrefu. Jack Ma aliyekuwa bilionea namba 1 China alijaribu kukosoa kwa mbali tu CCP wakomunisti wakamchukua wakamficha kwa muda aliporudi akawa anaimba Xi anaupiga mwingi na utajiri wake wakautikisa sasa hivi amepoa na kunywea kabisa.

Deng Xioaping hakubadilisha kwa sababu hakutaka na wakati huo kulikuwa na watu watata sana katika siasa za China kuliko walivyo leo hii. Hata Deng kuyapata madaraka ya China na kuwa mtawala kamili ilikuwa mtiti sio wa kitoto na palichimbika haswa ndani ya chama cha CCP hadi kuwazidi wengine.
Kuna sehemu nimecomment kuwa zipo factors ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa sana kuthrive kwa demokrasia Moja wapo ikiwa ni asili na historia ya jamii husika.

Kwa Marekani wameanza kufanya siasa za demokrasia ya kukosoana na kutukanana tangu enzi za Thomas Jefferson mwaka 1800s huko na hiyo imeshakuwa sehemu ya utamaduni wao....

Sasa kwa taifa kama la China ambalo kwa miaka mingi lilikuwa kama sisi tu na suala kukosoa kiongozi sio sehemu ya utamaduni waliouzoea, so obvious wewe ukileta mambo yako ya siasa za kimagharibi sijui unakosoa serikali lazima wakufinye utie akili.... Hizo ni distractions ambazo hazina ulazima,

Nafikiri unamkumbuka Magu😆😆😆 hakutaka kabisa distraction, wewe tulia hapo utengenezewe nchi basi, inaruhusiwa kukosoa pale unapoona serikali haitimizi wajibu wake na penyewe ni kwa nidhamu sio kuropoka tu.
 
Afrika tunastahili kuishi kama wanyama maana demokrasia na udikteta vyote vimefeli.
 
Nigeria Ina watu milioni 220, haiko hata kwenye nchi kumi zenye mafuta mengi duniani. Saudi Arabia ina watu milioni 36 ni nchi ya pili kwa mafuta duniani, Qatar ina watu milioni 2.7 ina mafuta na ni tatu kwa gesi duniani.
Mueleze pia Nigeria ilikuwa na madikteta kama Gen.Sani Abacha, na Gen.Ibrahim Babangida, lakini haikufanikiwa pamoja na rasilimali ya mafuta waliyobarikiwa nayo.
 
.
Kinachozibeba familia za Kifalme uarabuni ni kwamba pesa wanazopata za mafuta na gesi ni nyingi sana kiasi kwamba wanajichotea za kwao kuwafanya mabilionea na bado zinabaki nyingi tu za kufanya maendeleo kwa raia.
Na ndivyo jinsi madikteta wenye akili wanavyofanya hata kama ni walafi, basi wanawakumbuka na wanyonge... Familia ya Gaddafi enzi za uhai wake walikula sana Bata, watoto walijichotea sana mihela lakini pia baba yao w
aliboresha maisha ya wanainchi wa Libya.

Sasa viongozi wa CCM wanashindwa nini kufanya hivyo?

Kwa rasilimali zilizopo hapa nchini viongozi wa serikali ya CCM Wana uwezo wa kukwapua mabilioni ya pesa kadri watakavyo, wakati huo pia wanaboresha maisha ya Kila mtanzania kiasi Cha watanzania hao kutowaabugudhi kabisa watawala hao wa CCM.... Ila wanachofanya ni kufisadi mchinkwa sana huku wakizidi kuongeza ugumu wa maisha kwa watanzania, sababu ni nini hasa? Ni kukosa maarifa ya kiongozi au??
 
Back
Top Bottom