Kwanini Dar es Salaam magari binafsi aina ya Landcruiser V8 yako mengi sana?

Bro kuna watu wanalipwa mshahara zaidi ya mbunge wataachaje kumiliki magari kama hayo
 
Mtuache na V8 zetu na defender zetu..

Nyie mnazijua viiiieieee..[emoji318][emoji318]
 
Kwa akili yako ndogo ,kweli kwa Dar hilo ni jambo la kushangaza? Wakazi zaidi ya mil.5?

Pili kwa Dar sidhani kama wanaomiliki hayo magari wengi wao ni wafanyabiashara sio wafanyakazi japo nao wapo.

Huku mikoani nako wapo ila sio wengi na ni wafanyabiashara sio watumishi.
 
Bongo watu wana hela mzee wa kazi kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake..Ukiwa mtu wa kuweka rohoni yale unayoyaona Dar kila siku utaumia moyo wako cha msingi ridhika na ulichonacho

View attachment 2051683
Sio tuu magari, mimi huwa nikiona Mji ulivyojaa maghorofa halafu almost 90% ni ya watu binafsi hapo ndio huwa naona mikoani tunasindikiza maisha, so huwa sipendi kuja Dar.
 
Dar ni kitovu cha biashara, asilimia 90 ya shughuli zote ni za watu binafsi. Kuna watanzania zaidi ya 200,000 wenye zaidi ya 1m USDollars, yaani bilioni 2.3. Hivyo basi ata number ya V8 haitoshi, wengi ni mabahili.
Mkuu hata Africa nzima wenye $1m na kuendelea hawafiki 200,000. Tanzania wako kama 5,000 hivi.
 
Mkuu hata Africa nzima wenye $1m na kuendelea hawafiki 200,000. Tz wako kama 5,000 hivi.
Bro, means $1M kwa hapa Tanzania hawafiki hata laki moja??
Wachache hivyo, mbona naona idadi yako ndogo sana.

Japo sina mkwanja huo, ila naona madon wengi wapo ila kimya kimya wanakula mema ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…