Ni kweli mkuu ni kupambana na hali yako. Ukiishi masaki haya mambo ni ya kawaida. Gari za maana zote ziko masaki jamani.
Mwaka jana mwezi wa 6 tulipata msiba hapo masaki na covid ile watu walikuwa wanakuja kwa awam
Cha kushangaza nilikuwa naona kidada kidogo kama 20 yrs kinakuja kusalimia msiba kimevuta v8 ya maana. Wakitoka mi namuuliza mama anasema mtoto wa mama fulani kuleee mmh na unakuta sio familiya za viongozi wa serikali ni familiya za watu wa kawaida.moyoni najisemea watu wanaishi.😂😂😂
Kuna vitoto vingine vilikuja kusalimia msiba ahaaa mimi ndo nilifungua geti vinauliza mama yupo najibu ndio , mama kaja vikashuka na vikaputura vyao, vikasema mama pole na nsiba sisi hata hatukai tumetuma tu drop hapa hivi tu ahaaa hiyo chuma vilivyokuwa vikiendesha ilibidi tu nicheke.
So haya mambo yapo sana dar, ni kula kwa urefu wa kamba yako.