Kwanini Dar es Salaam magari binafsi aina ya Landcruiser V8 yako mengi sana?

Kwanini Dar es Salaam magari binafsi aina ya Landcruiser V8 yako mengi sana?

Yeah ni za mwanzo pre-orders hizo na zile ambazo zilikwishapelekwa Dubai! Kuagiza Japan hutoipata ziko Australia na Dubai ambako ndio masoko makubwa ya Land Cruiser!
Sawa chief,hizi LC 300 zenyewe zinatumia material gani mpk yamekua adimu mkuu?
 
Zile walisimamisha production Japan! Zinazalishwa Australia tu kwa sasa sababu material yalikuwa adimu!
Nmegundua kitu!

Australia wanazipenda sana toyota hasa hizi suv kubwa kubwa!

Hata hilux wana soko kubwa sana Australia sijui mazingira yao yanafanana na Afrika?
 
Sijajua watu wanafukua wapi hela, Kila cku huku dar Nakutana Na land cruiser v8 zenye condition nzuri tena Gari binafsi zenye Plate number d, najiuliza na hii mishahara midogo ya taasisi za kibongo ya laki 8 kwa mwezi, watu wanawezaje miliki Na ku-maintain gari ya Tshs million 80 - million 200 plus?

Anaenunua Toyota v8 kwenye account atakua na tsh ngapi? Ina maana hapa bongo Watu wengi kiasi ni matajiri?
ni kweli lkn nyingi pia ya hizo Vietii ni za kazi maalum hasa wazee wa Makumbusho!!
 
Nmegundua kitu!

Australia wanazipenda sana toyota hasa hizi suv kubwa kubwa!

Hata hilux wana soko kubwa sana Australia sijui mazingira yao yanafanana na Afrika?
Yeah Australia landscape yake ina miamba miamba sana mkuu! Pamekaa kama Upareni kule Mwanga mpaka Usangi.

Gari wanazopendelea ni 4*4 hasa za Toyota ndio maana kule LC series kuanzia 70 mpaka 300 sasa soko lipo hot! Achilia mbali hizo pickup za Hilux nazo zamoto sana kule.
 
Africa viongozi huku ni kama Miungu watu yani mtu akishapewa madaraka akili za kibinadamu anaziwacha pale anapoingia mlango wa ofisini tu😅!

Ni kujineemesha kwa kwenda mbele kwa kila fursa anayoona iko usawa wake yani na kejeli nyingi tu kwa wananchi sema tu ni vile tumeumbiwa upole ila kwa nchi ambazo wananchi ni vichaa upuuzi kama unaofanyika nchini hapa hawawezi uvumilia hata kwa week 1 tu lazma kiumane.

Yani mtu anafanya ufisadi kwenye hela za umma na still atatoa jibu jepesi tu akiulizwa na sababu ana backup ya askari anajua hatoguswa. Raisi nae unakuta wala hana habari na mtu😅
Ndo maana baada ya UHURU wakafata sera za ujamaa na ujamaa ukazaa udikteta.
Ujamaa na udikteta ni pacha Ili kuwadhibiti watawaliwa.
Thus awataki katiba mpya itawabana kuwatawala wananchi.
Afrika kuna watawala wenzetu hawana watawala Wana viongozi.
Thus huwezi kuta wanachezea kodi za wananchi.Watawala wa kiafrica baada ya kuzibomoa nchi zao wakawapropanda waafrika eti matatizo ya afrika yamesababishwa na wazungu lengo kuu ni kujificha na lawama ya aibu ya kudai UHURU kwa Mbwembe huku wakiwananga wakoloni baada ya UHURU tutakuwa mbali zaidi,wakaprovu failure mbaya sana mara mia ya mkoloni mwenyewe.Check mugabe,savimbi,banda nk ni wasomi wakubwa tu level ya phd wakazitumia vibaya phd zao kuzibomoa nchi zao zilizojengwa vizuri na wakoloni.
Always African leaders dies in foreign hospital hii ni shame sababu awaboreshi mifumo ya Afya ya nchi zao checkup na matibabu nje.
Hata mwendakuzimu alifia nje.
 
Yeah Australia landscape yake ina miamba miamba sana mkuu! Pamekaa kama Upareni kule Mwanga mpaka Usangi.

Gari wanazopendelea ni 4*4 hasa za Toyota ndio maana kule LC series kuanzia 70 mpaka 300 sasa soko lipo hot! Achilia mbali hizo pickup za Hilux nazo zamoto sana kule.
Alafu mbongo kutoka buza anadharau toyota eti ni ya watu masikini!
 
Yeah Australia landscape yake ina miamba miamba sana mkuu! Pamekaa kama Upareni kule Mwanga mpaka Usangi.

Gari wanazopendelea ni 4*4 hasa za Toyota ndio maana kule LC series kuanzia 70 mpaka 300 sasa soko lipo hot! Achilia mbali hizo pickup za Hilux nazo zamoto sana kule.
True Australia hali ya hewa na mazingira ni kama Afrika.
 
Hata hilux wana soko kubwa sana Australia sijui mazingira yao yanafanana na Afrika?
[/QUOTE]

Australi linchi likubwa saaana....na majamaa yanapenda sana Adventures na safari.....
 
Mkuu kama nchi tupo watu mill 60 unadhani hizo viieite ulizoona hapo Dar zinafika hata 1mill?

Halafu zipo pia za mchongo refer kesi ya sabaya ile aliinunua kwa mwarabu 60mill mpaka ikaja kujulikanika kwamba jamaa alikuwa na houseboy shoga.
Embu iweke vizur hiki kipande,ni nan alikuwa na houseboy shoga?

"Halafu zipo pia za mchongo refer kesi ya sabaya ile aliinunua kwa mwarabu 60mill mpaka ikaja kujulikanika kwamba jamaa alikuwa na houseboy shoga."
 
Utajiri ni mchanganyiko wa mambo mengi mkuu, positive mindset, determination, capital, risking. Kwenye capital ndio kuna mgawanyiko hapo; human capital na financial capital!

Ndani ya human capital kuna swala linaitwa connections. Askari,Wanajeshi,Matajiri,Wakurugenzi na zaidi ya hao.

Financial capital ndio pesa yenyewe sasa. Hapa ni hela ama cash money.Ukisikia pesa inaleta pesa ndio hivyo sasa usidanganyike na vitabu vya rich dad poor dad utachelewa maisha ni real sio story.

Ukivikosa hivyo ama ukawa huna access navyo jua utaendelea kuwa kapuku tu. Utajiri hauji kama hauna hivyo vitu hapo. Labda urithishwe mali kama Mo Dewji!
True kama wewe ni masikini jitahidi umiliki information, kama una information tayari ni pesa.Mwenye pesa anataka information Ili aingize pesa.
Information kuhusu marketing,raw materials, suppliers,nk unampatia muhitaji then anakupa pesa au kuingia ubia kwa kumuuzia information.Mfano wapi kuna mifugo,mazao bei rahisi ukiyaingiza mjini au nje pesa ipo.Au kipi kinapendwa vijijini tokea mjini unamfata mwenye navyo unapeleka mjini.
Mfano vijijini ndizi mkungu elf 4 Dar elf 25 hadi 30 mtu ana eka tatu kijijini ana link na muhitaji mjini.Wewe una information mhitaji na mkulima hawana information wapi watimize ndoto zao.
So wewe unakuwa mtimiza ndoto zao.
 
Kwa jiji la kibiashara kama Dar si jambo la kushangaza, labda huko mikoani ndo unaweza kukuta ipo ya mkurugenzi na mkuu wa mkoa.
 
Back
Top Bottom