Kusena
JF-Expert Member
- Aug 25, 2020
- 278
- 169
Naomba nikujibu hili japo ningetamani kuongea na wewe kwa simu. ANYWAY TWENDE KWENYE JIBU SASA[emoji120][emoji120]Maneno mengi hauna hoja hata moja,
Lete ushahidi jumapili ni siku ya sabato/ ya kuabudu
JUMAPILI NI SIKU YA KUABUDU? NA JUMAMOSI NI SIKU YA KUABUDU?
JIBU: Ndio jumapili ni siku ya kuabudu na hata jumamosi ni siku ya kuabudu.
Bila shaka Mimi na wewe tunaamini jumapili ni siku ya Kwanza ya juma na jumamosi ni siku ya Saba ya juma.
Kama ni kweli basi iwe hivyo twende kwenye andiko
Kutoka 12:16
Siku ya kwanza kutakuwa kwenu na kusanyiko takatifu, na siku ya saba kutakuwa kusanyiko takatifu; haitafanywa kazi yo yote katika siku hizo, isipokuwa kwa hiyo ambayo kila mtu hana budi kula, hiyo tu ifanyike kwenu.
Katika kutoka 12:16 inaonesha wazi kua kuna kusanyiko takatifu siku ya Kwanza ya juma na siku ya Saba ya juma kwa maana hiyo j.pili na pia jumamosi. Je SDA mnalo hili au na ninyi ni dhehebu mlioacha Neno?
Pia
Mambo ya Walawi 23:7
Siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu msifanye kazi yo yote ya utumishi.
Hapa pia tunaona katika siku ya Kwanza unaona hili ambayo siku ya Kwanza ni jumapili.
JIBU HILI LISIWAFANYE WAKATORIKI KWAMBA WAPO SAWA NA NENO HAPANA WAO WAMELIACHA NENO TANGU MWAKA 325 KWA KUINGIZA MAFUNDISHO MENGI AMBAYO YANAPINGANA NA NENO LA MUNGU.