Kwanini dhehebu la SDA huwa wanalishambiulia zaidi Kanisa Katoliki na siyo madhehebu mengine?

Kwanini dhehebu la SDA huwa wanalishambiulia zaidi Kanisa Katoliki na siyo madhehebu mengine?

Ufuasi wa dhehebu unatokeaje? Ufuasi wa dhehebu unatokea pale unapojiunga na dhehebu.
Mkristo hajiungi na dhehebu ama kanisa maana akifanya hivyo atatetea hilo kanisa hata kama limeenda chaka.
MKristo anazaliwa kwa Neno la Mungu na yeye daima atalitetea neno la Mungu bila kujari chochote kile


Kuhusu WAKATORIKI kutumia biblia. Kwanza tunatakiwa kufahamu biblia inasema kwamba halitakiwi kuachwa hata Neno moja Wala si ruhusa kuongeza. Kwa maana hiyo naamini bible ni Neno la Mungu na Mungu ni Neno. Hivyo ukiacha ama kuongeza huko ni kutokutumia bible ndivyo ilivyo Leo kwa catholic na madhehebu mengine wameacha NENO LA MUNGU Lakini kwa kujiongezea mafundisho Yao kwa mfano ;mwanamke kuhubiri, kunena kwa lugha bila kua na mfasiri, ubatizo wao ulivyo tofauti na ule wa mitume, kuwaomba wafu na maraika, n.k
Ni mapokeo na jinsi madhehebu yanavyotafsiri biblia mkuu.
Kila mmoja humuona mwenzie anakosea na yeye yupo sahihi zaidi.
Na ukizingatia hawafanyi hayo nje ya bible ila kuna vifungu kila mmoja anaondoka na tafsiri yake, kama ulivyo ubishani wa najisi, siku ya sahihi ya kuabudu, kunena kwa lugha n.k

Pale aya ya kwanza umeandika vyema sana.
 
Sijawahi kuona mkatholiki akikashifu au kukosoa dini za wengine ila wengine ndio huwa wanakashifu. Kwa misingi hii, hakuna vita hapa zaidi ya shambulio
True ndio huwa naona niko sehemu sahihi
Hao wenzetu mahubili yso ni kuponda dini nyingine huwa naona dini za ajabu sana
 
USICHOKIFAHAMU KUHUSU BIBLIA NA UKRISTO: JE! UNAJUA NINI KILITOKEA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 400 YA UKIMYA KATI YA AGANO LA KALE NA AGANO JIPYA?

Ukristo ni neno linalotumika kuelezea watu wanaomfuta Yesu Kristo ambao wako katika Makanisa na madhehebu yanayotumia Biblia kama Maandiko yao Matakatifu. Kwa ujumla Biblia ni sehemu ya Maandiko Matakatifu yanayotambuliwa pia kama Maandiko Matakatifu katika Dini ya Kiyahudi ambayo ni vitabu vya Historia, Unabii, Hekima, na Ushairi. Katika Ukristo, vitabu vya Injili, Nyaraka na Ufunuo vimeongezeka wakati vitabu hivyo havipo katika Dini ya Kiyahudi. Hata hivyo, kuna vitabu kadhaa ambavyo viliandikwa katikati ya Agano Jipya na Agano la Kale.

Biblia imegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni Agano Jipya na Agano la Kale. Kipindi cha Agano la Kale kinakoma:

1. Wakati Waashuru (Assyrians) walipoivamia Israeli ya Kaskazini na kuwapeleka Utumwani

2. Wakati Wakaldayo (Babeli) walipoivamia Israeli ya Kusini (Yuda) na kuwapeleka Utumwani Babeli

3. Wakati baadhi ya mateka (exiles) walipoanza kurejea Yuda wakati wa Utawala wa Waajemi. Wayahudi hao waliongozwa na Ezra, Nehemia, nk. (Soma vitabu vya Ezra na Nehemia).

Matukio yote hayo matatu yaliyoashira mwisho wa kipindi cha Agano la Kale yalitukia katika Karne ya Sita na Karne ya Tano Kabla ya Kuzaliwa kwa Yesu Kristo (KK). Na huo ndio uliokuwa mwisho wa Uandishi wa Vitabu vinavyounda Agano la Kale ambapo katika Biblia, Kitabu cha Mwisho cha Agano la Kale ni Kitabu cha Nabii Malaki.

Tangu wakati wa Malaki hadi wakati wa Kuzaliwa kwa Yesu, kuna utofauti wa muda wa zaidi ya miaka 400 au Karne Nne. Kipindi hicho cha katikati cha miaka 400 ndicho ambacho Wataalamu wa Historia ya Kanisa na Wataalamu wa Theologia hukiita kwa majina tofauti tofauti kama:

1. Kipindi cha Miaka 400 ya Ukimya (The 400 Silent Years) - Kwa sababu katika kipindi hicho cha miaka 400 kulikuwa na ukimya wa Sauti za Kinabii; na pia kwa sababu ya kutokuwepo kwa kumbukumbu ya vitabu vya Biblia (the gap of the Biblical records).

2. Kipindi cha Katikati ya Maagano (The Intertestamental Period or Between The Testaments) - Kinaitwa hivyo kwa sababu ya kutenganisha Kipindi cha Agano la Kale na Kipindi cha Agano Jipya.

Katika kipindi hicho cha miaka 400, ndicho kipindi ambacho Iskanda Mkuu (Alexander the Great) alikuwa ndiye Mkuu wa Mashariki ya Kati kwa kuwashinda Waajemi katika mapigano makali ya Granicus (334 KK), Issus (333 KK), na Arbela (331 KK). Kipindi hicho ndicho ambacho utamaduni wa Kiyunani (Kigiriki) ulioitwa Uheleni (Hellenism) ulianza kuenea kupitia biashara na makoloni ya Kigiriki. Lugha ya Kigiriki ndiyo iliyokuwa Lugha ya Ulimwengu (lingua franca), Lugha ya Biashara na Lugha ya Kidiplomasia.

Kipindi hicho kilikuwa na mapambano makali ambapo Wamisri na Waashuru walikuwa wakipambana kuliteka eneo ambalo sasa ndio Israeli/Palestina. Lakini Wamisri wakashindwa na Mgiriki aliyeitwa Antiochus III (198 KK). Katika kipindi hicho kuliibuka makundi au madhehebu mawili ya wapigania Uhuru ya Kiyahudi nayo ni Nyumba ya Oniasi - hawa walikuwa wakiungwa mkono na Wamisri; na kundi la Nyumba ya Tobiasi - hawa walikuwa wakiungwa mkono na Wasiria (Syrians).

Mgiriki aliyeitwa Antiochus IV alipoingia madarakani, alitaka kuendesha au kudhibiti Dini ya Kiyahudi kwa kumuondoa Kuhani Oniasi III na kumuweka Jason ambaye alikuwa upande wa Magiriki aliyetaka kuufanya Yerusalemu kuwa Mji wa Kigiriki. Hayo na mambo mengine ndiyo yaliyowakasirisha Wayahudi na kuzua Vita ya Makabayo iliyoongozwa na Juda aliyepewa jina la utani la Makabayo likiwa na maana ya nyundo!

Ufame wa Kirumi uliokuwa umeanza Karne Nane kabla wakati Rumi ilipoanza kama Jamhuri uliendelea kukua taratibu baada ya kuiteka Carthage (sehemu ya Algeria na Tunisia mwaka 146 Kabla ya Kristo (KK) na baadaye Pompey kuiteka Mashariki ya Mediterania na Julius Kaisari kuiteka Gaul (Ufaransa). Baada ya Julius Kaisari kuuawa, Octavian ambaye baadaye alijulikana kama Mfalme Augusto aliwashinda wapinzani wake Wakuu ambao ni Anthony na Malkia Cleopatra katika mapambano ya Pwani ya Actium, Ugiriki mwaka 31 Kabla ya Kristo (KK).

Mfalme Augusto alitawala hadi mwaka 14 Baada ya Kristo (BK) na ndiye aliyeamuru kufanyika kwa Sensa wakati ule Yesu anazaliwa (Luka 2:1-7). Wakati wake, Sensa ilifayika mara mbili. Ya kwanza ilikuwa kutoka mwaka 6 hadi 4 Kabla ya Kristo na Sensa ya pili ilifanyika kutoka mwaka 6 hadi 9 Baada ya Kristo. Ni kwa sababu hiyo, Yesu anakadiriwa kuwa alizaliwa kati ya mwaka 6 hadi 4 Kabla ya Kristo (KK). Changamoto ya miundombinu ya wakati ule ilipelekea Sensa kufanyika kwa kipindi cha miaka miwili.

NB: Kumbukumbu nyingi kuhusu kipindi hicho cha miaka 400 hazimo katika Biblia bali zinapatikana katika vitabu vya Apocrypha kama Makabayo, Tobiti, Danieli na Susana (Sura ya 13 ya Danieli, Judith, Waraka wa Yeremia, nk. Kwa ujumla, kuna vitabu zaidi ya 105 vinatambulika kama sehemu ya Biblia. Kati ya hivyo, Waprotestanti wanavitambua 66, Roman Catholic wanavitambua 73, Orthodox Catholic Church wanavitambua kama 85, Kanisa la Syria hutambia vingi zaidi.

Je, ni jambo gani limekushangaza? Tuwe wapole kwa kuwa hakuna dhehebu linaloweza kujivuna kuwa linamiliki kweli yote. Anayemiliki kweli yote ni Mungu peke yake!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula ambaye ndiye mwandishi wa makala hizi, ni Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani. Pia, ni Mhadhiri wa Theologia, Falsafa, Soshologia, Literature, Missiologia, Ecclesiologia (Historia ya Kanisa) na Utafiti. Amefundisha masomo hayo kwa miaka kadhaa katika Chuo Kikuu, St. John's University of Tanzania
 
HISTORIA YA KANISA IV: MARTIN LUTHER NA VISABABISHI VYA MATENGENEZO YA KANISA - 1.
Sababu zilizopelekea Matengenezo ya Kanisa (the Reformation) zilikuwa ni nyingi na zilianza hata kabla Martin Luther hajazaliwa. Nitakuwa nikieleza moja baada ya nyingine. Leo nitagusia mgogoro wa kiuongozi uliodumu kwa miaka 39.
Mgogoro huo wa uongozi ulilipasua Kanisa hadi kuwa na Mapapa 3 kwa wakati mmoja. Papa Urban VI alichaguliwa mwaka 1378 kuwa Askofu Mkuu wa Roma na hivyo kuwa Papa. Miezi michache baada ya kuchaguliwa kwake aliwaweka kando Nyumba ya Makadinali (College of Cardinals). Baada ya kuona kuwa wamepuuzwa na kuwekwa kando, Makadinali wa Ufaransa na wengine waliondoka Roma na wakatangaza kuwa uchaguzi wa Papa Urban VI ulikuwa batili (kwa maneno mengine walibatilisha uchaguzi)!Baada ya hapo Makadinali wale walimchagua Kadinali Robert wa Geneva kuwa papa na kujulikana kama Papa Clement VII. Papa Urban IV aligoma kuondoka Roma (ofisini) hivyo Papa Clement VII pamoja na Makadinali wake walihamia Avignon, Ufaransa na hivyo Kanisa la Roman Katoliki lilikuwa na Mapapa wawili kwa wakati mmoja kila mmoja akijiona kuwa ndiye Papa kwa kuwa kila mmoja alikuwa na idadi ya Makadinali waliokuwa wakimuunga mkono.
Mtaguso Mkuu wa Pisa uliofanyika mwaka 1409 uliazimia kumaliza tatizo kwa kuwafukuza Mapapa wote wawili na badala yake akachaguliwa Papa Alexander V. Mapapa wale wawili kila mmoja alikataa kujiuzulu na hivyo kukawa na Mapapa watatu!
Mtaguso Mkuu wa Constance uliitishwa mwaka 1414-1418 ulihudhuriwa na Makadinali, Maaskofu Wakuu, Maaskofu, Wakuu wa Vyuo nk. Mfalme wa Dola ya Kirumi alimshawishi Papa mmojawapo ili aitishe Mtaguso Mkuu. Yule Papa alifanya hivyo akijua kuwa yeye angepona. Matokeo yake alichaguliwa Papa mwingine kabisa baada ya wote watatu kutolewa. Papa mpya aliitwa Martin V. Mara tu baada ya kuchaguliwa Papa Martin V alijitangaza kuwa juu ya Mtaguso Mkuu wa Kanisa! Katika kipindi chote hicho, Mapapa walikuwa katika magomvi ya madaraka hivyo mambo ya kiroho yaliachwa kando na kulikuwa na mmomonyoko mkubwa wa maadili miongoni mwa Mapadre na watawa hasa ikizingatiwa kuwa Mapapa wenyewe walikuwa wamekosa uadilifu. Katika kipindi hiki ndipo Padre Profesa John Huss alianza kuhubiri uamsho (matengenezo). Cha kusikitisha ni kwamba Mtaguso wa Constance ndio uliomhukumu kifo. Wafuasi wake waliendelea na uamsho (matengenezo) na hatimaye walianzisha Kanisa la Moravian.
Martin Luther alikuja miaka 100 baadaye.

Mwanakondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania.
 
Kwa sababu nyingi,miongoni mwanzo ni katoliki ni dini dhaifu kimisingi hata kwa biblia,yaani Haina uhusiano wowote na biblia,pili wakatoliki hawasomi,hawawezi Jenga hoja dhidi ya mtu,hawajui chochote ni kondoo

Ni kweli ndio maana ni ngumu kukuta jamii iliyojaa wakatholiki ikawa na mikwaruzano au umaskini wa kupitiliza kwa sababu ukatholiki unahubiri upendo kwa watu wote pasipo kujali misingi ya imani yao lakini pia ukatholiki, unakumbatia elimu dunia na maisha nje ya imani..

Hizi ndizo sababu, mkatholiki lazma awe mtu peace asiyebagua watu na sio kama wengine wanaojazwa sumu hadi kuona wanamiliki milango ya pepo huku wakitumia Bible kusambaza chuki tofauti na Yesu mwenyewe, aliyehubiri upendo kama amri kuu tena kiasi cha kukaa na wadhambi ili wapate kuokolewa.
 
JE, NAMBA 666 INAMHUSU PAPA?
Hili ni moja ya maswali yaliyopatwa kuulizwa na kujibiwa na Waseminari wa Seminari Kuu ya Peramiho kwenye Kipindi cha IJUE BIBLIA-REDIO MARIA
Swali hili limeulizwa na watu zaidi ya mmoja, kwanza limeulizwa na Catheline Lacha, yeye anauliza hivi; Kitabu cha Ufunuo kinamaanisha nini juu ya namba 666? Na je, Kaisari Nero aliyewatesa Wakristo wa mwanzo anahusianaje na namba 666? Pili, limeulizwa na makatekista wa Dekania ya Konsolata-Iring
a wakisema; Tunaomba tupate maelezo juu ya namba 666 inayozungumziwa katika kitabu cha Ufunuo. Tatu, limeulizwa na wana TYCs wa Songea Boys wakisema; Kitu gani kinaonesha kwamba maneno NERON KAISAR alikuwa memba wa Freemason? Na je, ni kweli herufi hizo zipo katika kofia ya Papa? Na zina maana gani?
Wapendwa mliouliza swali hili, napenda niwapongeze kwa swali lenu zuri kabisa, ambalo limeulizwa mara nyingi na kujibiwa mara kadhaa na wataalamu wa Maandiko Matakatifu. Hata hivyo tutalijibu ili tuendelee kuifahamu vizuri Biblia Takatifu na kujiimarisha katika imani yetu Katoliki. Na hivi naomba tufuatane kwa makini ili tupate kueleweshana na kuwekana vizuri kabisa, kwani siyo ninyi tu mnaopatwa na utata huo, wapo wengine ambao wao wamevuka mipaka ya kuuliza, wakuamua kutoa shutuma kwamba namba hiyo 666 inamhusu Papa au Baba Mtakatifu na imeandikwa kwenye mavazi yake, kitu ambacho si kweli kabisa.
Wapendwa wauliza swali, nanyi wasikilizaji wote wa Redio Maria, kimsingi swali hili ni moja lililoulizwa kwa namna tofauti tofauti, kwani linahusu namba 666 iliyoandikwa katika kitabu cha Ufunuo sura 13:18, na hivi naomba nitoe majibu ya pamoja kwa maswali yote matatu. Basi, namba yenyewe 666 inapatikana katika kitabu cha Ufunuo sura 13:18, hapo imeandikwa hivi; “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita” (Ufu 13:18).
Mpenzi msikilizaji wa Redio Maria, kwa nukuu hiyo mwandishi wa kitabu cha Ufunuo alimaanisha jina la kiongozi wa dola ya Kirumi zamani zile, yaani Kaisar Nero. Hivi ni kweli kwamba Kaisar Nero aliyewatesa Wakristo wa mwanzo, anahusika moja kwa moja na namba 666, kwani namba hiyo ni hesabu ya jina lake ukikokotoa kwa kigematria, maneno NERON KAISAR kwa Kiebrania.
Hivyo namba hiyo, 666 ilimhusu na bado inamhusu kiongozi huyo wa dola ya Kirumi zamani zile na wala siyo kiongozi mwingine kama Baba Mtakatifu, na wala haikuandikwa kwenye mavazi yake, kama wanavyodai wale ambao wanasoma kwa makengeza kitabu cha Ufunuo, huku wakiwa na mawazo yao binafsi.
Na pia kinachoonesha kwamba Neron Kaisar alikuwa ni memba wa Freemasoni ni namba hiyo 666 ambayo ni namba ya Freemasoni na kuhusu suala la kuwatesa Wakristo na kutaka kuangamiza Ukristo ambalo ndilo lengo la Freemasoni pia.
Wapendwa wauliza swali, ili tuelewe vizuri sura hiyo ya 13 ya kitabu cha Ufunuo, ni vema na haki kabisa, tuzingatia kwamba kitabu cha Ufunuo wa Yohane, kina mazingira yake ya kihistoria ambayo ni muhimu kuyaelewa vizuri katika kujibu swali letu hili, na mazingira hayo ni ya historia ya dola ya Kirumi.
Mpenzi msikilizaji wa Redio Maria, kama nilvyosema ili tuelewe vizuri majibu yetu, hebu tutazame kwa kifupi maana, sifa na mazingira ya kitabu hiki cha Ufunuo. Ufunuo wa Yohane ni maandishi ya “kiapokaliptiko”. Apokalipsisi ni neno la Kiyunani lenye maana ya Ufunuo. Na hivi maandishi yote ya kiapokaliptiko ni aina ya ufunuo, kwani Mungu humfunulia mtu fulani mambo yaliyofichika ambayo mpaka sasa yamejulikana na Mungu tu. Mambo hayo yanahusiana hasa na siku za usoni. Si rahisi kuona hitirafu kati ya ufunuo waliojaliwa manabii na vitabu vya kiapokaliptiko.
Tofauti ni kwamba manabii wa zamani waliyasikia maneno ya Mungu na kuyakariri walipoyahubiri. Kumbe waandishi wa funuo za kiapokaliptiko hupewa funuo zao kwa njia ya njozi, na hatimaye huziandika njozi hizo katika vitabu fulani. Waandishi wa funuo za kiapokaliptiko huona njozi za mifano, hawaoni tukio lenyewe la siku za usoni. Hivyo mambo yote hufahamika katika njozi kama mfano wa kitu kingine. Kwa mfano huona vitu mbalimbali kama tarakimu, viungo mbalimbali vya mwili, wanyama na watu, na vinginevyo vinavyotajwa.
Hivi kitabu cha Ufunuo ni kitabu chenye habari zilizofunuliwa kwa mwandishi juu ya mipango ya siri za Mungu. Maandishi haya ya “ufunuo” yanapatikana pia katika Agano la Kale, kwa mfano katika kitabu cha nabii Danieli 7-12; Ezekieli 26-35 na Zekaria 9-14). Basi, kwa kawaida vitabu vya Ufunuo vinazingatia mfumo maalum wa uandishi wenye vipengele vifuatavyo; Mosi, utumiaji wa jina bandia, yaani mwandishi hajitambulishi kwa jina lake halisi, bali hutumia jina la mtu maarufu aliyeishi enzi za kale. Pili, maono, ni katika mazingira ya maono au ndoto mwandishi anapata fursa ya kuona siri za mipango ya Mungu.
Tatu, utumiaji wa ishara. Ni vema tujue kuwa, vitabu vya Ufunuo hutumia ishara mbalimbali kuwakilisha au kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa watu. Na katika kitabu cha Ufunuo wa Yohane kuna ishara za aina tatu, nazo ni; Mosi, ishara za vitu: kama macho (19:2), pembe (12:13), kiti cha enzi (4:4), kanzu ndefu (28:4), mabawa (4:8), lulu (17:4), upanga (6:4).
Aina ya pili ya ishara ni nambari. Nambari zinazotajwa mara nyingi katika Ufunuo wa Yohane ni namba nne (7:1), namba saba (1:12), namba kumi (2:10) na namba kumi na mbili (21:12). Aina ya tatu ya ishara ni rangi ya vitu kama nyeupe (3:5), nyekundu (6:4; 17:3-4). Nne na mwisho ni maelezo ya ishara. Maana ya ishara hutolewa na malaika wa Mungu kwa yule anayepata maono. Tano, mpangilio maalum wa mada. Mada moja hurudiwa mara kadhaa katika mtiririko uleule, lakini kila mara kwa kutumia lugha na ishara tofauti.
Na walengwa wa kitabu hiki cha Ufunuo walikuwa ni Wakristo walioteswa vikali kwa sababu ya imani yao (2:10). Baadhi ya waamini walikwisha kumwaga damu kama mashahidi (2:13; 6:9; 20:4). Madhulumu hayo yaliendeshwa rasmi na vyombo vya dola ya Kirumi. Kihistoria inajulikana kwamba watawala wa dola ya Roma walioitwa Makaisari waliwadhulumu sana waamini Wakristo kutokana na imani yao. Na Kaisari Nero aliyetawala tangu mwaka 54BK hadi 68BK alikuwa wa kwanza kuendesha madhulumu dhidi ya Wakristo walioishi mjini Roma.
Kiongozi mwingine aliyeendesha madhulumu ni Kaisari Domitiani aliyetawala kati ya mwaka 81BK na 96BK. Huyo alikuwa mtu katili sana na alijihisi ana hali za kimungu. Na hivi raia wote katika dola yake walipaswa kuungama kama kanuni ya imani maneno haya: “Kaisari ndiye Bwana.” Na pia wakati Domitiani alipoingia katika ukumbi wa mkutano, wote waliokuwemo ndani walitakiwa kumsalimu kwa maneno haya; “Salamu kwako wewe Bwana wetu na kwa mkeo.”
Na hivi Wayahudi na Wakristo waliokataa kumtii Domitiani waliadhibiwa vikali sana, na Wakristo waliokataa kutolea sadaka kwa heshima ya Domitiani ndiyo waliolazimika kumwaga damu yao, yaani kufa kifo cha kishahidi. Katika hali hiyo kuzingatia dini ya Kikristo iliyokataa kabisa kumtolea sadaka mwanadamu mtawala lilikuwa jambo la kijasiri na fundisho kwetu kuwaabudu na kuwasujudia wanadamu kwani hiyo ni heshima anayestahili apewe Mungu pekee.
Basi, Wakristo walipokuwa wakidhulumiwa na dola hiyo, mtume Yohane alichukua kalamu na kuandika ujumbe wa matumaini ili kuwaliwaza, kuwapa nguvu, na kuwafariji ndugu zake waliokuwa wakiteseka pamoja naye, chini ya utawala wa Kirumi.
Maandiko Matakatifu yanasema hivi, “Mimi Yohane, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme, na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu.
Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana, nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu, ikisema, haya uyaonayo uyaandike katika Chuo, ukayapeleke kwa hayo Makanisa saba’ Efeso, na Smirna, na Pargamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia” (Ufu 1:9-11).
Basi ndugu zangu, wakati Yohane anandika kitabu hicho, akawa anatumia lugha ya mafumbo, ili kusudi watesi wao wasifahamu wanayosemwa na kumwangamiza. Ndipo basi, utaona kisa cha joka kuu lenye pembe kumi na vichwa saba na juu ya vichwa vilemba saba nakadhalika. Katika maapokeo ya Wayahudi joka ni mfano wa kila enzi mbaya na adui wa Mungu na wa taifa lake, ndipo hapa, joka linamaanisha dola ya Kirumi, na mkubwa wa dola ya Kirumi naye akapewa jina la kupachikwa, ua jina la kupanga, yaani jina la kifumbo kwa mtindo wa kucheza na namba za jina lake ambapo tumesema ukikokotoa kigematria kwa Kiebrania unapata namba 666.
Mpenzi msikilizaji wa Redio Maria, ili kuonesha maana ya sura 13:18 ya kitabu cha Ufunuo na namna namba 666 inavyohusiana na Neron Kaisar aliyewatesa Wakristo wa mwanzo, nakualika tuone kwa pamoja ufafanuzi au tukokotoe kigematria hesabu ya jina hilo inayohesabiwa kwa konsonanti za Kiebrania NERON KAISAR.
Hapa katika maneno hayo mawili, Neron Kaisar, zipo herufi N-ambayo kwa Kiebrania ni Nuni, nayo thamani yake ni 50, ipo herufi R-ambayo kwa Kiebrani ni Reshi, nayo thamani yake ni 200, kuna herufi W-ambayo kwa Kiebrania ni Vavu, nayo thamani yake ni 6, ipo herufi Q-ambayo kwa Kiebrania ni Kofu, nayo thamani yake ni 100, na pia ipo herufi S-ambayo kwa Kiebrania ni Sini, ambayo thamani yake ni 60.
Na hivyo hesabu yetu inakuwa kama ifuatavyo; NERON KAISAR linazo herufi za Kiebrania
N(50)+R(200)+W(6)+N(50)+Q(100)+S(60)+R(200)=(666), na jumla yake ndiyo tunapata namba 666.
Basi pia ukikokotoa kigematria kwa maneno ya Kigiriki KAISAR THEOS, yaani Kaisar Mungu pasipo kuzungukazunguka utapata namba 616. Hii tafsiri ya KAISAR THEOS, yaani Mungu Kaisari ndiyo inayopatikana kwenye Biblia zile zenye kuandika jumla ya namba 616.
Lakini vile vile 616 inaweza kupatikana kwa kuondoa konsonanti N, ya mwisho kwenye jina Neron Kaisar katika Kiebrania kama tulivyokokotoa wote hapo awali. Hivyo basi ukikokotoa kigematria kwa kutumia konsonanti za Kiebrania NERON KAISAR, yaania Kaisari Neron unapata jumla ya namba 666 na ukikokotoa kigematria kwa Kigiriki maneno KAISAR THEOS, yaani Mungu Kaisari utapata jumla ya namba 616.
Hivyo ndugu yangu ukishaelewa kukokotoa kigematria jina hilo Neron Kaisar huwezi kupata shida na kuwabambikizia wengine jina lisilo lao. Na hivi kwa Wakristo wa mwanzo namba 666 au 616 ilipomtaja Neron Kaisar, ilisema pia kwamba ni mpinga Kristo kwani alikuwa ni kunyume cha ukamilifu. Unajua ukitazama kinambari kwa Wakristo utimilifu ni namba 777, nayo inapatikana ukikokotoa kigematria jina la Yesu, kumbe kwake yeye Neron namba yake ni pungufu ya ukamilifu, kwani hesabu yake ni 666 ambayo ni 777 ya ukamilifu kutoa 111. Na hivi kwa kuzingatia maelezo hayo, namba 666 inasimama badala ya Neron Kaisar na siyo mtu mwingine kama Baba Mtakatifu kama wengine wanavyosema.
Mpenzi msikilizaji wa Redio Maria na kipindi hiki cha Ijue Biblia, katika kusoma Biblia Takatifu, hakuna mahali popote ambapo msomaji ameombwa kutumia akili isipokuwa katika kitabu cha Ufunuo hususani sura ya 13:18, kwa kuwa ili kuipata hesabu hiyo kunahitaji mtu atumie au achezeshe ubongo ipasavyo, yaani akokotoe kigematria, na hivi wasomaji wote wa kifungu hiki, walialikwa na hivi hata sisi leo tunaalikwa kutumia akili katika kupiga hesabu hiyo. Ndiyo maana Maandiko Matakatifu yanasema hivi, “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo, maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita” (Ufu 13:18).
Kumbe ndugu zangu, kinyume na matumizi ya akili, katika kifungu hiki, basi ndipo utakapoona wasomaji wengi “huingia mkenge” au hupoteza vichwa, yaani wasomaji wasipotumia akili zao hupotea na kushindwa kuelewa maana yake na hatima yake huishia katika ulalamishi, ubishi na utoaji wa majungu na uzingiziaji tu. Basi msikilizaji wangu, nakualika usomapo kitabu cha Ufunuo, sura 13 aya 18, utumia akili ili nawe usipotee katika kuelewa ujumbe wake ipasavyo.
Hapa wapo watu chungu nzima waliosoma kifungu hicho kwa makengeza ya akili zao, na hivyo kushindwa kuelewa maana yake na kuanza kueneza tafsiri potofu ama tafsiri isiyo sahihi ya namba 666, kwamba inamhusu kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, yaani Baba Mtakatifu na imeandikwa kwenye mavazi yake, kitu ambacho siyo kweli, kwani ni namba ya jina la Kaisar Neron aliyekuwa kiongozi wa dola ya Kirumi wa zamani zile, aliyewatesa Wakristo wa mwanzo.
Mpenzi msikilizaji wa Redio Maria, tukiendelea kujibu swali letu, naomba tujiulize, hivi ni nani, katika karne ya kwanza aliyekuwa adui wa Wakristo na jina lake linazaa namba 666? Bila shaka kama tulivyosema, alikuwa ni Kaisar Neron ambaye ukikokotoa kigematria jina lake unapata namba 666.
Tukitafsiri Biblia kwa usahihi huo, tunaona kuwa mtesi wa walengwa wa kitabu cha Ufunuo, aliyekuwa akifumbiwa katika sura 13:18, kwa hesabu ya jina lake kigematria, hawezi kuwa mtu wa karne ya tano au ya ishirini na moja. Ukweli ni kwamba walengwa wa kitabu cha Ufunuo walikuwa ni Wakristo wa karne ya kwanza na adui yao mkubwa alikuwa akiishi pamoja nao katika wakati huo, naye si mwingine bali ni Kaisar Neron.
Na hivi lengo la kitabu cha Ufunuo lilikuwa ni kuwatuliza waamini katika mateso yao, kuwahimiza waendelee kuzingatia imani yao. Kitabu kizima kinasema hivi, kwa kifupi, licha ya madhulumu makali mnayopata sasa hivi, hatimaye mtashinda. Muwe waaminifu kwa Yesu Kristo ambaye pia alimwaga damu yake, hivyo nanyi msikubali kusalimu amri inayowataka kumwabudu binadamu, kwani siku itafika Mungu atakapowaadhibu wale maadui zao.
Hapa, Wakristo waliyakumbuka maneno ya Yesu yaliyopo katika Injili ya Yohane sura 16:33, alipowaambia kwamba, “Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo mimi nimeushinda ulimwengu”. Na hivi Yohane katika kitabu cha Ufunuo anawafariji katika masumbuko hayo akisema kwamba yote yatabadilika na mambo yatakuwa shwari. Katika kueleza njozi zake Yohane anatumia mfano uliotumika na manabii wa zamani walipoeleza “Siku ya Bwana” (Amo 5:18).
Zamani hizo taifa teule lilidhulumiwa mara nyingi na Waashuru na Wakaldayo na Wayunani, na kuhamishwa mbali na nchi yao. Katika taabu hizo manabii walitabiri siku ya wokovu kwamba ipo karibu, na kwamba taifa hilo teule litajitawala na Mungu atawaadhibu maadui zao, hayo yote yatatokea siku ya Bwana. Yohane naye anatumia mfano huohuo katika kuelezea historia ya Kanisa, taifa jipya na teule, kwamba taifa hili jipya linadhulumiwa kama ilivyokuwa taifa teule zamani zile. Wakristo wengi wanauawa kwa sababu ya imani yao kama tunavyosoma katika Ufunuo 13; 6:10-11. Na madhulumu hayo yanafanyika na Warumi (Mnyama ailiyetajwa katika sura 13:1, na nyuma ya Warumi ni shetani, adui mkubwa kupita wote wa Kristo na taifa lake. Haya tunasoma katika kitabu cha Ufunuo sura 12 na 13: 2, 4.
Katika kufikisha ujumbe huo, ili watesi wa Wakristo wasiambulie chochote hata wakisoma kitabu hicho, ndiyo sasa mwandishi anatumia majina ya mafumbo au majina ya kupanga. Unajua ndugu yangu, watu hawatoi majina ya kupanga kwa watu wasio wafahamu, yaani huwezi kumpa jina la kupanga mtu ambaye hayupo au hajazaliwa bado. Wala hawatoi majina ya utani kwa watu wasiowajua au watu wasiowadhuru.
Hiki kitakuwa ni kituko ambacho ni sawa na kufukuza upepo wakati hufahamu unatoka wapi wala unaelekea wapi! Basi watu, hutoa majina ya kupanga au ya utani kwa watu wanaowafahamu na wanaowadhuru. Na hivi kufuatana na ukweli huo, walitoa jina hilo kwa Kaisar Nero aliyejifanya Mungu na kuwatesa Wakristo na hivyo kupewa jina la kupanga ambalo ukikokotoa kigematria jina lake kwa Kiebrania unapata jumla ya namba hiyo 666.
Tukizingatia mazingira ya kitabu cha Ufunuo, namba 666 au 616 haiwezi kusimama kwa ajili ya mtu mwingine kama Hitler, mtume Muhammad, Mussolini au Baba Mtakatifu. Hawa wote hawakuwepo enzi zile kilipoandikwa kitabu cha Ufunuo, na zaidi hawakuwa maadui wa Wakristo na hivyo wapewe majina ya kimafumbo. Naomba tuelewe vizuri kuwa hata wale wanaotoa shutuma kwamba namba hiyo imeandikwa kwenye mavazi ya Baba Mtakatifu, kwamba haipo na pia hakuna anayeweza kuonesha vazi hilo kwa ushahidi, kama ni maandishi ni mitra yake tu, yaani Kofia ile ya kiaskofu ambayo ina herufi mbili tu, nazo ni A na W ambazo ni Alfa na Omega kwa Kigiriki, yaani mwanzo na mwisho, ambayo tunapata katika sura ya 1:8, 17. Hivyo ndugu zangu kama tunatafuta uzima wa milele, basi tuache uongo na majungu kama haya ya kuwabambika watu majina yasiyo yao.
Hapa wapo pia wanaombambika Baba Mtakatifu namba 666, wakidai kuikokotoa namba hiyo katika majina matatu tofauti, yaani jina la Kilatini, VICARIUS FILII DEI (yaani Kaimu wa Mungu, jina la Kigiriki LATEINOS (yaani Mlatini) na jina la tatu ni la Kiebrania ROMIITH (yaani Mrumi), ukikokotoa majina hayo kigematria utapata namba 666 kadiri yao. Lakini tukumbuke kwamba kwa misingi halali ya kusoma Biblia hatuwezi kuyapokea majina hayo na kuyafanyia tahakiki ya kihistoria, kwani majina haya hayajawai kutumiwa na Baba Mtakatifu yeyote katika historia ya Kanisa, sembuse na karne ya kwanza baada ya Kristo wakati ambapo hata upapa wenyewe ulikuwa bado haujakua na kuanza kutumika.
Hakuna Papa ambaye aliwahi kuwa hatari na adui wa Wakristo, kwani Papa au Baba Mtakatifu ni Halifa wa Mtume Petro, askofu wa Roma, wakili wa Yesu Kristo duniani na mkubwa wa Kanisa Katoliki. Sasa kama ni wakili wa Yesu Kristo duniani, je, atakuwaje kinyume kwa kuwatesa wale walio wafuasi wa Yesu anayemwakilisha? Bila shaka hilo haliwezekani. Zaidi ni kwamba watu wasio hatari wangalipewaje majina ya kupanga ama ya siri? Ndugu zangu kwa hilo haiwezekani. Pia wale wasomaji wa kitabu cha Ufunuo wangelielewaje aya ngumu inayotaja kitu kisichojulikana kwao? Wangelifanyaje hesabu za kigematria kwa kutumia majina wasiyoyajua?
Hapa wapo ndugu zetu Wasabato na mafundisho yao ya Bibi Ellen White, ambaye katika kitabu chake kiitwacho VITA KUU, ametumia Biblia kufundisha na kuthibitisha chuki yake kinyume na ukweli, kwani katika kitabu hicho Ukurasa wa 18, amemtaja Papa kama ndiye aliyejitwalia majina ya Mungu. Pia Ukurasa wa 21, wa kitabu hicho VITA KUU, Bibi Ellen White anasema yule mdanganyifu mkuu (yaani shetani), alikuwa hajamaliza kazi yake. Aliazimia kukusanya jamii ya Wakristo wote chini ya uongozi wake, na kutumia nguvu zake kwa njia ya Askofu wa Rumi mwenye kujivuna na kujidai kuwa ni makamu wa Kristo. Kwa kifupa Bibi white anadai kuwa Papa ni mtumishi wa shetani.
Zaidi katika Ukurasa wa 24-wa kitabu hichi VITA KUU, Bibi White anasema mwanzo wa utawala wa Kanisa la Rumi ulikuwa mwanzo wa zama za giza. Kwa mafundisho hayo ya Bibi Hellen White, Wasabato wanaadai kwamba “mnyama” anayetajwa katika kitabu cha Ufunuo 13:1, ndiye Papa au Baba Mtakatifu.
Kwa mafundisho hayo tunaona wazi elimu ndogo ya Biblia aliyonayo Bibi Ellen White, kwani pia anatumia kitabu cha nabii Danieli na maelezo ya ndoto ya mfalme Nebukadreza, akidai kwamba maelezao hayo yanamhusu Papa. Lakini ukweli ni kwamba mwandishi wa kitabu cha Danieli hakuwa na wazo la kusema chochote kuhusu Papa.
Ndugu zangu, hapa wapo pia Wakatoliki ambao wameamua, kuyavulia maji nguo na kuyaoga ama kuwatolea uvivu wale wanaowasema kuhusu imani yao, hao wanapenda malumbano na hivi katika kujibu malumbano ya chuki na uadui, wametoa tafsiri mpya ya namba 666 kwa Wasabato.
Ndugu zangu matusi watu hawasomei darasani kiasi kwamba aliyefika darasa la juu au aliyechukua stashahada, ndiye mwenye uwezo wa pekee kuyapata matusi makubwa kabisa. Tukikumbuka hili, tuangalie mfano huu jinsi namba 666 inavyoweza kugeuzwa kwa yeyote. Madhalani, ukichukua kauli mbiu za Wasabato, namba 666 ni yao kwa nambari za Kilatini. Kwa mfano maneno ya Wasabato CURE VITAL SEVENTH DAY, ukikokotoa kigematria utapata namba 666, pia kauli mbiu inayosema CURATUS VITALE SABBATA DIES, ukikokotoa kigematria utapata namba 666. Tena Wasabato wanayo kauli mbiu nyingine inayosema SALVUS, CURARE SABBATA DIES, kigematria ni namba 666. Na maneno yao mengine yanasema, DEAL AXE VIE PAPACY, ukikokotoa nayo kwa kigematria utapata jumla namba 666. Mwisho kauli mbiu ya Wasabato inayosema SALVATION, CURE SEVENTH DAY, ukikokotoa kigematria utapata jumla ya namba 666 kwa nambari za Kilatini.
Wakatoliku hao wanadai kwamba kwa kadiri ya maandiko, mnyama anayetajwa katika kitabu cha Ufunuo na kidogo katika kitabu cha Danieli ni Kanisa la Wasabato. Wakianza na ufunuo 12:18, wanaonesha kwamba ni Wasabato na makanisa mengine yaliyosimama ufukoni maana yana makao makuu mjini New York, Chikago ua Los Angeles, miji ambayo imejengwa ufukoni na siyo Roma kwani Roma ipo kilomita 16 kutoka baharini.
Pia Ufu 18:4-5, inawahusu Wasabato na 13:4, inasema mnyama amepata kiti cha mamlaka yake kutoka Roma. Neno hili linawataja Wasabato kwani nguvu yao inatoka kwa taaifa kubwa la Marekani ambalo ndiyo Roma ya siku hizi.
Imeandikwa mnyama anatawala dunia miaka 1260, ndivyo ilivyo kwa Wasabato, kwani namba hiyo inapatikana kwa kuzidisha tarakimu za mwaka 1546 aliozaliwa, Martin Luther, mwanzilishi wa mageuzi karne ya 16, kwa idadi ya makanisa maarufu yaliyotokana na mafundisho yake, yaani Walutheri, Wakalvini, Wazwingli na nusu kanisa yaani Wasabato, na hivyo kufanya namba 3.5. Ndipo basi 15x4x6x3.5=1260.
Ya kwamba mnyama alipata dondo ambalo limepona (Ufu 13:3), ni Wasabato na wakubwa wao, kwani wamekuwa wakijaribu kutabiri mwisho wa dunia bila mafanikio, hadi mwaka 1980 walipaacha. Miaka waliyotabiri kuwaa mwisho wa dunia bila kutokea lolote ni 1874, 1878, 1914, 1925, 1932, 1939 na mwisho 1975.
Ya kwamba nguvu ya kisiasa na kidini inayoabudiwa inatimia tena kwa Wasabato, kwa maana wao ni kikundi cha kidini kinachosaidiwaa sana na taifa babe la Marekani.
Pia kwamba mnyama ametibua amri ya Mungu (Dan 7:25), inatimia tena kwa Wasabato kwa sababu badala ya kukazia amri mpya iliyoachwa na Yesu ya upendo (Yn 13:35, Mt 22:34-40), wao wanakazia amri ya kushika sabato iliyoachwa na Bibi Ellen White.
Basi Wakatoliki wanaopenda malumbano wanaendelea kujibu wakisema, kuwa wana kiongozi anayedai hadhi ya Mungu, inatimia kwa wasabato, ambapo wanmtukuza “nabii mke”, Bi Ellen White ama Charles Taze au Jonathan Cuming. Na dhambi wanayosamehe wao ni siasa, kwani waanajidai hawajihusishi nayo kabisa.
Zaidi ya hapo ni kwamba mama Kanisa kwa vile mabinti wametoka kwake (Ufu 17:5), inatimia kwa wasabato kwa sababu nabii Bi Ellen White ni kweli mwanamke wa kuzaa kama mama na kutokana na mafundisho yake kunazaliwa makanisa mengi kila siku.
Tena kwamba nguvu ya dunia inayoajabiwa (Ufu 13:3-4), inatimia sasa kwa wasabato kwani ijapokuwa wapo kidogo kiitikadi, hawaogopi kugombana na waamini wengine popote pale duniani.
Kwa kuongeza tu ya kwamba amefanya vita dhidi ya watakatifu (13:7), inatimia kwa Wasabato sasa, kwa sababu kwa vile wao hawalali usingizi katika kuwapiga vita Wakatoliki (ndiyo watakatifu wa Mungu, wavumilivu).
Ndugu zangu matusi watu hawasomei darasani kiasi kwamba aliyefika darasa la juu au aliyechukua stashahada, ndiye mwenye uwezo wa pekee kuyapata matusi makubwa kabisa. Tukikumbuka hili, tunaona pia mfano huu jinsi namba 666 inavyoweza kugeuzwa kwa yeyote. Madhalani, ukichukua kauli mbiu za Wasabato, namba 666 ni yao kwa nambari za Kilatini. Kwa mfano maneno ya Wasabato CURE VITAL SEVENTH DAY, ukikokotoa kigematria utapata namba 666, pia kauli mbiu inayosema CURATUS VITALE SABBATA DIES, ukikokotoa kigematria utapata namba 666.
Tena Wasabato wanayo kauli mbiu nyingine inayosema SALVUS, CURARE SABBATA DIES, kigematria ni namba 666. Na maneno yao mengine yanasema, DEAL AXE VIE PAPACY, ukikokotoa nayo kwa kigematria utapata jumla namba 666. Mwisho kauli mbiu ya Wasabato inayosema SALVATION, CURE SEVENTH DAY, ukikokotoa kigematria utapata jumla ya namba 666 kwa nambari za Kilatini.
Basi ndugu zangu tuache ubishi, na tubaki na ukweli mmoja kwamba sura ya 13:18 ya kitabu cha Ufunuo ilizungumzia jina ambalo wasomaji wake walikuwa wakilijua kama ni jina la adui yao, yaani Kaisar Neron aliyekuwa akiwatesa na kuwadhurumu Wakristo wa mwanzo na siyo jina la ndoto au majungu ya karne ya ishirini na moja ama karne hii tuliyonayo sasa. Wapendwa wasikilizaji naomba tukumbuke kwamba, watu wanapotukana, kila mmoja anaweza kulipa tusi kubwa na kumtukania mwenzake.
Hivyo ndugu zangu kwa heshima ya Maandiko Matakatifu, tuitafsiri namba 666 kwa kukokotoa kigematria asili na kukomea hapo. Tusiende mbali na kuingiza majungu na ubunifu wa uongo. Tusiihamishe namba hiyo na kuwapachika watu wasio na hatia. Kufanya hivyo ni kujiongezea majungu na ni dhambi ambayo kwa Mkristo anayeitafuta zawadi ya uzima wa milele haifai.
Basi, ndugu zangu tunapolisoma Neno la Mungu ili lituambie tunachopaswa kufanya au kukiacha ili tupate uzima wa milele, badala yake tukaichukua Biblia kupigania, hivi ndivyo tunavyoweza kugeuziana matusi. Kumbe kufanya hivyo itakuwa ni kumkasirisha Mungu.
Sasa tuelewe kuwa Mungu ametupatia sisi watoto wake, Wakristo, Biblia kama tunda, mamoja liwe chungwa, embe au ndizi na mengine. Tukiwa watoto wema tutalila hilo tunda ili tujipatie vitamin C tunayohitaji sana kwa afya zetu. Kumbe, tukiwa watoto wabaya Biblia itakuwa ni silaha ya kupigania na hivyo kuwa sumu ya kutuingiza motoni mwa milele.
Basi hili la pili tumuombe Mungu atuepushe mbali nalo, ili sisi tubaki watoto wema wa Mungu na hivyo tufaidi tunda tulilopewa na Mungu ili tuurithi uzima wa milele.
Tusimwangushe Mungu kwa kugombana na kusemana sisi wa sisi huku tukitumia Biblia kwa kuupotosha ujumbe wake.
Kwa kukazie tuseme namba 666 au 616 haimhusu Papa wala Baba Mtakatifu yeyote, na ukimwona mtu anadai hivyo ujue kwamba kama ulikuwa hujakumbana na mbeya ndiyo sasa umekutana naye katika nafsi ya mtu huyo, haijalishi awe askofu, padre, mhubiri, mchungaji au mwinjilisti.
Na wewe Mkristo mwenzangu, umbeya siyo suala lako, achana naye, na uisome Biblia Takatifu yako na kuitafsiri kwa utulivu, huku ukimwomba Mungu Roho Mtakatifu akusaidie kuelewa vizuri ujumbe wake na siyo kwa majungu na ulalamishi wa kusemana kama vile tungelikuwa watoto wa shetani., wakati sisi ni watoto wa Mungu.
Mpenzi msikilizaji wa Redio Maria, hadi hapa naomba nihitimishe jibu langu kwa swali lililoulizwa, kwanza na Catheline Lacha akisema hivi; Kitabu cha Ufunuo kinamaanisha nini juu ya namba 666? Na je, Kaisari Nero aliyewatesa Wakristo wa mwanzo anahusianaje na namba 666? Pili, limeulizwa na makatekista wa Dekania ya Konsolata-Iring
a wakisema; Tunaomba tupate maelezo juu ya namba 666 inayozungumziwa katika kitabu cha Ufunuo. Tatu, limeulizwa na wana TYCs wa Songea Boys wakisema; Kitu gani kinaonesha kwamba maneno NERON KAISAR alikuwa memba wa Freemason? Na je, ni kweli herufi hizo zipo katika kofia ya Papa? Na namba hizo zina maana gani?
Basi, kama tulivyosema katika jibu letu la msingi, ni kwamba mwandishi wa kitabu cha Ufunuo katika sura 13:18, alimaanisha jina la kiongozi wa dola ya Kirumi zamani zile, yaani Kaisar Nero, na hivi Kaisar huyo ndiye anayehusika moja kwa moja na namba 666, kwani namba hiyo ni hesabu ya jina lake, na namba yenyewe 666 inapatikana katika kitabu cha Ufunuo sura 13:18, hapo imeandikwa hivi; “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita” (Ufu 13:18).
Ukikokotoa kigematria maneno Neron Kaisar kwa Kiebrania kama tulivyosema hapo awali utapata jumla ya namba 666 na ukikokotoa kigematria kwa Kigiriki maneno KAISAR THEOS, yaani Mungu Kaisari utapata namba 616 kwenye Biblia zinazoandika hivyo. La msingi tujue iwe ni namba 666 au 616 zote zinamhusu Kaisar Nero aliyekuwa mtesi wa Wakristo wa mwanzo.
Mpenzi msikilizaji wa Redio Maria, kwa nukuu hiyo katika kitabu cha Ufunuo sura 13:18, mwandishi alimaanisha jina la kiongozi wa dola ya Kirumi zamani zile, yaani Kaisar Nero. Hivi ni kweli kwamba Kaisar Nero aliyewatesa Wakristo wa mwanzo, anahusika moja kwa moja na namba 666, kwani namba hiyo ni hesabu ya jina lake ukikokotoa kwa kigematria, maneno NERON KAISAR kwa Kiebrania.
Hivyo namba hiyo, 666 ilimhusu na bado inamhusu kiongozi huyo wa dola ya Kirumi zamani zile na wala siyo kiongozi mwingine kama Baba Mtakatifu, na wala haikuandikwa kwenye mavazi yake, kama wanavyodai wale ambao wanasoma kwa makengeza kitabu cha Ufunuo, huku wakiwa na mawazo yao binafsi. Na pia kinachoonesha kwamba Neron Kaisar alikuwa ni memba wa Freemasoni ni namba hiyo 666 ambayo ni namba ya Freemasoni na kuhusu suala la kuwatesa Wakristo na kutaka kuangamiza Ukristo ambalo ndilo lengo la Freemasoni pia.
Na huo ndio mwisho wa jibu langu kwa swali linalohusu ufafanuzi wa namba 666 inayopatikana katika kitabu cha Ufunuo sura 13 aya 18. Asanteni sana kwa kunisikiliza, Mungu mwema awabariki!
 
Katoliki kanisa lenye mambo ya kushangaza.

Kanisa linaruhusu kunywa pombe ila linakataza viongozi wake wa ibada kufunga ndoa.

Kuna siku nilienda kwenye mkutano baraza la maaskofu kurasini.. nikakuta mapadri wapo kwenye mkutano wao.. muda wa lunch ulivyofika. Mapadri wakaanza kula pombe kwa raha zao. Watu wanakula bia za kutosha
Maswali ya Bibilia yajibiwa
Menu icon
JUA JINSI YA ...
Kutumia milele na Mungu
Pata msamaha kutoka kwa Mungu
SWALI
Biblia inasema nini juu ya kunywa kileo? Je, ni dhambi kwa mkristo kunywa kileo?
JIBU

Maandiko yana ilani nyingi juu ya kunywa kileo (mambo ya walawi 10:9; hesabu6:3; kumbukumbu la torati 29:6; waamuzi 13:4,7,14; samueli wa kwanza 1:15; methali 20:1; 31:4,6; isaya 5:11;22; 24:9; 28:7; 29:9; 56:12; mika 2:11; luka 1:15). Maandiko hayakatazi mkristo kunywa pombe, divai wala kinywaji chochote chenye kileo ndani. Maana maandiko mengine huzungumzia kileo kwa kuhalalisha matumizi yake. Mhubiri 9:7 inaamuru, “ kunywa kileo na moyo mkunjufu.” Zaburi 104:14-15 inaeleza Mungu hutoa divai “ inayofurahisha mioyo ya wanadamu.” Amosi 9:14 inazungumzia juu ya kunywa divai kutoka kwa shamba lako kama alama ya baraka za Mungu. Isaya 55;11 inapongeza “ naam, njoo ununue divai na maziwa…”

Kile Mungu anachowaamuru wakristo juu ya kileo ni wajizuie na ulevi (waefeso 5:18). Biblia inakataza ulevi na athari zake (methali 23:29-35). Wakristo wanakatazwa kuachilia miili yao itawalwe na vitu vinginevyo. (wakorintho wa kwanza 6:12; petro wa pili 2:19). Kunywa kileo kingi kunaathiri mtu. Maandiko yanakataza chochote kile ambacho kwa kukifanya unasababisha wengine kujikwaa( wakorintho wa kwanza 8:9-13). Kwa mujibu wa haya ni vigumu mkristo kukiri kuwa anakunywa kileo kwa utukufu wa Mungu ( wakorintho wa kwanza 10;31).

Yesu aligeuza maji kuwa Divai. Huenda ikawa Yesu alikuwa akinywa divai katika karamu Fulani Fulani (Yohana 2:1-11; Mathayo 26: 29). Katika nyakati za agano jipya, maji yalikuwa yakijawa na vidudu na uchafu kama hali ilivyo sasa katika mataifamengine ya ulimwengu wa tatu. Hii ndiyo sababu watu walipendelea kunywa divai kutoka kwa zabibu ili kuepukana na taka taka hizi. Katika timotheo wa kwanza 5:23, Paulo alimkataza timotheo kunywa maji yaliyokuwa yakimtatiza tumbo lake na mahali pake anywe divai. Divai ilikuwa na asili ya kileo ndani lakini haikuwa na kiwango cha kilevi sawa na cha leo. Haikuwa maji ya mzabibu moja kwa moja wala kileo sawa na cha leo. Maandiko hayakatazi mkristo kunywa kileo cha aina yoyote bali yanakataza ulevi na utumwa wa kileo (waefeso 5:18; wakorintho wa kwanza 6:12).

Kileo, kinapotumiwa kwa uchache hakina athari kwa mwenye kukitumia. Kutumia kiasi kichache cha kileo ni jambo linaloruhusiwa mkristo. Ulevi na utumwa wa kunywa kileo ni dhambi. Kwa sababu ya kushindwa kujizuia katika viwango vya matumizi ya kileo, kukwaza wengine na hata kupatikana na hatia mbali mbali, ni vizuri mkristo aepukane kabisa na matumizi ya kileo cha aina yoyote.
 
Ni mapokeo na jinsi madhehebu yanavyotafsiri biblia mkuu.
Kila mmoja humuona mwenzie anakosea na yeye yupo sahihi zaidi.
Na ukizingatia hawafanyi hayo nje ya bible ila kuna vifungu kila mmoja anaondoka na tafsiri yake, kama ulivyo ubishani wa najisi, siku ya sahihi ya kuabudu, kunena kwa lugha n.k

Pale aya ya kwanza umeandika vyema sana.
Nikuambie kitu kimoja Tu ambacho ni muhimu.
Madhehebu hufasiri biblia wanavyotaka wao, biblia imekataza na unatakiwa ufahamu kwamba Neno la Mungu ni Neno la kinabii.

Sasa biblia imepiga marufuku kufasiri kama mtu anavyotaka
2 Petro 1:20-21
Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.
Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Hivyo Neno la Mungu harifasiliwi kama mtu anavyota Bali Tu lazima uongozwe na Roho mtakatifu. Na Roho mtakatifu hamuongozi mtu ambaye hafuati neno lake,

Mfano Leo hii huwezi kuniambia hasa hawa wachungaji wa kimadhehebu wana Roho mtakatifu wakati huo wameruhusu haki Sawa kanisani
Twende kwa andiko maana daima nitatetea Neno la Mungu naomba Mungu anisaidie kwa hilo.

1 Wakorintho 14:34
Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.

Haina haja ya kufasiri ni kwamba mwanamke ni marufuku kuhubiri kanisani.
Sasa je unaweza kuniambia huyu anaongozwa na Roho mtakatifu wakati ameshindwa kulifuata neno la Roho mtakatifu?

NAludia tena ndugu nakupenda mno kutoka moyoni, usijiunge na kanisa toka kwenye hiyo mifumo uludi kwenye Neno, ulitetee Neno,uliishi Neno ili uwe salama ndugu yangu🙏 na lazima upate ubatizo Harisi hiyo ni kweli.

ukiacha ama kuongeza neno kwenye biblia. Maana yake huifuati bible
 
Hili huwezi kulithibitisha hata kidogo. Mimi nikuulize swali kama WAKATORIKI NI waandishi WA bible mbona hawaifuati? Bible imekataza mwanamke asihubiri mbona wao wanahubiri?, askofu imempasa awe na mke mmoja mbona hawaoi? Bible inasema hata maraika asiabudiwe mbona hao ndio wamewafanya ndio WA kuwaomba?

ndugu yangu nakupenda mno usitetee dhehebu tetea neno la Mungu hakika itakua salama katika ufalme wa Mungu Amini Tu hilo.
Hayo yote uliandika ni uongo
1. Umesema mwanamke anahubili neno umeshawahi ona sister anaongoza misa? Sio kweli mwanamke kuongoza ibada
2. Kwa nini Mapadri na maaskofu hawaoi ni kwa sababu ya ufalme wa Mbinguni. Soma andiko la
Mathayo 19:12
Maana kuna sababu kadhaa za kutoweza kuoa: Wengine ni kwa sababu wamezaliwa hivyo, wengine kwa sababu wamefanywa hivyo na watu, na wengine wameamua kutooa kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea fundisho hili na alipokee.
Je mtume Paulo alioa na kwa nini hakuoa?

3. Kanisa katoliki ni kanisa takatifu la mitume
Linalomuabudu Mungu
 
Hili huwezi kulithibitisha hata kidogo. Mimi nikuulize swali kama WAKATORIKI NI waandishi WA bible mbona hawaifuati? Bible imekataza mwanamke asihubiri mbona wao wanahubiri?, askofu imempasa awe na mke mmoja mbona hawaoi? Bible inasema hata maraika asiabudiwe mbona hao ndio wamewafanya ndio WA kuwaomba?

ndugu yangu nakupenda mno usitetee dhehebu tetea neno la Mungu hakika itakua salama katika ufalme wa Mungu Amini Tu hilo.
Hayo yote uliandika ni uongo
1. Umesema mwanamke anahubili neno umeshawahi ona sister anaongoza misa? Sio kweli mwanamke kuongoza ibada
2. Kwa nini Mapadri na maaskofu hawaoi ni kwa sababu ya ufalme wa Mbinguni. Soma andiko la
Mathayo 19:12
Maana kuna sababu kadhaa za kutoweza kuoa: Wengine ni kwa sababu wamezaliwa hivyo, wengine kwa sababu wamefanywa hivyo na watu, na wengine wameamua kutooa kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea fundisho hili na alipokee.
Je mtume Paulo alioa na kwa nini hakuoa?

3. Kanisa katoliki ni kanisa takatifu la mitume
Linalomuabudu Mungu
 
kanisa katoliki wana katabia ka ukatili wa kisaikolojia,
Hata kama kanisa Fulani au walokole wakiwashambulia Imani yao, wao wanawaskiliza tu bila tashwishwi yeyote na hawajibu chochote na mambo yanaishia apo, basi
Nimekaa na kutafakari sana Kwa nini wasabatho wanalipiga vita sana kanisa katoliki na hiyo vita siyo kwa makanisa mengine?

Wajuzi mnijuze!

View attachment 2757316
 
Yesu hajawahi kutunga SHERIA na Hana sheria hata Moja. Acha upotoshaji.

Hiyo sheria ya mpende Mungu na jirani yako Ipo kwenye Torati. Acha kupotosha.

Haya soma

Luka 10: 25 “Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?

26 Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje?

27 Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.

28 Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi.
Kuna sehem nimesema Yesu alitunga sheria? Acha kukurupuka. Yesu alikazia hilo kuwa msingi wa sheria zote. Amri saba za torati zinaingia hapo tumia akili kufikri sitak kuandika sana. Pili hujajib swali lang... Sabato manyoshika ni ile ya Mungu kumaliza kazi, ile ya waisrael kufanya kazi siku sita na kupumzika au zinginezo? Mind you sabato zilikua nyingi tu. Mwisho ujibu kwann mnangangania tu hii ya kufanya kaz siku sita na saba kutofanya?
 
Hakuna ibada ya misayoyote ya kanisa katoliki ambayo inakosa injiri ndio yanafuata mahubiri ya kuifafanuwa injiri, sasa somo laq kwanza na somo la pili linasomwa kutoka wapi kama siyo kwenye vitabu vya biblia? kimsingi ibada nzima iko hapo kwenye injiri.
Unaniangusha Dr..ni Injili
 
Hayo yote uliandika ni uongo
1. Umesema mwanamke anahubili neno umeshawahi ona sister anaongoza misa? Sio kweli mwanamke kuongoza ibada
2. Kwa nini Mapadri na maaskofu hawaoi ni kwa sababu ya ufalme wa Mbinguni. Soma andiko la
Mathayo 19:12
Maana kuna sababu kadhaa za kutoweza kuoa: Wengine ni kwa sababu wamezaliwa hivyo, wengine kwa sababu wamefanywa hivyo na watu, na wengine wameamua kutooa kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea fundisho hili na alipokee.
Je mtume Paulo alioa na kwa nini hakuoa?

3. Kanisa katoliki ni kanisa takatifu la mitume
Linalomuabudu Mungu
Ndugu basi nisamehe kama nimesema uongo. Ila twende kwa fact NENO LA MUNGU liwe kweili na la mtu liwe uongo.
Najibu kwa fact.
1. Neno limesema mwanamke ni marufuku kufundisha wala kuhubiri chochote kanisani, na katika hilo sijatenganisha ni mwanamke wa namna gani!! Neno limesema mwanamke anyamaze katika kanisa hii ni kwa wote..sasa kwa sababu ulichojibu umebase Sana kutetea dhehebu la roma usijali twende taratibu kuhusu, (a)nimekaa katika KARISMATIKI KATOLIKI Karibu matawi mengi wanahubiri wanawake (b) nimekaa na kusalia Roman Catholic tangu nikiwa mdogo na nilibatizwa nikiwa mdogo(ambayo ubatizo wa kinyume na maandiko, bible inasema aaminie na kubatzwa. Sasa mtoto anaamini nini?)Hadi mwaka 2018 mda huo wote nawaomba wanawake wakipewa mamlaka makubwa kuanzia kwenye jumuia kigangoni, palokiani Hadi jimboni, utakuta mwenyekiti ni mwanamke ama katibu. je hatofundisha utaratibu? Je bado unasema mimi ni muongo? (C) Mathayo 19:12 inasema hivyo Lakini ni Mimi na wewe ndugu yangu sio kwa askofu kwa askofu Paulo anasema hivi 1 Timotheo 3:2 ....imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja.....
UNaomba kwa askofu imempasa imempasa sio HIARI ila IMEMPASA KUOA kwa maana nyingine ni razima. Unapokuja kwa Paulo kutokua Mungu kalifanya liwe hivyo kwake maana alikua na huduma kubwa mno ya kupeleka injili kwa wamataifa yeye alikua mjumbe wa kipekee

SHIKILIA HILI NENO LA MUNGU LIMESEMA IMEMPASA ASKOFU AOE HIYO NI RAZIMA. MIMI NA WEWE si lazima.
Simama na Neno
 
Islamic empires za wapi!?..maisha yalikua murua chini ya Dola za kiislam,refer utawala wa Saladin,kule Spain Islamic empire ilikua baraka tupu
Kupatikana kwake kulikua na kipigo kitakatifu...jasho na damu vilimwagika..so kila kitu kina dark side zake..lakini wote Mungu aliwashika mkono.
 
Katika watu wasiokuwa na akili duniani Wewe ni namba moja.

Calendar inayotumika ni Gregorian calendar ambayo ni ya wakatoliki, sasa ni kichaa peke yake ndio anaweza kusema jumapili ni siku ya kwanza ya Juma, unless unioneshe unatumia calendar gani? Ya kiislamu? Ya kichina au ya Ethiopia?
Katika mtu mjinga na poyoyo duniani,wewe wa kwanza, "ijumaa kuu" inaadhimishwa kwanini? Kwanini iwe ijumaa na siyo siku nyingine?kwanini pasaka inakuwa jpili? Unajua siku ya pasaka kuwa watu wanaadhimisha kufufuka kwa yesu? Unajua kwenye biblia kuwa kuna mtu alienda kuuomba mwili wa yesu siku aliyokufa kwa madai sabato isije kuukuta ukiwa bado msalabani? Ewe msomi mjinga, mwenye PhD ya ujinga ushawahi kutulia na kusoma biblia?ushawahi kuunganisha nukta kwanini kuna ijumaa kuu?kwanini pasaka iwe jumapili inayofuata?
 
Back
Top Bottom