Kwanini frame za Sinza Kodi ipo juu Lakini sioni muingiliano wa watu madukani?

Sinza,kinondoni na makumbusho.
Kwa sisi tuliopo idara shetani tunaelewa kinachoendelea.

Hizo sehemu kuna vijana wengi na watu wazima wapenda maisha kama vijana na wale wasiojielewa.

Mnajiuliza kwa nini maeneo hayo ugombaniwa sio tu frem mpaka nyumba za kupanga.

Sehemu tatu zina wimbi kubwa la wapenda starehee,upatikanaji wa vyakula vya anasa,ukaribu ukifika maeneo mazuri na kote ni katikati.

Kuanzia wanavyuo,wafanyakazi vijana,wanaojiuza,wasanii,masharobaro wanapapenda huko.

Kipindi makonda anataja orodha ya wauza sembe kumbuka idadi kubwa ilitoka maeneo hayo.

Black market zote zipo sinza,kinondoni na makumbusho ndio zipo hapo na zipo smart kuliko ukienda mbagara au temeke.

Vigogo na wakubwa serikalini ndio maeneo yao ya kuwabeba vijana wanavojua ili wasionekane wao.

Makumbusho asilimia kubwa ni watoto wa wastaafu,walioachiwa mitaji,watoto wa matajiri ndio maana wameishia makumbusho tu sababu wanatoka maeneo kama mbezi beach,tegeta,mwenge,moroco,kawe,ostabey na maeneo ambayo yanafikika makumbusho ndio walipo zaliwa au kukulia hizo sehemu.

Kinondoni kiufupi biashara ni zadili sana kuliko zilizopo machoni mwa watu. Na maduka mengi ya nguo ukiangalia ndani nguo zao sio za kuvaa hata uswahilini ndio maana unaona wanawake wa kinondoni na sinza kuanzia nguo za ndani mpaka za nje zipo kimitego tego sana.
Ukahaba na starehe ndio zinaendesha fremu kuna wale walio beti wakapata pesa na kujionesha kaingia dukani kununua nguo.wale wa mikoani kuja kutoa shamba na pesa zao.


Nitaendeleaa…..
 
Mkuu elewa hata nguo zinazouzwa sinza bei ni tofauti kubwa na kariako.


Wenye pesa zao hawana muda kuingia kariakoo kupigana vikumbo na wamachinga bali wanaenda kununua Sinza, hivyo pango linalipika kirahisi tu
Yah ni kweli, niliwahi kununua kava ya simu kwa sh 15,000 hapo ni baada ya punguzo alianzia 20,000. nimefika nyumbani waif kaniambia unaona hii yangu nimenunua kariakoo buku tano.
 
Wanaosema habari za kujiuza sijui money laundering mara madawa ni wivu tu na wengi pengine hawajawahi kufanya biashara. Hivi watu biashara ya madawa wanaivhukulia poa sana kiasi hata mtu yeyote tu anaweza kuifanya eeh!?

Wafanyabiashara wengi wa sinza ni legit kbs na wapambanaji wenye style yao tofauti ya biashara. Ukija kuchunguza utagundua hata kkoo mzunguko umepungua sio km ule wa miaka 10 iliyopita na moja ya sababu ni pamoja na kuongezeka maduka sehemu nyinginezo kama sinza nk.

Kama mtu anauza mf. nguo na anaagiza mwenyewe mzigo unafika loose cargo yake pc 1k, 2k, mpk 5k na anaweza kuusukuma wote dukani jumlisha online ndani ya miezi mi2 au chini ya hapo atashindwaje kulipa kodi ya laki 5 kwa mwezi!? Kama unajua profit margin wanazoweka/pata hao watu wa sinza ni kitu kidogo sana hiyo kodi. Ktk miezi 12 mtu kashusha mzigo mara 6 au 7 na zote umeisha km lbd ulikwama mmoja akauza sale sio mbaya still hela ya kodi hakosi na faida ya kuendeshea mambo yake mengine anakuwa nayo. Nendeni kwenye ofisi za mabasi pale shekilango muone parcel zinavyosafirishwa kila siku kwenda mikoani na hao wafanyabiashara ndio mtajua kuwa hamjui kitu.

Kushindwa na kurudisha frem ni kawaida hata kkoo inatokea sana. Haimaanishi wote wanashindwa au wote wanafanikiwa. Tusipende kuhitimisha mambo bila kufanya udadisi wa kutosha. Tujifunze kujifunza! Mwisho kuchunguza fulani anafanikiwaje bila ya tamaa ya kutaka kujifunza ni dalili za mwanzo kbs za UCHAWI
 
Wewe ndo uko nyuma ya muda. Tunaosema money laundering na michezo mingine michafu tuna uhakika 100%. Na uhakika wetu unachangiwa na kuwahi kufanya biashara huko pia. Ingawa wapo wanaofanya biashara halali pia. Ndugu yangu haya mambo ni tofauti unavyoona. Miaka ya 2000 kuna fundi wetu mmoja mzuri sana pale Sanawari Arusha alikuwa akitutengenezea magari. Yule kijana alikuwa smart na msikivu kinyama hana shida na mtu. Tulipigwa surprise ya mwaka tulivyosikia kashiriki tukio la ujambazi ubungo kupora hela za nmb.
 
Oyaa ila Kuna ukweli hapo. Sawa na maduka ya iPhone makumbusho. Utakuta anauza simu moja tu kwa wiki lakini nje ya duka kapaki Toyota crown.
Afadhali maduka ya simu kidogo inaingia akilini kwa sababu kuna simu hadi za milioni 2 akiuza moja kwa wiki inaweza kumsukuma lakini suruali au shati ni elfu 30 tu hawezi kuendesha maisha
 
Ukwepaji mkubwa wa Kodi!
 
Money laundering ipo kila mahali tena maeneo yenye mzunguko mkubwa wa pesa ndipo inafanyika vzr. Na kwanza utakatishaji kupitia bidhaa halisi mf nguo na viatu ni mgumu sana. Tofauti na huduma. Unatakatishaje bilioni 10 kwenye biashara ya nguo!?

Vijana wanapambana hapo sjnza kwa namna wanazozijua wao pesa ya kodi wanapata na pesa ya kuendesha maisha inapatikana. Biashara za haramu zipo lkn ni kwa % chache sana huwezi kusema maduka yote sinza wanajihusisha sijui na kujiuza mara madawa mara utakatishaji. Si kweli! Ni wivu tu
 
Mkuu wewe ni mzoefu wa jiji vipi mtu akiwa na milioñ 50 anaweza kufanya biashara ya kueleweka hapo town?
 
Ukimaliza research hii hamia kwa watu wanaoishi mahotelini maisha yao yote na haijurikani wana shughuri gani.

Na kuna wale wenye makazi yao lakini wanashinda Kilimanjaro hotel, Serena, Sea cliff hotel daily.
 
Mkuu nikutumie picha ya huyo mwenye t-shirt 12 shop na Kodi ni laki 3?..utanambiaje huyo anafanya online na mzigo Hana? Ofisini kwake Kuna masofa na urembo mwingiii, inatia mashaka
 
Baki na unachoamini wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…