Kwanini hamtaki kujibu haya maswali kwenye Biblia?

Ukiuliza kawekwa na nani,maana yake umekubali yupo,sawa!?
Ukikubali tukajadili uwepo wake maana kuna mashaka anaweza asiwepo kweli , ulisha wahi sikia nan humu ndani ana mashaka na uwepo wa Mr Mello? Na kuhoji
 
Adam na Eva waliiwahi kuzaa watoto wa kike pia, ila hawakutajwa kwenye Biblia na mmoja wao ndiyo huyu aliyekuja kuolewa na Kaini. Walikuwa wanaruhusiwa kuoana mtu na dada yake
Kuna mtoto mmoja wa kike wa Adamu na hawa ametajwa kwenye Biblia mara moja tuu ila sikumbuki ni kwenye kitabu gani ngoja ntafatilia.

Mwanzo 5:4
Baada ya kumzaa Sethi, Adamu aliishi miaka 800, na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike.
 
Biblia yaliyoandikwa ni yale muhimu kwa mhtasari tu kati ya mambo mengi yakiyotokea.Baada ya adamu kuumbwa alizaa watoto wakiume na wakike na walizaana wenyewe kwa wenyewe hadi wakaongezeka.Watoto walioandikwa ni watatu tu wakiume waliokua na jambo la muhimu.Pia unatakiwa kujua toka Adam hadi Mussa ambaye ni mwandishi wa kitabu cha mwanzo ilipita miaka mingi.kwahiyo maisha yalishaendelea miaka mingi.Kwa mfano rahisi ni huu,waliopigania harakati za uhuru wa Tz walikua wengi lakini wanaotajwa nakuwepo kwenye maandishi ya historia ni wachache.Nadhani umeelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
majadiliano yenu Nasikitika kusema kwamba yatazid kuwachangany nyinyi wenyewe .Asilimia kubwa ya wachangiaji wanataka kujiona wao ndo wajuzi zaidi ya wachangiaj wengine mnapotez lengo la kuelimishana
 
majadiliano yenu Nasikitika kusema kwamba yatazid kuwachangany nyinyi wenyewe .Asilimia kubwa ya wachangiaji wanataka kujiona wao ndo wajuzi zaidi ya wachangiaj wengine mnapotez lengo la kuelimishana
Apo ili kuelimishwa inabidi upande mmoja ukubali kuwa zuzu ili kulishwa matango pori
 
Ukikubali tukajadili uwepo wake maana kuna mashaka anaweza asiwepo kweli , ulisha wahi sikia nan humu ndani ana mashaka na uwepo wa Mr Mello? Na kuhoji
Hakuna anayehoji uwepo wa Mello humu ndani sababu hakuna kipofu,Ila duniani mpo vipofu msioona alama/dalili za Mungu,hapo mna mapafu na pua za kuvutia na kutolea hewa iliyopo bwerere duniani
 
Muulize Mungu mwenye biblia yake
 
Kutoka misri mpka Israel ni km 623, ila musa na genge lake walitembea miaka 40, wastani wa km 15 kwa mwaka ,sawa na km 125 kwa mwezi, saw na mita 42 kwa siku sawa na uwanja wa mpira wa miguu[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
Biblia ni chai [emoji478][emoji478][emoji261][emoji261]
 
Hakuna anayehoji uwepo wa Mello humu ndani sababu hakuna kipofu,Ila duniani mpo vipofu msioona alama/dalili za Mungu,hapo mna mapafu na pua za kuvutia na kutolea hewa iliyopo bwerere duniani
Mbona sasa unalalamika , ili uamini uwepo wa Mungu lazima ukubali kuwa kipofu.
 
Hakuna anayehoji uwepo wa Mello humu ndani sababu hakuna kipofu,Ila duniani mpo vipofu msioona alama/dalili za Mungu,hapo mna mapafu na pua za kuvutia na kutolea hewa iliyopo bwerere duniani
Hewa iliyopo duniani ina thibitisha vipi uwepo wa huyo Mungu?

Kwanza kama huyo Mungu yupo anacho jifichia huko ni nini?
 
Kwahiyo watoto wa Adamu wa kike walizaa na Kaini?? Kama hivyo kwann hairusiwi kuzaa na ndugu yako
Hairuhusiwi na nani?.Hizo ni sheria za nchi mbalimbali kulingana najinsi walivyoona.Na ziko nchi wanazaana,labda sheria ya nchi yako kwasababu za ustaarabu na magonjwa.Uko nyuma walikua wanazaana ndo maana kipindi cha safari ya waisraeli walipewa amri ya kutokulala na dada yako,walikatazwa kwasababu nijambo ambalo lilikuwepo.soma kumbukumbu la torati 27:22.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona sasa unalalamika , ili uamini uwepo wa Mungu lazima ukubali kuwa kipofu.
Ni kinyume,sisi waislam QUR'AN inatutaka tutafakari maumbile ya ulimwengu na walimwengu Kama dalili ya kuwepo Mungu,hatuamini kibubusa,ndiyo maana Quran Inauliza Sana maswali 'hivi hawafikiri' 'hivi hawana akili'?!..tusipokuteremshieni maji mawinguni je ni nani atakuteremshieni!?..tumekuumbeni kwa tone la manii hatua kwa hatua,hivi hamfukiri,hivi tumekuumbeni nyingi imara au mbingu tulizoziumba!?..yote kufanya mtu atafakari
 
Hewa iliyopo duniani ina thibitisha vipi uwepo wa huyo Mungu?

Kwanza kama huyo Mungu yupo anacho jifichia huko ni nini?
Pua yako na mapafu vilijuaje kwamba utahitaji hewa iliyopo duniani ili uweze kuishi Hadi vikawepo hapo!?..macho yako yalijuaje kuwa duniani Kuna mwanga so yakae hapo ili uone!?
 
Kama yaliyo andikwa kwenye Biblia ni yale ya muhimu tu,

Hayo mambo mengine ya kwamba Adamu alizaa watoto wakike na wakiume kisha waka zaana wao kwa wao na kuongezeka, Umeyapata wapi?

Na umejuaje na unathibitishaje?

Haya mambo yasiyo ya muhimu ambayo haja andikwa, kwa nini hayaku andikwa?

Unathibitishaje yaliyo andikwa kwenye Biblia ndio ya muhimu tu?
 
Nadharia ya Mungu imetengeneza nadharia ya shetani ili fake character Mungu apate sababu ya kuwa Mungu.
 
Anae hoji hivyo ni nani kwenye hiyo Qur'an?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…