Kwanini hamtaki kujibu haya maswali kwenye Biblia?

Kwanini hamtaki kujibu haya maswali kwenye Biblia?

Huyo mke alitoka wapi, embu tupeni majibu?
Ina maana hata wewe hujui mkeo alitoka wapi?

Biblia ipo wazi sana "zaeni mkaongezeke...."

Baada ya ndoa ya Adam na Eva wanadamu walizaliwa na wakazaliana, hadi leo hii wanazaliana na ndio maana na wewe ulizaliwa.
 
Kama yaliyo andikwa kwenye Biblia ni yale ya muhimu tu,

Hayo mambo mengine ya kwamba Adamu alizaa watoto wakike na wakiume kisha waka zaana wao kwa wao na kuongezeka, Umeyapata wapi?

Na umejuaje na unathibitishaje?

Haya mambo yasiyo ya muhimu ambayo haja andikwa, kwa nini hayaku andikwa?

Unathibitishaje yaliyo andikwa kwenye Biblia ndio ya muhimu tu?
????
 
Ina maana hata wewe hujui mkeo alitoka wapi?

Biblia ipo wazi sana "zaeni mkaongezeke...."

Baada ya ndoa ya Adam na Eva wanadamu walizaliwa na wakazaliana, hadi leo hii wanazaliana na ndio maana na wewe ulizaliwa.
Kabla dini hazijafika Africa miaka 200 iliyopita tulikua hatuzaliani kwani?
 
Habari zenu,

Naombeni majibu ya haya maswali kwenye maneno ya Biblia:

"Ukisoma mwanzo unaambiwa Adam na Hawa walimzaa Kaini na Habili, baadaye Kaini alimuua nduguye Habili. Baada ya hiyo hali Mungu akamfukuza Kaini (Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana akakaa katika nchi ya Nodi mbele ya Edeni). Kaini akamjua mkewe naye akapata mimba akamzaa Henoko."

Swali liko hapo; Huyo mke wa Kaini alitoka wapi wakati Mungu alikuwa ameumba watu wawili tu na walizaa watoto wawili na kati ya hao mmoja alikuwa amefariki? Huyo mke alitoka wapi, embu tupeni majibu?
Hadi Leo upo serious unaamini story za biblia. Ungeanza kuuliza nyoka aliongeaje ningekuona wa maana. Ungeanza kuuliza maji ya kujaza mafuriko dunia nzima yanatokea wapi ningekuona kidogo upo logical ? Achana na majibu ya wakristo kutetea kitabu Chao Cha katuni...ukweli ni hio ni story na zipo kibao Kama hizi katika dini za kale za middle east ni copy n paste n edit so zoea makosa mengi kwenye genesis story nyingi sio original ni oral traditions za watu wa jamii mbalimbali kipindi hicho
 
Adam aliendelea kuzaa Wana na mabiti hao wawili wametajwa Kwasababu walikuwa kwenye divine appointment
 
Kuna wengne wanadai bustani ya edeni ilikua ni maabara ya kufanya modification ya mtu, kutoka viumbe wa sayari za mbali , ndio wakatuletea hawa ngozi nyeupe wote , ila mtu ambae ni mweusi alikuwepo tu ,hao viumbe ni wana wa adamu, na ulikua ni mpango wa hao viumbe kuitawala dunia kupitia hao wanadamu ( weupe) dhidi yetu sisi watu , hizi ni dhana ambazo bado zipo kama story ila zinafkirisha coz inaaminika mtu mweusi kaishi miaka mingi duniani kuliko mweupe .
We unaongea Nini wewe
 
Sio balaa ww unaamini kabisa eti watu walijenga mnara kumfikia Mungu????
Leo hii watu wanaenda mwezini mbona hawamfikii huyu Mungu...sembuse ghorofa... afu eti lugha. Burj khalifa imejengwa na watu wa mataifa na lugha tofauti na limesimama...😂yaani genesis nzima ni kama animation tu
 
Hakuna cha kutunga. Kila kitu ni Halisia. Mwalimu wa wa theology alikueleza ukweli. Biblia katika mwanzo 5:1-2 inasema "Adamu alizaa wana wa kike na kiume". Mwanzo 6:1-2 pia inasema Wana wa "Wanadamu waliopoongezeka juu ya uso wa nchi, wana wa Mungu wakijitwalia wanawake miongoni mwao na wakazaa nao watoto"

Umeeleza vizuri na mwalimu wa theology alikueleza vizuri. Hawakuwa wanahesabu wanawake na pia wasingeweza kuandika majina ya watu wote wawe Bible Characters lakini baadhi ya maandiko nje ya Biblia"Abrahamic Texts" kama 'The book of Jubilee" kinaeleza mke wa Kaini alikuwa ni mmoja wa Dada yake yaani pacha wake aliyekuwa anaitwa "AWAN" na pia ndio chanzo cha kifo cha Habili kwani walimgombea Dada yao.
What's the historical evidence to back up this story? Au ni hekaya tu za abunuasi
 
Kabla dini hazijafika Africa miaka 200 iliyopita tulikua hatuzaliani kwani?
Kuzaana hakukuletwa na waeneza dini.

Ipo hivi watoto wa Adam walipozaana waliongezeka na kuenea kila pahali wengine walikuja hadi koromije na Gamboshi wapo huko mpaka leo.
 
Biblia haielezi umri wa Kaini wakati alipomuua ndugu yake Habili (Mwanzo 4:8). Kwa kuwa wote walikuwa wakulima, lazima wawe walikuwa watu wazima, hata pengine na jamii zao.

Adam na Hawa walikuwa wamepata watoto wengine mbali na Kaini na Habili wakati Habili alipouawa. Walipata wengi wengine baadaye mwanzo 5:4.

Ile hali ya Kaini kuhofu sana juu ya usalama wake baada ya kumuua Habili mwanzo 4:14 inathibitisha kulikuwako na watoto wengi wengine pia na wajukuu na hata vilembwe wa Adamu na Hawa.

Kwa kuwa Adamu na Hawa walikuwa wanadamu wa kwanza duniani, watoto wao hawakuwa na lengine ila kuoana.

Mungu hakukataza kuoana kwa jinsi hii mapema mpaka dunia ilipokuwa na watu wakutisha ndipo akakataza aina hii ya kuoana mambo ya walawi 18:6-18.

Sababu ya madhara ya ndoa za kaka na dada ni kwamba kama kila mmoja wao alikuwa na hali Fulani ya kilema ndani yaoya kurithi basi atakayezaliwa atakuwa mwenye kurithi kutoka kwa wote wazazi wawili, hivyo basi kuwa hali mbaya zaidi kuliko waliomzaa
😂Mpo serious na hizi sheria kweli...Mungu alisema msichanganye mazao kwenye shamba moja mbona hamfati
 
Habari zenu,

Naombeni majibu ya haya maswali kwenye maneno ya Biblia:

"Ukisoma mwanzo unaambiwa Adam na Hawa walimzaa Kaini na Habili, baadaye Kaini alimuua nduguye Habili. Baada ya hiyo hali Mungu akamfukuza Kaini (Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana akakaa katika nchi ya Nodi mbele ya Edeni). Kaini akamjua mkewe naye akapata mimba akamzaa Henoko."

Swali liko hapo; Huyo mke wa Kaini alitoka wapi wakati Mungu alikuwa ameumba watu wawili tu na walizaa watoto wawili na kati ya hao mmoja alikuwa amefariki? Huyo mke alitoka wapi, embu tupeni majibu?

Hayo maswali tumeshatoka huko. Ni maswali ya wanafunzi au watoto waliochini ya miaka ishirini.

Kwenye simulizi yoyote msimuliaji husikiliza matukio na wahusika wakuu kutegemea na dhamira na ujumbe wa simulizi yake.

Ni sawa na Uulize Mke wa Nuhu au Daniel, au Isaya, aliitwa nani?,
Au Uulize Mke wa Ishmael aliitwa nani?

Huwezi elezea kila kitu
 
Kuzaana hakukuletwa na waeneza dini.

Ipo hivi watoto wa Adam walipozaana waliongezeka na kuenea kila pahali wengine walikuja hadi koromije na Gamboshi wapo huko mpaka leo.
😂😂kumbuka katikati Kuna mafuriko hapo na Kuna babel pia...so eleweka watu walitawanyika lini
 
Back
Top Bottom