Kushanrishathaimu
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 220
- 347
Jibu ni kwamba Kaini alioa dada yake kwa sababu Adam alizaa watoto wa kiume na wa kike, Watoto wa kike hawakuwa wakitajwa sana kwa majina yao lakini walikuwepo.Habari zenu,
Naombeni majibu ya haya maswali kwenye maneno ya Biblia:
"Ukisoma mwanzo unaambiwa Adam na Hawa walimzaa Kaini na Habili, baadaye Kaini alimuua nduguye Habili. Baada ya hiyo hali Mungu akamfukuza Kaini (Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana akakaa katika nchi ya Nodi mbele ya Edeni). Kaini akamjua mkewe naye akapata mimba akamzaa Henoko."
Swali liko hapo; Huyo mke wa Kaini alitoka wapi wakati Mungu alikuwa ameumba watu wawili tu na walizaa watoto wawili na kati ya hao mmoja alikuwa amefariki? Huyo mke alitoka wapi, embu tupeni majibu?
"Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake."
Wakati huo hakukuwa na amri ya kukataza mtu kuoana na dada yake, amri ilikuja baadae kipindi cha Musa.