kwa harakaharaka, tangu enzi, mtu wa muhimu alikuwa ni mwanaume, wanawake hata wakiwepo walikuwa hawahesabiwi. hata unapoambiwa Yesu alilisha watu 5000 mikate, hao ni wanaume tu, wanawake walikuwa hawahesabiki. pamojana kwamba Adam na Eva walizaa Kaini na Habili awali, na baadaye seti baada ya kifo cha Habili, wapo wanawake pia walizaliwa out of them, pia jua watu hao waliishi miaka mingi sana duniani, kwamfano, Kaini aliishi duniani kwa miaka 730, na inasemekana kipindi anamuua kaka yake habili, alikuwa na miaka 130. kama adam alikuwa na mabinti, jua wakifikisha miaka 13 tu wameshavunja ungo, wanaweza kujamiiana na kupata mimba, toka miaka kumi na hadi miamoja, hapo unafikiri watu watakuwa wameshazaliana kiasi gani? habili na kaini lazima walilala na dada zao wakawazalisha watoto na ndani ya miaka 100 tu watoto wa watoto wao lazima watakuwa walishazaliana wao kwa wao. ukichukulia sasaivi, mtu hadi anafikisha miaka 100 anaweza kuwa na uzao hata 4 (kitukuu). hapo sasa huelewi kuwa ilikuwa rahisi sana kuzaliana na dada, mabinamu, ndugu kwa ndugu? cha msingi ni kwamba waliohesabiwa hao ni wanaume tu wanawake walikuwa hata kwenye namba hawahesabiwi kwasababu wao hawana uzao. hawazalishi.