Sina hakika kama Biblia huaga unasoma mwenyewe au hua unasoma vipande vipande.
Nitajaribu kukujibu hili swali lako kwa reference za Biblia hiyo hiyo, kwa ufupi hilo swali wala halijawahi kunitatiza au hata kunifanya nipate mashaka na historia ya uumbaji. Iko hivi, katika Biblia kuanzia mwanzo hadi mwisho, hakuna sehemu utapata historia ya mtoto wa kike kwa familia yoyote mule kwamba alizaliwa lini na alifatana na nani, again hata katika sensa kadhaa zilizofanywa (Kitabu cha Hesabu ni full sensa) walikua hawahesabu watoto na wanawake regardless their age. Kuna mtu anaitwa Yakobo or Israeli, huyu mwamba kazaa watoto 12 wa kiume na wanatajwa walizaliwa lini na kwa mama yupi, hakuna mtoto wa kike hata mmoja anaetajwa, baadae sana huko wakati hao watoto wote 12 wamezaliwa, anatokea binti yake mmoja kubakwa na watu wa taifa fulani na kumuondolea BIKIRA yake, ndio sasa tunakuja kumjua mama wa huyo binti na ndugu zake ni kina Lawi na Gadi...., you see? Means kama lisingetokea tukio hilo la ubakaji wala tusingejua kwamba kuna mtoto wake mmoja anaitwa Dina. Ipo kwenye Biblia. Again, huyu Yakobo baada ya kufika Misri, Biblia inasema mwamba alipiga copy 64, unajua tafsiri yake? Wa kiume ni 12 then 64-12 wanao baki ni wa KIKE. So sio ajabu kwamba Adamu alikua na watoto wengine wengi wa kike. Hata huyo Habili baada ya kifo chake, inaonekana kabla hajauawa alikua tayari ana mtoto/watoto. Means alikua kaoa. Fatilia uzao wa Yesu from Yesu mwenyewe rudi hadi kwa Adam, anaonekana anatokea uzao wa Habili na sio Kaini, so the question is, nae alioa nani?