Kwanini huwa tunalipia kodi ya pango la ardhi wakati ardhi tumeikuta ipo bure? Why?

Kwanini huwa tunalipia kodi ya pango la ardhi wakati ardhi tumeikuta ipo bure? Why?

Kwa mujibu wa Sheria, Hakuna Ardhi iliyokaa bure tu, Ardhi ni mali ya umma na msimamizi mkuu ni Rais, wewe unakuwa umepewa tu hati ya kuimiliki kwa miaka kadhaa lakini lazima uendelee kulipa kodi kwa msimamizi mkuu (Rais)
 
Kwa mujibu wa Sheria, Hakuna Ardhi iliyokaa bure tu, Ardhi ni mali na msimamizi mkuu ni Rais, wewe unakuwa umepewa tu hati ya kuimiliki kwa miaka kadhaa lakini lazima uendelee kulipa kodi kwa msimamizi mkui (Rais)
Aahajajaaaa

Rais ni mtu mkubwa sana aisee
 
Maji watasema kuna miundombinu ya kununua! Sasa ardhi ni ileile kama ilivyo hewa! Sasa kwanini tunalipia?
Ninaposema maji namaanisha mtu umechimba kisima chako nyumbani kwako, kesho yake wanakuja vijana na suti za mkia wa kondoo wanasema unatakiwa kulipia hayo maji kwa mamlaka ya maji wakati hawajawekeza hata senti
 
Mambo mengine mtu ukiwaza unaona kabisa maisha ni mepesi kimtindo lakini kuna baadhi ya wanadam wenye dhamana ya uongozi ndiyo waliyoyafanya maisha yawe magumu!

Tumeumbwa ardhi ilikuwapo, tumepata Uhuru, ardhi ilikuwapo milele hadi milele yote!

Sasa kwanini tunalipia kodi ya pango la ardhi wakati tayali ipo BURE?
Huduma zingine za kijamii tunazolipia naelewa ni sawa zinazalishwa viwandani hivyo ni mhimu kulipia!
Sasa hili la kodi ya pango ya ardhi kwanini tulipie wakati tumekuja duniani ili tuishi kwenye ardhi halisi BURE?
yaani kwa lugha nyepesi Ardhi ipo kundi moja na hewa! Kama tunalipia kodi ya ardhi kwanini tusilipie na kodi ya hewa?

Naomba kueleweshwa! Vinginevyo naomba serikali ifute hii TOZO ya ARDHI ya ardhi mara moja!r
Ardhi Haipaswi kabisa kutozwa kodi TUMEPEWA BURE ! WACHA TUISHI NAYO BURE!
Kodi ya ardhi sawa kwa sababu tunapata miundombinu ambayo kimsingi ni haki yetu.

Lakini kodi ya jengo ni wizi kwa mujibu wa sheria. Serikali inanidai vibali kabla sijajenga na hainipi unafuu wowote kipindi cha ujenzi. Vifaa vya ujenzi nalipia kodi na bado inanitaka kulipia kodi ya jengo.

Huu ni wizi unaolindwa na sheria.
 
Ninaposema maji namaanisha mtu umechimba kisima chako nyumbani kesho wanakuja vijana na suti za mkia wa kondoo wanasema unatakiwa kulipia hayo maji kwa mamlaka ya maji wakati hawajawekeza hata senti
Mimi walikuja kwangu nikawafungulia MBWA! Napenda haki ila ujinga SITAKI!
 
Ninaposema maji namaanisha mtu umechimba kisima chako nyumbani kwako, kesho yake wanakuja vijana na suti za mkia wa kondoo wanasema unatakiwa kulipia hayo maji kwa mamlaka ya maji wakati hawajawekeza hata senti
Hiki no zaidi ya kituko 😆
 
Kodi ya ardhi sawa kwa sababu tunapata miundombinu ambayo kimsingi ni haki yetu.

Lakini kodi ya jengo ni wizi kwa mujibu wa sheria. Serikali inanidai vibali kabla sijajenga na hainipi unafuu wowote kipindi cha ujenzi. Vifaa vya ujenzi nalipia kodi na bado inanitaka kulipia kodi ya jengo.

Huu ni wizi unaolindwa na sheria.
Hiyo miundombinu mbona tunailipia? Ingekuwa mtu akijenga anasogezewa Huduma zote BURE sawa lakini huduma zote tunauziwa ni BIASHARA!
 
Kuna kitu kinaitwa Universal Law hizi sheria zote unazoziona hadi Sheria ya kulipa Zaka na Sadaka zimekopiwa kutoka kwenye Sheria za Mama Ulimwengu (Mother Nature)
In short

Nothing is for free,hizo Kodi Kwa kifupi tunajikata sisi wenyewe na kuzichanga kwenye mfuko unaoitwa Serikali Ili zitufae wote(theoretically)

Nasema wote Kwa kuwa hii ardhi wanaimiliki walio Serikalini na wasio Serikalini Kwa kumiliki viwanja
 
Hii ni moja ya makosa yaliyofanywa na watangulizi wetu baada ya kupata uhuru. Nadhani wakati huo walioelimika aidha kwa kutokujua au kwa kufuata mkumbo tu waliamua kuweka mipaka ya nchi na kumilikisha kipande cha ardhi iliyopimwa yaani Tanganyika kwa kikundi kidogo cha wajanja wajanja kinachoitwa "Serikali".

Uporaji huu kwa jina la kupata uhuru na kujitawala ndio ulioleta haya mambo ya kodi kwa lengo la dude Serikali kupata pesa za kujiendesha kwa kukiuka misingi ya haki asilia ya mwananchi kumilika ardhi. Kimsingi Serikali ndio inapaswa kuwalipa wananchi kodi ya pango na kulipa fidia pale inapotaka kutwaa ardhi ya mtu.

Nchi hii inatakiwa kusukwa upya kwa kutengeneza katiba itakayo zingatia suala la ardhi kuwa mali ya mtu mmoja mmoja na sio huu ulaghai wa ardhi kuwa mali ya Serikali chini ya uangalizi wa taasisi ya Rais.
 
Back
Top Bottom