Kwanini huwa tunalipia kodi ya pango la ardhi wakati ardhi tumeikuta ipo bure? Why?

Kwanini huwa tunalipia kodi ya pango la ardhi wakati ardhi tumeikuta ipo bure? Why?

Wala sijataja dini yangu hapo,niko neutral.
Labda uniambie kwamba kuna mtu yeye anaamini uhai amejipa mwenyewe,na ardhi pia kuna watu wameitengeneza.
Ukishasema serikali ya JMT mambo ya Mungu hayapo tena, ndio raia na viongozi wana Mungu ila wakishakuwa katika muunganiko ukaitwa serikali hapo ni mamlaka na utii wa hayo mamlaka baasi.

Askari atapewa oda akuue na utauliwa na huyo askari ana Mungu ila hatafuata miongozo ya Mungu wake atatii mamlaka ya serikali yake.
 
S
Boss, kodi ya ardhi ipo kisheria kupitia bunge lako tukufu. Hakuna aibu hapo kuna sheria. Kama hatuitaki ni suala la kushinikiza mbadala bungeni pawepo mswada sheria ibadilike.
Sasa kumbe tunafanyeje hapa! Tunaomba sheria ibadilishwe kodi ya ardhi ufutwe
 
Hata kama ardhi tumepewa bure lakini bado ni scarcy commodity hivyo lazima iwe na gharama. pia hataka kama ardhi ni bure bado inahitaji Administration. na kuadminister kunahitaji fedha, hivyo lazima kuwe ada za kila wakati.

jambo limeundiwa hadi wizara na sheria so haliwezi kuwa rahisi kadili ya mawazo yako
 
S

Sasa kumbe tunafanyeje hapa! Tunaomba sheria ibadilishwe kodi ya ardhi ufutwe
Okey mkuu, sawa. Unapendekeza kiasi cha kodi kinachokusanywa kupitia kodi ya ardhi kikusanywe kupitia nn? Lets say serikali imetusikia, bajeti ijayo deficity itakayotokana na kuondoa mapato ya kodi ya ardhi itakuwa covered how?

Wanasiasa wenyewe wanatamani uwape huo mbadala 2025 majukwaani wapate la kusema.
 
Ingekuwa ni Mimi kiongozi ningefuta kodi ya ardhi halafu ile kodi ya jengo ningeibadilisha ikawa kodi ya huduma (government service/municipal service) hii inatosha kuhudumia kila kitu hadi kuzoa taka. Hakuna haja ya mwananchi kubughuziwa na mi tozo ya ziada
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Hujui kuna watu wanajiita mamlaka ya maji mijini wanakusanya fedha kwa watu wenye visima?
hilo sikujua nilijua unalipa ile ada yakuchimba ya mwanzo tu, kumbe kuna mwendelezo wa malipo hata baada ya kuchimba
 
Ingekuwa ni Mimi kiongozi ningefuta kodi ya ardhi halafu ile kodi ya jengo ningeibadilisha ikawa kodi ya huduma (government service/municipal service) hii inatosha kuhudumia kila kitu hadi kuzoa taka. Hakuna haja ya mwananchi kubughuziwa na mi tozo ya ziada
Okey boss. Nani atakidhi kulipa hiyo kodi ya huduma, analipa kwa kupata huduma ipi na kwa mfumo upi?
 
Wala sijachanganya mada,kuna mtu nilikuwa nimemjibu hiyo comment,aliniambia kuwa mimi sijui umuhimu wa kodi wala maana ya kodi ndio nikamjibu yeye anayejua umuhimu wa kodi ameona wapi hiyo kodi ikifanya kazi ipasavyo
... pitia kitu kinaitwa "the Great Survey" upate historia kidogo ya modern property act ilivyoanza huko UK middle ages around 1066 AD. Kodi ya ardhi ni kati ya kodi kongwe kabisa; 1000 yrs ago!
 
Hata kama ardhi tumepewa bure lakini bado ni scarcy commodity hivyo lazima iwe na gharama. pia hataka kama ardhi ni bure bado inahitaji Administration. na kuadminister kunahitaji fedha, hivyo lazima kuwe ada za kila wakati.

jambo limeundiwa hadi wizara na sheria so haliwezi kuwa rahisi kadili ya mawazo yako
.... na duniani kote hakuna nchi isiyo na wizara inayoshughulikia masuala ya ardhi ikiwa ni pamoja na kutoza kodi. Jina lake linaweza kusomeka vyovyote ila neno ARDHI halijawahi kukosekana.
 
... pitia kitu kinaitwa "the Great Survey" upate historia kidogo ya modern property act ilivyoanza huko UK middle ages around 1066 AD. Kodi ya ardhi ni kati ya kodi kongwe kabisa; 1000 yrs ago!
Sawa
 
Mkuu umeanzisha mada nzuri wengi tumefaidika na mijadala. Itoshe kusema kodi ya ardhi ni kati ya kodi kongwe, muhimu, na iko duniani kote.

Bila hiyo kuna walafi wangejimilikisha vijiji kwa hoja ardhi ni bure na wengine tungeishia kuwa manamba na vizazi vyetu for ever and ever.
 
Ndugu mwana JF
Ukitaka kujuwa serikali nini tokewa na mambo haya hapa.

Shamba lako likibainika lina-Alimasi linakuwa mali ya Serikali.
Ila shamba lako likibainika lina-Bangi hiyo ni mali yako mkuu! 😀
Naomba niishie hapa siwezi kuendelea hadi aje mwanasheria wangu!
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Haijaandikwa popote,

Nahisi tu

Ebu nielimish,ardhi ni ya nani!!
Ardhi ya nchi hii ni mali ya umma.

Ordinance No. 3 of 1923

It is a law deeper than the constitution itself.
Ina miaka 100 na miezi mitatu toka ilipopitishwa January 1923.

Ni nzee kuliko Katiba, ni nzee kuliko bunge lenyewe, ambalo liliundwa June 1926.

Ilitungwa na Gavana and Commander in Chief, Tanganyika Territory, Horace Archer Byatt.

Horace_Archer_Byatt.png

BE IT THEREFORE ENACTED by the Governor and Commander-in-Chief of the
Tanganyika Territory as follows:-

The whole of the lands of the Territory, whether occupied or unoccupied, on the date
of the commencement of this Ordinance are hereby declared to be public.
===============

Na akasimika kwenye sheria hiyo, Ibara ya 10 (g), inayosema mwenyeji (native ) au mjuba yeyote yule atakaefumwa amejaribu kumuuzia ardhi mgeni (non-native) atanyang'anywa ardhi yeye na mgeni wake.

Ndio mpaka leo ardhi ni kwa Watanzania tu, unless una kadi ya NIDA ya magumashi, mfumo unakusoma lakini unaishi kwa kujificha ficha tusigundue kwamba uraia wako ulishauza.
 
Back
Top Bottom