inamankusweke
JF-Expert Member
- Apr 24, 2014
- 20,344
- 21,967
Porojo,benguria
Hakuna peasant wa kiarabu aliyelipwa fidia,ilikua naqba,watu wameporwa na wanaendelea kuporwa Leo kwa msaada wa uingereza,mwanzilishi wa taifa la Israel benguria akiegemea turkey,alipobaini centre of gravity inaelekea west akafanya alliance na west,hakuna taifa si ulaya si marekani waliokua wanawahitaji wayahudi,ingekua Wana umuhimu huo Hitler asingewaokaUnasema "itoe Marekani na Uingereza nyuma ya Israel" sasa kwani ujanja wa Israel uko limited kwenye nini? Kwani mkuu aliyekwambia nikitaka kukupiga ni lazima nije mwenyewe nani. Hiyo ni sawa na kusema itoe polisi na NEC tuone CCM kama watashinda. Alliances zipo, za wazi wazi na za kimya kimya na huwezi lazimisha zivunjwe. Hao Waarabu wenyewe waliungana kwenye Israel Arab conflicts na walishindwa.
Ukianzia namna gani Jewish state ilianzishwa eneo la Palestina ambapo Waingereza walikuwa wanatawala. Ukafuata namna gani wale peasants wa Kiarabu walilipwa fidia na wengine kutimuliwa wakati nchi inaanzishwa, ukaangalia ile vita uchwara ya Wayahudi dhidi ya Waingereza pale Palestina utaona kabisa Myahudi alikuwa anafanya calculated moves.
Kwanza kabla ya hapo, wakati Britain inaingia WW1 miaka ya 1910s ilitaka support ya Wayahudi duniani na ikawaambia waiunge mkono ili ikiishinda Ottoman Empire ikate eneo la Palestina ambayo haikuwa nchi rasmi na haina mipaka ikiwa chini ya Ottoman. Baadae miaka ya 1930s mojawapo ya sababu ya Hitler kuwakataa Wayahudi ni kwamba wao duniani agenda yao ni moja, haijalishi huyu yuko Argentina na huyu yuko South Africa. Hawana uaminifu na serikali za nchi zao, wana nidhamu na jamii yao na agenda zao tu, ila hawavunji sheria bali mara nyingi wanagoma kuunga mkono agenda wasizotaka. Pale WW1 Ujerumani inapigana na Uingereza, wao Wayahudi agenda yao ni kuunga mkono Uingereza wapate nchi pale. Wakati humohumo Ujerumani kuna Wayahudi kibao, ila eti wanataka Uingereza iishinde Ottoman wapate nchi yao ya kudumu. Unahisi Waingereza walikuwa wajinga kuomba kuungwa nao mkono? Wanajua nguvu yao.
Wimbo wa taifa wa sasa wa Israel ulitungwa na Myahudi wa eneo la Ukraine ya sasa ila lilikuwa Austria ya Poland miaka hiyo ya 1800 (unaona mkanganyiko). Ila nchi wameanzisha 1948, so you can imagine agenda yao ilikuwa nini. Huwezi wapoteza kizembe wao wanawaza mbele, they have all options on their table.
Na kama unasema Cohen alijua siri za silaha za Soviet tu unakosea. Siri nyingine Wayahudi hawakusema, ila mojawapo iliyowasaidia wakati anafanya ziara kwenye kambi za kijeshi aliwashawishi majenerali wapande miti ya mikaratusi Golan heights ili wanajeshi walio kwenye outposts na kambi wapate vivuli. Lengo ni vita ikianza miaka ijayo, Israel pilots waweze locate positions za outposts. Rubani yuko jangwani ghafla anaona miti ya kijani, target destroyed!