Kwanini kelele za "Linda Mgongo" wanapigiwa wa kiume tu? Kwani mabinti wako salama?

Hoja imesimama hapa. πŸ‘πŸ‘
 
msome kiranga post #30 mkuu
 
Mimi naona ni propaganda tu za kututoa kwenye mambo ya msingi
Ndiyo maana mimi nikasema Wabongo wengi hawajui wanataka nini.

Mtu anapigania katiba mpya itakayotoa uhuru zaidi kwa kila mtu.

Sawa.

Lakini, akija mtu mwingine anataka uhuru wake kuwa shoga, anapigwa vita.

Mnataka uhuru wa mtu binafsi kuamua kuishi anavyotaka au hamtaki?

Mnaelewa freedom of sexual orientation ni uhuru wa mtu binafsi pia?
 
Hii ni sawa na kipindi cha kampeni ya Black Lives Matter,kuna watu nao wakaanza kampeni Ya White Lives matter too,.watu waliokua katika kampeni ya Black Lives matter wakawa wanachukia wakitafsiri kama White Lives matter ni protest against their protest wakati kihualisia maisha ya kila mtu yana thamani bila kujali rangi au jinsia..

Kama watu wanajali sana migongo, kampeni iwe general principle sio 'mtoto wa kiume Linda mgongo wako'
 
hivi hii inaweza kutumiwa na ccm kama point ya kupngza mashinikizo ya katiba kwa namna moja ama nyingine?

au tuseme kupunguza baadhi ya madai?
 
Hawawezi kufanya kampeni general kwa sababu wengi wao wanamendea migongo ya wanawake.

Halafu wanapinga ushoga.

Wao wana tatizo na mwanamme kufirwa, kwa mwanamke ni sawa.
 
Mambo ya msingi yapi?
Kuna mambo mengi ya msingi ya kujadili ila sio mambo ya chumbani ambayo watu wazima wanafanya kwa kuchagua wenyewe kwa utashi wao

Mwaka 2019 katika interview na BBC(HARDtalk) Lissu aliulizwa kuhusu sheria za Tanzania zinazo kataza mapenzi ya jinsia moja,Lissu alijibu

"Haki ya mtu ya faragha ilindwe serikali haipaswi kuingilia kinachotokea katika maisha binafsi ya watu,hasa ndani ya vyumba vyao"
 
Hawa hawajui hata Katiba ni nini achilia maana ya uhuru.

Haki ni haki pale tu ambapo inawahusu wao. Kama haiwahusu hiyo si haki.
 
Subiri uje uambiwe wewe ni shoga, πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Tena umesema na lissu, watamgeuka wafuasi wake sasa hivi
Huwajui wabongo wewe.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…