Kwanini Kikwete hakumshauri Samia amteue Prof. Mwandosya kuwa Makamu wake wa Rais?

Sikuhizi Hana professional arrogance
Hivi ukimsema Mwandosya alikuwa na professional arrogance, Mwakyembe je, aliyetamba kuwa na degree nne!

Halafu kulikuwa na Tuntemeke Sanga bwana, ambae alikuwa na degree saba sijui, akamwambia Nyerere hakuona kazi ya kupewa na serikali hapa Tanzania, labda awe raisi! Alifungiwa kijijini kwao hadi Nyerere alipong'atuka!
 
Mwandosya na ujeuri wake, kiburi na Kujifanya ana akili nani amuweke?

Yule ni Mr.Haambiliki angemsumbua Rais..
 
Wote walipigwa chini na Proffessional arrogance zao walipogombea nafasi kuanzia Mwandoshya alipigwa chini alipogombea uraisi,Mwakyembe na Tumtemeke Sanga wote walipigwa chini walipogombea ubunge kwao na walipigwa chini na watu wa Elimu ya chini sana
 
Kwa hiyo umeamua kuja hapo kujipigia debe? Wazee wengine ni shida tupu!!! Mbona hajabadilisha chochote cha maana huko kwao Busiokelo ambako alijichimbia muda mrefu huku akijihusisha kumubagaa hayati JPM kupitia mitandao ya kijamii?
Kwa hiyo mnatak kumwuua makamu wa rais aliyepo ili nafasi hiyo apewe yeye? Inaonesha wewe una nia OVU
 
Kwa point kama hizi ndio unajiita Intelligence Justice? Badilisha uwe Idiotic justice
 
Wote walipigwa chini na Proffessional arrogance zao walipogombea nafasi kuanzia Mwandoshya alipigwa chini alipogombea uraisi,Mwakyembe na Tumtemeke Sanga wote walipigwa chini walipogombea ubunge kwao na walipigwa chini na watu wa Elimu ya chini sana
Halafu utakuta vilaza wa shule ndio wanatoa maamuzi ya kupiga chini vipanga wa shule.

Ule msemo kwamba waliokuwa vilaza darasani ndio wanaongoza nchi na kuwaamulia mambo na kuwapangia mishahara waliokuwa vipanga wa darasani ni kweli kabisa. Tumekuwa na awamu raisi na diploma ya ualimu anawafukuza kazi maprofessor eti wa kuwa hawako serious na kazi, kina Msukuma wanawatungia sheria watu na degree zao hadi saba wakati hawajui hata kuongea sentensi moja ya kiingereza, yeeewiii!!!
 
Mwandosya na ujeuri wake, kiburi na Kujifanya ana akili nani amuweke?

Yule ni Mr.Haambiliki angemsumbua Rais..
Na alipokuwa Waziri asiye na Wizara Maalum akimsaidia Kikwetealimsumbua kwa jambo gani?

Unajua watu wasio na uwezo mkubwa kichwani siku zote wanawaona wenye uwezo mkubwa kichwani wana kiburi.

Inaitwa intelligence inferiority complex. Ni ugonjwa mbaya sana. Tukiwa shule ukiwa kipanga unapewa majina ya utani nk na wale walio na inferior intelligence. Hukuona hilo, au wewe ulikuwa kwenye kundi la kutoa majina kwa vipanga?

Sasa kwa tunaomfahamu Mwandosya, hajifanyi ana akili, bali ana akili kwelikweli.
 
Ndio maana alipuuzwa kwa kupewa hiyo Wizara isiyo na bajeti
 
Ndio maana alipuuzwa kwa kupewa hiyo Wizara isiyo na bajeti
Wale wote wasio na akili hawaelewi maana ya kuwa Waziri Usie na Wizara Maalum. Hicho cheo ni sawa na Waziri Mkuu asiye rasmi juu ya Waziri Mkuu aliye rasmi. Ndio maana Ofisi ya Mwandosya kama Waziri Asiye na Wizara Maalum ikawa Ofisi ya Raisi, wala sio Ofisi ya Makamu wa Raisi au Waziri Mkuu. Bajeti yake inakuwa kwenye bajeti ya Ofisi ya Raisi Lakini huwezi kujua hilo
 
Porojo za kujifariji
 
Porojo za kujifariji
Kaulize ujione usivyojua haya mambo bali unaropoka tu, hana bajeti. Kama hana bajeti alitendaje kazi kwa niaba ya raisi?

Kwa taarifa yako, hata Waziri Mkuu anakuwa wa pili kujdili uteuzi wa mawaziri, baada ya raisi kujadiliana na waziri asiye na wizara maalum. Hata waziri mkuu anakuwa hana mamlaka juu ya waziri asiye na wizara maalum
 
Wapi alitenda kwa niaba ya Rais? Porojo za kujifariji kwa kuwa Chawa na mnoko.
 
Hizi ni fikra zako mkuu, hao viongozi wote wanaishi pamoja huko juu na wanajuana vyema nani ni nani na anajua nini, mi siamini kama kikwete anamshauri mama samia, hao wote ni viongozi wa ccm na lao ni moja, kama nchi ikiharibika tatizo ni ccm sio viongozi waliopewa nafasi unaeza kuta rais mshauri wake mkuu ni katibu wa chama sio mawaziri wala makamu wa rais

Sent from my Infinix X624B using JamiiForums mobile app
 
Hebu onesha alichokifanya hadi unampigia debe wewe unayejiita 'Kisanishi'
 
Haya, endelea kuishi kwa imani, acha reality ikupite
 
Wanyakyusa wako blessed sana and very wise. Ukigombna na mnyakyusa basi jua wewe ndio mkorofi
 
Wanyakyusa wako blessed sana and very wise. Ukigombna na mnyakyusa basi jua wewe ndio mkorofi

🤣🤣
..kila kabila / jamii ina watu wema na watu wa hovyo-hovyo.

..sasa hapo unapowataja Wanyakyusa kwa upole, umemsahau Jimmy Ngonya " Gobarchev" kiongozi wa Simba aliyeshindikana kwa kiburi chake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…