Kwanini Kikwete hakumshauri Samia amteue Prof. Mwandosya kuwa Makamu wake wa Rais?

Wanyakyusa wako blessed sana and very wise. Ukigombna na mnyakyusa basi jua wewe ndio mkorofi
Mkuu unaonekana hujapambana na Wanyakyusa wa Kyela unawasema Wanyakyusa wa Tukuyu! Tukiwa shuleni mgomo ulikuwa unaanzishwa na Wanyakyusa wa Kyela. Wakisema Aiseeeee, ujue mgomo unaanza!😅😅😅

By the way, Prof. Mwandosya ni Mnyakyusa wa Tukuyu, na Dr. Mwakyembe Mnyakyusa wa Kyela. Unaona tofauti eeh?
 
John Mwakangale aliyetajwa kwenye Long Walk to Freedom alikuwa ni wa wapi?
 
Mwandosya na ujeuri wake, kiburi na Kujifanya ana akili nani amuweke?

Yule ni Mr.Haambiliki angemsumbua Rais..
Hapana, kwa sababu sio yeye ambae angekuwa anaambiwa bali yeye ambae anamwambia Samia, na Samia angekuwa na uhuru na uwezo wa kukubali anachoambiwa au kukataa
 
Lakini kama una habari za ndani utakumbuka kwamba climax ya yote ilikuwa ni Prof. Mwandosya kuamrisha meli iliyoleta mafuta machafu ya TIPER iondoke nchini ndani ya masaa 24, kitu ambacho Kikwete alipinga akidai wasamehewe.
Kwa namna Serikali ya Tanzania inavyofanya kazi, karibu mkuu hawezi kuwa na power ya kutoa 24hrs meli iondoke. Yaani ultimatum ya 24hrs na ikizingatia yuko against na Waziri. Katibu mkuu anaweza kutengeneza biti na mabishano ya hapa na pale lkn si kutoa saa 24 meli iondoke Tanzania (bila maelekezo ya Waziri au Rais).
 
Okay. Labda tuseme hakulazimika kutoa masaa 24 bali alisema piga ua hiyo meli isingeshusha mzigo wake TIPER. Kumbuka, TBS na wipimanji wengine walishasema ile crude ilikuwa sio ya standard na specifications za TIPER, kwa hiyo hata asingewapa masaa 24 wangefanya nini, wakae tu wakisubiri huruma za Prof. Mwandosya? Prof. yeye alisimamia ripoti za vipimo vya quality ya crude na specifications za TIPER, wakati Kikwete alitaka wafanye waiver na kuwasamehe kwa kuleta substandard crude oil. Management ya TIPER ilikuwa inalalamika kuwa hata huko nyuma walikuwa wanalazimishwa kupokea substandard crude. Na hichi ndio kilimuudhi Prof. Mwandosya, kwamba Kikwete siku zote alijua walikuwa wakileta crude isiyofaa. Kikwete akajitetea mtoto wa Mkulu alikuwa na hisa katika huo mzigo. Prof. Mwandosya akasema nonsense, hata angekuwa Mkulu mwenyewe asingeruhusu crude ipakuliwe. Unaona palivyokuwa patamu?

Hiyo issue bwana ilienda hadi Ikulu, lakini ilikuwa awkward sana kusuluhishwa Ikulu kwa sababu za personal interests. Ila meli iliondoka. Serikali ya wakati ule wee isikie tu. Kina Prof. Mwandosya ambao wanafuata ethical principles wasingedumu kwenye ile serikali. Kikwete mtoto wa mjini yeye alijifitisha popote pale, akiangalia upepo.

Ndio maana akawaambie kwa confidence mno, mie bwana ni lecturer wa UDSM. Nilikuwa appointed kuja wizarani kutokana na utaalamu wangu, haikuwa political appointment. Kama mnaona si-fit kwenye domain yenu acha nirudi zangu chuoni kufundisha vijana. Msitegemee leo nitakuwa Katibu Mkuu Nishati, kesho mnipeleke Wizara ya Utamaduni na Michezo sijui! Wapo Makatibu wakuu wa namna hiyo, ambao ukatibu mkuu ni career, lakini sio mimi. Yaani kwa kauli hii nilimpenda Prof Mwandosya - aliwapa vidonge vyao🤣🤣🤣🤣
 
..Mark Mwandosya ni msomi wa kweli sio mbabaishaji.

..huyu ni mmoja wa " Tanzania One " wa miaka hiyo.
Kwa sasa tuna tatizo la Bunge la Ulaya kusema ile pipeline ya mafuta kati ya Tanzania na Uganda isijengwe. Yaani Prof. Mwandosya ni mtu muafaka wa kutusaidia katika hili. Huyu January Makamba hataweza lolote hapo, kwanza hana charisma na confidence ya kuwaweka sawa hawa watu wa Bunge la Ulaya. Nani atamsikiliza? Abaki akijibu hoja za mambo ya Crane za Nyerere Hydopower project na kwa nini umeme unakatika, local stuff.
 
Yaan hii nchi imechoka sana.Kikwete ni failure wa muda wote .Yupo tu kwa ajili ya katiba mbozi ya Nyerere.Leo ndio awe mshauri ?Tunazid kuanguka kwa ajili ya huyi Mzee asiyejitambua
Sasa mtu kama Jiwe eti akawa Rais
 

..sidhani kama ni mgogoro mkubwa kiasi hicho.

..kwanza makampuni ya hukohuko EU yanahusika ktk ujenzi.

..pili njia itakapopita hilo bomba ni rafiki zaidi kwa mazingira na gharama kuliko lingepitia Kenya.

..muelekeo ya Kenya kuna miinuko na vyanzo vingi vya maji kwa hiyo hatari kwa mazingira na gharama zitakuwa kubwa.

..naamini ni suala la kupeleka wawakilishi wetu huko EU kuwatotoa wasiwasi wadau wetu wa maendeleo.

..tatizo tuna watawala wanaochukia kuulizwa au kuhojiwa kwa maamuzi yoyote wanayoyafanya. They are very good at making decisions but pretty bad at justifying or explaining them.
 
Umemsikia Museveni alivyoongea? Tayari anakebehi na kusema hivi visichana vidogo huko Ulaya leo vinataka kutuambia nini cha kufanya?

Sasa katika mambo ya diplomasia hatuendi hivyo. Huwezi kuwa confrontational na hizi nchi ukashinda. Always diplomacy inashinda, na ndio maana suala la rada Prof. Mwandosya aliliweza kirahisi sana.
 
Mi naona angeitumia elimu yake kuinufaisha nchi ili wanaosoma waone manufaa ya elimu.
 
Mkuu,wakati haya yanatokea,wewe ulikua umejibanza wapi unasikilizia?
 
Kwa hiyo makamu wa Rais aliyepo hafai ? Kila mtu na wakati wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…