Kwanini kila anayeondoka CHADEMA anamtaja Mbowe?


Hata Nyerere aliambiwa hivyohivyo, ukiiachia Tanzania itafutika lakini mpaka leo ipo. Mbowe must go
 
Wewe acha upuuzi Mbowe ndiye chanzo cha Chadema kufa baada ya kukiuka misingi ya Chadema kitupa wapambanaji akina Slaa na kumleta Lowassa na kuumpa nafasi kubwa ya kugombea urais kupitia tiketi ya Chadema pasipo kufuata katiba wala kanununi za chama,tokea hapo kuyumba kwa chadema kulianzia hapo haya Mambo ya ununuzi ni Propaganda za kushindwa tu, Maana Wakati wa akina Slaa walisha wahi fukiza madiwani hapo Arusha walioonekana kukiuka misingi ya chama,nawakashinda hivyo viti vya udiwani.Magufuli nikisingizio tu cha kifo cha Chadema,aliyeuwa chadema ni Mbowe kwa tamaa zake ila machawa Mbowe hawataki huu ukweli, Sasahivi miaka 3 Magufuli hayupo mbona chama bado hakina mwelekeo?Achani kujificha kwenye kivuri cha Magufuli hata hakina Zitto walitoka Kabla ya Magufuli je hao walinunuliwa nanani?
 
Mbowe huyo mnayemwogopa sana nyie CCM unafikiri sisi CHADEMA tutamtoa?
 
Mbowe kinara wa kukimbiza wenzake
 
Mbowe ndio engine ya CHADEMA, hakuna anayewaweza isipokuwa huyu, waondoke CHADEMA haitakufa, kama MAGU, alishindwa ndo hu KIROBOTO mmoja?!
 
Lengo la chama cha siasa ni kushika Dola.
Kama umekua mwenyekiti kwa muda mrefu na umeshindwa kushika Dola achia wengine.
Naiona CHADEMA ya mwenyekiti Lissu ikifanikiwa Sana kuliko ya Mbowe.
Lissu huwa harudi nyuma kwenye ukweli na CCM watashirikiana na yoyote wanaemmudu ili Lissu asiwe mwenyekiti maana hawammudu.
Hata maridhiano Lissu alinusa mapema Sana kwamba CCM inawapumbaza lakini kuna viongozi walishupaza shingo na kuchelewa Sana kuelewa sijui ni kwanini.
 
Feisal alivyoondoka yanga alimtaja engineer daah lakini engineer naye ni binadamu tu bado yanga ya moto nawasifu japo mimi ni simba,uongozi una mambo mengi hata hapa tulipo tuna amani bwerere,lakini kuna watu hawamkubali mwalimu Nyerere may his soul rest in peace
 
Mbowe mpe muda hadi tumalize mchakato wa kupata katiba mpya.
Hakuna democracy ya kweli kama katiba ya nchi yenyewe ina mapungufu ya democracy.
Ukimuondoa leo Mbowe Chadema haitachukuwa muda mrefu kuwa kama vyama vingine vidogo.
Wafadhili wa Chadema wakishirikiana na Mwenyekiti Mbowe ndio wanaiweka Chadema barabarani.Tusisahau hilo,hata Mjomba Magu pammoja na kuwanunua bila kificho wabunge na makada maarufu lakini Chadema iliendelea kutamalaki.
Mitafaruku katika vyama hua ipo na hutatuliwa na vikao rasmi vya chama.
Mgogoro kati Mchungaji na uongozi wa Chadema nadhani utapata uvumbuzi.
 
Sawa tuwekee na Wanoondoka ccm kwenda cdm Huwa wanasemaje?

Hii project ya tiss na Lumumba
mbona imefeli kabla

Hamtutoi kwenye ajenda ya msingi ya kuhoji uuzwaji wa rasilimali zetu

Hayo Mambo ya kuhama cdm ni mambo madogo sana
 
Kwa sababu lengo la waliowatuma wanamuona kuwa ni tishio kwao. Hivi wanataka tuamini kuwa isingekuwa Rais anabanwa na Katiba kuhudumu kwa terms mbili tu, wenyeviti wao wangeachia uongozi ? Wao badala yake wanafanya nafasi zao kuwa za urithi! Hiyo ni mbaya kuliko kiongozi wa chama cha upinzani kuongoza kwa miaka 30.
Hao wakina Pendeza, Lijualikali, Zitto walijijenga wakiwa chini ya uenyekiti wa Mbowe. Wangekuwa upande wa pili wasinge fika walipofika wakiwa chini ya Mbowe. Na wote tunaona jinsi nyotazao zinavyo fifia wakiwa huko kwenye neema.

Amandla...
 
Swali zuri sana hili
 
Hahaha mipango ya CCM. Kama mmemsikiliza MSigwa anasema, Magufuli alikuwa anamshauri sana ahame Chadema aende CCM lakini akamwambia nitakusaidia nikiwa huku(CHADEMA). Kuna kitu alikuwa kaagizwa kufanya, hakuweza kukipata.

Alitaka nafasi ya juu ili akihama awe gumzo, CHADEMA walimuelewa mapema, wakaamua kumuweka anapostahili, ili akiondoka, asiwe na impact yoyote, na sasa ndipo alipo.

Mbowe ni mwiba kwa CCM, wao walitaka vyama vinavyowekwa mifukoni mwao(CCM). Lakini CHADEMA imekuwa tofauti, imekuwa kama mende, ukimuua kwa kumsigina, umemsaidia kueneza mayai na watazaliwa wengi zaidi.
Demokrasia gani wanayoitaka, Kule CCM Magufuli alimfukuza SOFIA SIMBA, na Benard MEMBE kwa kutofautia naye siyo chama, na ilionekana sawa.

Huku wanaoondoka wanakuwa Ma agent wanaotaka kufanikiwa lakini wanakosea, wanaondoka chama kinaerndelea kustawi, ni kama magamba ya nyoka, yanapotoka ndio nyoka anapendeza.

Binafsi naona waondoke tu, na ikiwa wanataka Mbowe aondoke, basi watafute njia nyingine hii ya kumtuhumu iliishashindwa.
 
Kingine ulichosahau kuuliza ni hiki, kwanini hawa unaowasema wakiondoka Chadema huko waendako wanapewa vyeo, na kuwapiku wanaccm wa miaka mingi wafia chama?

Ukiunganisha hoja hizi mbili tunaweza kupata jibu kirahisi sana
Nakusalimu Mzee Mbowe
 
Ngo πŸ“ŒπŸ”¨ Ngo πŸ“ŒπŸ”¨ Ngo πŸ“ŒπŸ”¨
 
Nimekuja kugundua hiki Chama kimejaa uhuni mwingi,

Kwanini mtu aachwe Mwenyekiti miaka 30 huku akifukuza huyu na yule?

Sasa lengo la vyama vingi liko wapi si Bora tuseme CCM ibaki madarakani milele kama Upinzani hata kujiongoza tu hamuwezi.
Ngoja tuone itakuwaje
 
Kingine ulichosahau kuuliza ni hiki, kwanini hawa unaowasema wakiondoka Chadema huko waendako wanapewa vyeo, na kuwapiku wanaccm wa miaka mingi wafia chama?

Ukiunganisha hoja hizi mbili tunaweza kupata jibu kirahisi sana
Mbowe ni king'ang'a ,kigando,ruba ,kupe hatoki wala atolewi ni ayatollah mtupu,kiufupi ni mr slim mwingine,au Mu7
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…