Kwanini kujenga nyumba imekuwa ni fashion kwa Watanzania?

Najiuliza mnoo,hii mentality tulirithishwa na nani? Yaan kila mtu ndoto pekee ni kujenga..eti reason ni kodi ya nyumba..mtu hawazi kukuza uchumi wake
 
Kuna biashara yoyote unayofanya? Na km unabiashara mpaka sahizi umefikia wapi? Je unakiwanja,umejenga? Je una gari? Ukinijibu hili nitakuja ku comment
Unataka kumjua mtu ambaye ata jina analotumia ni feki? Unataka kujua investment nilizofanya nitakuaminishi vipi wakati hunijui rudi kwenye mada husika tuendelee kujadiliana kama ni sawa au sio sawa
 
Mimi nadhani mleta mada ana akili na tabia za kikubwa kuliko wewe uliyekuja kumshambulia moja kwa moja badala ya kujadili hoja zake.

Una mentality ya kichawi na kifukara sana, hii itakusumbua sana.
 
Mafanikio makubw ya wabongo ni kujenga, matokeo yake wanazika pesa kwa kujenga vitu visivyoeleweka.
 
Hata kama unafanya biashara jiwekee mikakati ya kujenga nyumba ya ndoto zako mapema.
Ukiwekeza sehemu salama na ukajikita katika kuukuza uchumi wako huku ukijipunguzia stress za matumizi ya pesa (kama kujenga kwa kudunduliza), basi mambo hayawezi kuwa mabaya.

Hiyi nyumba ya ndoto unayodai utaijenga ndani ya miezi miwili tu ukiwa na uchumi mzuri, badala ya kuishi ukijenga nyumba ambayo utakuja kuikamilisha uzeeni, tena ikiwa imeshapitwa na fashion.
 
Hata kama unafanya biashara kumiliki ardhi na kujenga ni muhimu sana. Wajanja wote kwenye biashara wako mstari wa mbele kumiliki ardhi na kujenga.
Kimikiki ardhi ni jambo lingine tofauti na kuamsha ujenzi ambo hauumudu, mtu unakuta anajenga nyumba kwa miaka 20 ikiisha tayari ilishatoka kwenye form na imezeeka.

Miliki viwanja kadiri uwezavyo kisha imarisha uchumi wako ili unapoanza kujenga unakuwa ni ujenzi wenye kueleweka.
 
Nakuunga mkono. Wengi hawatakuelewa.
Nyumba nyingi zinazojengwa ki ukweli ni za viwango duni na zisizo na mpangilio imara kwenye miji yetu. Pia nyumba ina incur liabilities nyingi. Kinachopanda thamani si nyumba bali ni ardhi kwa sababu nyumba iliyowahi jengwa miaka 20 nyuma haiwezi fanana na nyumba za kisasa. Bali thamani ya ardhi hubaki vilevile ama kuongezeka zaidi, ni nadra thamani ya ardhi kupungua.
Kiasi ambacho mtu amekifukia labda tuseme zaidi ya milioni 20 mtu huyo angeweza kujiendeleza vizuri kibiashara na kuwa mshindani mzuri kwenye masoko.

Wengi hujenga nyumba wakitaka security, kwani huogopa kiasi ambacho wangeweza kuwekeza labda pengine kingefilisika na hapa ndipo watu wengi hubakia static katika kujiendeleza kibiashara.
 
Siku mkeo atakapopigwa Pu**mbu na mwenye nyumba wako,
Ndy siku utakayojuwa umuhimu wa kukaa kwenye nyumba yako hata kiwe chumba kimoja.

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
Na siku mkeo atakapopigwa pu*mb na kashikaji fulani humohumo kwenye kachumba kako kamoja, ndio utajua kuwa watu hawatakiwi kujenga kwa kuogopa kupigiwa wake zao.

Hiyo haiwezi kuwa sababu makini ya kwanini mtu ajenge.
 
Wkt nafanya biashara yangu ya kiduka,sehem nilipokuwa nafanya bizinesi nilikuwa Sina mpinzani kivilee so nilikuwa nauza sana,so nikaanza kuongeza vitu kila nilipokuwa napata faida,zaidi nilikuwa nalipa Kodi na ghalama zingine ambazo zilikuwa zinahusiana na biashara na Mimi pia,xo nikawa na malengo ya kupanua zaidi biashara yangu kwa kuongeza bidhaa zaidi Ila Sasa gafla watu walivyoona dogo dizaini napata Sana wakaanza kufungua na wao mtaa huo huo,nikaanza kupambana Ila kadri siku zinaenda nikaona mauzo na faida inapungua kadri siku zinaenda,hapo muhuni Sina hata shamba ni Mimi na duka langu tu Yani ikitokea siku duka linaungua Sina kitu naanza ziro,mtaji ukaanza kupanda na kushuka dizaini TRA,manisipaa na mazaga mengine nikaona hapa mtaji utaisha alafu nitakuwa sijafanya kitu hapa,nikaanza kununua mashamba kwanza maana uwezo kwa kununu kiwanja center uongo,gafla mzee ikatokea Corona virusi nilijifunza Soma gum Sana kuwa Kuna siku itatokea nitabaki na pum** zangu mbili tu 😄, biashara ya bongo nyoso Sana kati ya sehem nilizopata nikasema sehem gani nitaweza Jenga hata kibanda Cha chumba na sebure na baada ya miaka kadhaa naweza fanya kitu,nikona sehem moja ipo barabarani na mtembeo wa dakika tatu Kuna zahanati na shule ya msingi nikafanya hivyo nikapiga bati sahiz nimetulia ni sehem ambayo mpaka leo japo sijamaliza Ila inanipa matumaini ktk kipindi kigum ninachopitia,lengo kubwa ni kuweka ka frem kamoja na kufanya ufagaji
 
Risk ya biashara hapa kwetu ni kubwa kuliko kujenga nyumba..

biashara hazitabiriki hapa nchini so bora ujenge tu ujue pesa umeizika..
Sasa nyumba ya kuishi unawezaje kuiita asset?

Au mimi ndio sijui maana ya asset?
 

Sema umri wako, maisha kwako bado ni nadharia, huu ujuaji unamalizwa na umri, sio maelezo, hutaelewa.
 
Unataka waishi maisha ya kiaje?.
 
Tunajenga sababu sekta ya makazi ya kupanga kwa tz bado haijaweza kutoa utulivu kwa mpangaji na akawa na amani,yaani inshort hii sekta kwa tz imekaa kihuni haikupi guarantee ya maisha yako,mwnye nyumba anaweza akakutoa muda wowote anaotaka yeye,masharti mengi hayapo kisheria,huwez kukatia bima nyumba ya kupanga kwamba ukiyumba kiuchumi ulipiwe kodi,pindi ukifa au ukiugua au ukiyumba kiuchumi familia yKo ni rahisi sana kudhalilika ndani ya muda mfupi,ndo maana kila mtu mwnye future na maisha yakw kwanza anatafuta utulivu wa makazi ili aweze kufocus kujijenga kiuchumi,mm naamini huwez kutulia kujijenga kiuchumi kama huna makazi ya uhakika,kipato changu kwa kwanza kwanza nilitumia ktk kujenga kwanza ndo nikahamishia nguvu ktk biashara,japokuwa biashara zina ups n down lkn kidogo unakuwa na utulivu wa nafsi jioni ukirudi kwako naukiiona familia yako inaishi kwa amani wakipanga mipango yao pasipo kuhofia kutolewa nyumbani etc
 
ni vizuri kua na sehemu yako ya kupumzisha mwili na akili unapotoka kwenye mizunguko ya kutafuta riziki,sio unarudi home unaanza kupambana na majirani wapunguze sauti za redio ili upumzike 😀
Sasa mtu mwenye uwezo wa kupanga sehemu ambayo kuna majirani wapiga mziki na muingiliano wa watu, hapa si unazungumiza kodi ya 50K-60K ?

Sasa huyu nae apambane kujenga, kwa kipato kipi? Na hata akianza ataimaliza lini, au ndo kujenga nyumba ya vyumba viwili kwa miaka 20? Kwanza hicho kiwanja atakipata katika mazingira gani na je kitakuwa karibu na sehemu ya mihangaiko yake ya kila siku?

Huyu anatakiwa akuze kipato kabla hajawaza kujenga, akuze kipato ahamie sehemu zenye utulivu, kisha akuze kipato kitakacho mruhusu kujenga bila stress.

Ukiwa na uchumi unaoleweka, nyumba unaijenga kwa miezi miwili tu.

NB: Kitu pekee cha kushauri vijana ni kununua viwanja kwa kadiri wawezavyo, iwe ni maporini au mijini kulingana na uwezo wao.
 
Ngumu watu kukuelewa. Wengine wanakuja na matusi na kejeli. Ukweli ninaouona ni kuwa Watanzania wengi sio wafanyabiashara. Ai unadhani ni wafanyabiashara wanafanya baada ya kukosa kazi. Wanaziogopa hela. Wanahofu kuzipoteza. Sasa njia pekee ya kuzitunza ni kununua viwanja na kujenga.

Kingine ni jamii, jamii yetu unaona ufahari ni kujenga hata kama ungekuwa una mali kiasi gani. Hata kununua apartments hakuonekani kama kujenga.

Wahindi wanaishi kwa kupanga wakizungusha hela zao mpaka wanazeeka.

Mtu yuko tayari kujenga Bunju, Chanika, Kigamboni halafu anarumia 600,000 za mafuta kuliko kupanga flat ya 400,000 akatembea kwenda kazini kwake.
 
Mkuu Iringakwanza nakuunga mkono kwa maoni yako, but kwa kiasi kikubwa waafrika hatuna mawazo endelevu hasa katika uwekezaji wa miradi hilo ndilo tatizo letu.

Issue ya kodi si kitu kikubwa kama una income isiyokoma, tatizo wengi wetu ni jua limechomoza siku ya pili*

Ukikaa na wenye akili zao wanakwambia wekeza kwanza kwenye miradi itakayokupa uhakika wa pesa ukiona umekomaa sasa, ndipo unakuwa na uwezo wa kufanya lolote as ukaishi wapi, coz ujenzi wa haraka kisa unakimbia kulipa kodi ni unajenga 'kwa kulazimishwa si kwa kupenda'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…