Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Mkuu,Mbona we mwenyewe hujathibitisha uwepo wa nguvu inayokufanya uishi (roho/hewa) iwe visible na tangible zaidi ya kuhisi tu?
Sauti je?
Akili je?
Unaelewa "logical non sequitur" ni nini?
Unaelewa kwamba mimi kushindwa kuthibitisha hayo uliyoyasema hakuthibitishi Mungu yupo?
Unaelewa kwamba mimi ninaweza kushindwa kuthibitisha hayo yote, kwa sababu Mungu hayupo?
Unaelewa kwamba, katika ulimwengu ambao Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo, watu kushindwa kuthibitisha vitu na kuwa na majibu ya uhakika si kitu cha ajabu, kwa sababu hakuna Mungu wa kuwapa majibu na wao inabidi wachambue mambo na kupata majibu, na hawana uwezo wa kupata majibu yote mara moja.
Kwa hiyo, kushindwa kwangu kuwa na majibu ya maswali, hakuoneshi mgogoro wowote na dhana kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na mapenzi yote hayupo.
Ila, katika ulimwengu ambao Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo, mtu yeyote anatakiwa kuwa na majibu ya swali lolote na ujinga hautakiwi kuwepo.
Kwa sababu, Mungu huyo mwenye neema kuu hawezi kuruhusu viumbe wake watawaliwe na ujinga.
Na ikitokea kuthibitika kwamba kuna ujinga wowote popote, huo ni uthibitisho kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.
Angekuwepo angefuta ujinga wote.
Hoja yako ya kuniuliza maswali ambayo unaona nitashindwa kuyajibu, ambayo wewe unaona inathibitisha Mungu yupo, kiukweli ni hoja inayothibitisha Mungu hayupo.
Unaelewa kwamba umetoa hoja inayozidi kuthibitisha Mungu hayupo?