Kwanini mfalme Zumaridi anasumbuliwa sana na dola? Uhuru wa kidini uko wapi!?

Mfalme Zumaridi ananyanyaswa na kubaguliwa kwa sababu ya imani yake kinyume na katiba inayotoa uhuru wa kila imani na dini zote, aachwe na imani yake kama vile wengine walivyo huru katika kutekeleza imani zao.
Malalamiko yako haya yatakuwa na mashĺiko baada ya mahakama kutoa hukumu itakayoenda kinyume na msimamo wako.
 
Unaandika kama mtu mwenye uelewa na kilichofanywa na Polisi au unaandika kama mwenye negativity na chochote kinachofanywa na Vyombo vya Dola?
 
Jirani yangu amekamatwa ila nimejua kupitia mtandao
 
Kosa lake kuwaambia watoto ye ni mungu hapa anakosea ilitakiwa awasubirie wakue
 
Huyo Zumaridi ni mgonjwa wa akili anayehitaji tiba.
 
Sawa tumekuelewa mungu wako aachiliwe mara moko
 
Kwanini asitulie nyumbani na mume wake na kufanya biashara nyingine za kumuingizia kipato badala ya kuwalaghai watanzania wenye wasio na akili?
Hii ndiyo inamlipa kwa nini atafute ingine?
 
Sasa mungu yupo rockup nani anaendesha shuguli za kimungu za kila siku, ndiyo maana Mungu Jehovah ni Roho tu ,sasa kama angekuwa kama Zumaridi si leo hapo Mwanza ingekuwa ni taharuki
 
Zuma namkubali sana sijui kwa nini.

Mtoto wangu wa kike nitamwita Zumaridi.

Shuleni ataitwa Zumaridi secretarybird.
 
.Naishi jirani yake kabisa,ila sijaona ubaya anaoutangaza.sisi majirani tumeshamzoea.ana umati mkubwa thou na watu wanapona kama kwa mwamposa,nina watu tunaheshiminiana nao ni waumini wake.wamuache tu maana wakifunga kanisa lake au hilo hekalu lake mtaani kunapoa biashara ina lala boda dolo.ila atakua hajui kula na sirikali ndo maana wanamuandama.mimi huyu zuma ni mteja wangu wa maziwa muacheni basi ni mpiga pesa tu wala hana madhara huyu
 
Malalamiko yako haya yatakuwa na mashĺiko baada ya mahakama kutoa hukumu itakayoenda kinyume na msimamo wako.
Mahakama gani? Hiihii ya sisiemu iliyomuachia mwanzo? Kama unategemea matokeo tofauti utakua we mgonjwa jipime
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…