Kwanini Mkuu wa Majeshi(JWTZ)anatokea Kamandi Moja tu, wakati tuna Kamandi Sita?

Mimi naona sahihi kupata mafunzo ya infantry kila mwanajeshi.

Fikiria rubani wa air Force ametua porini na parachute baada ya kutungiliwa au ndege kuleta shida ata survive vipi kwa muda mrefu kabla ya kuokolewa?
Askari wa Navy ata survive vipi porini au kisiwani baada ya kupata ajali au kudhibitiwa na adaui akakimbilia nchi kavu Kama lile tukio la wa Cuba waasi kwenye kisa cha Bay of pigs?
Mimi tuko tofauti kidogo, kila mtu aspecialize kwake mapema kama majeshi ya wenzetu, unakuta mtu kafanya kozi ya infantry, vifaru , na navy lkn mwisho wa siku anatumia ujuzi mmoja tu, jeshi linakua linaingia gharama kubwa kuwafundisha vitu ambavyo hawavitumiaa.. kuhusu ikitokea umetekwa au pilot kuangukia porini, ukishakua mwanajeshi haijalishi ni airforce , navy au landforce lazima uweze kujua kutumia personal weapon , uwe na uwezo wa kutembea some Kms, uwe na uvumilivu wa kusurvive kwenye harsh environment,, haikuhitaji kuwa askari wa miguu kujua haya mambo.
 
Mwamunyange nlikua sijui hii, shukrani sana.
Kutokea kamandi ya JKT hiyo siyo factor ,hakuna kozi utayopiga kwamba uwe kamandi ya JKT,Kamandi mama ni 3 anga ,navy ,nchi kavu ,alafu zinafata hizo zingine kama kamandi ya JKT,kamandi ya jeshi la akiba na kamandi ya vikosi chini ya makao makuu ya jeshi ambapo zamani walikuwaga TAU na sasa wako upanga, mkuu wa kamandi ya vikosi chini ya makao makuu ya jeshi wa kwanza alikuwa anatokea airforce na alikuwa mzenji meja jenerali mstaafu chema Mohamed chema,

Kwaiyo hizo kamandi za ziada itaongozwa na afisa yyte kutoka hizo kamandi mama navy ,land force au airforce

Hizi zingine huwaga wanateuliwa makamanda waliobobea kwenye hizo kamandi japo basic training au knowledge za kamandi zingine Huwa wanazijua ,kwani ukishafika huko juu kuanzia briged kamanda kwenda juu hapo uongozi unakuwa zaidi wa kiutawala na utendaji kivita

mwamunyange alikuwa mkuu wa JKT mwaka 2001 Hadi 2006 lakini basic course zake ni infantry ,ila wew umeuliza why CDF ni nadra ambaye ana taaluma za airforce au navy na mara nyingi wengi ni waliotokea kamandi za nchi kavu....so ndomana hapo mwànzo nikajibu swali lako ni technical ila majibu yake yapo na siyo kwamba ni mlolongo ambao umewekwa ni lazima atokee land force ila ni coincidence tu inatokea ....

Mabeyo ni lando force lakini kabla ya kupanda juu kuwa Chief of staff au CDF alikuwa mkuu wa tawi la usalama na utambuzi ila basic training zake ni za land force , lutein Jenerali shimbo alikuwa mkuu wa JKT kabla ya kuwa Chief of staff lakini alitokea land force hiyo kamandi na siyo navy au anga ......
 
Kuna Luteni Jenerali alishawahi kuwa Mkuu wa Kamandi alikua anaitwa Luteni Jenerali Wyjones Kisamba
Wynjones Mathew kisamba alikuwa mkuu wa kamandi akiwa na cheo cha meja jenerali mwaka 2008-2012 ambapo alivyopanda kuwa luteni jenerali alikuwa huko Sudan kamanda wa vikosi vya UN Sudan Hadi alipostaafu 2014 , Tanzania hatujawai kuwa na mkuu wa kamandi mwenye cheo cha luteni jenerali ,japo tushawai kuwa na 4 star general kiwelu ambaye hakuwa CDF na ndo pekee ambaye alifika cheo cha jenerali bila kuwa CDF na baada ya hapo 95 akateuliwa balozi ufaransa ila walimkataa ...
 
Mfano mwaka 2012 chuo cha NDC kilivyozinduliwa mkuu wake wa kwanza alitokea airforce Charles Lawrence makakala lakini alikuja kupanda cheo na kuwa luteni jenerali lakini sare zake Bado alikuwa anavaa za airforce,ila angeteuliwa kuwa Chief of staff au CDF angebadili sare na kuvaa za land force ambazo ndo kamandi mama ,aliyekuwa Mlinzi wa kikwete kamali kimario baadaye brigedia jenerali yule kamandi yake ni airforce lakini pale alikuwa akivaa barret za land force akiwa nyuma ya raisi,pia brigedia jenerali mkeremi aliyeañza Kwa kikwete 2014 Hadi Kwa magufulini 2018 ni airforce na nilijua baada ya kukutana naye akiwa na cheo cha brigedia jenerali so hapo inamaanisha basic course zake alizobobea kiutendaji vita ni za anga,japo Kwa sasa ni mkuu wa usalama na utambuzi jeshini na sare anavaa za land force
 
Nimesoma uzi huu nimekuja kudundua kuwa watu wengi hawafahamu namna mashirika na taasisi zinazofanya kazi.

Ukitoa mgambo, askari wengine wote mliowazungumzia hapa ni waajiriwa wa Jeshi la wanachi wa Tanzania, kulikana na majukumu au mahitaji ya jeshi wanaweza kupangiwa au kupenda kufanya majukumu mengine yoyote yale ndani ya Jeshi.

Kamandi kwa Kiingereza Command.

Askari wa Navy au JKT anaweza kuamua kuomba au kupangiwa kwenda kutekeleza majukumu mengine kulingana na yeye au jeshi linavotaka.

Kwa hiyo kuwa mkuu wa majeshi kutokea Makao makuu sio significant sana kumaanisha Kamandi zingine hazina humuhimu, Ukuu wa Majeshi ni issue ya kiutawala zaidi so kuna wakati utawala lazima uzingatie exposure na mahitaji ya wakati husika
 
Wynjones Mathew kisamba alikuwa mkuu wa kamandi akiwa na cheo cha meja jenerali mwaka 2008-2012 ambapo alivyopanda kuwa luteni jenerali alikuwa huko Sudan kamanda wa vikosi vya UN Sudan Hadi alipostaafu 2014 , Tanzania hatujawai kuwa na mkuu wa kamandi mwenye cheo cha luteni jenerali ,japo tushawai kuwa na 4 star general kiwelu ambaye hakuwa CDF na ndo pekee ambaye alifika cheo cha jenerali bila kuwa CDF na baada ya hapo 95 akateuliwa balozi ufaransa ila walimkataa ...
Mkuu unantoa tongotongo naona kumbe kuna mapaka 4star General na hakuwa CDF hii inawezekanaje? Ebu nipe madini kidogo.
 
So watu wa Navy hawafanyi kabisa mafunzo ya infantry!?
Basic za infantry wanafanya wakiwa RTS ila baada ya hapo sasa level ,3,2 na kuendelea watapiga kwenye kamandi zao sasa japo Bado watu wanapiga Kwa kuchanganya ,ila kila askari unayemuona infantry lazima abobee hizo zingine ndo zinafata na hii ni kutokana na geography ya nchi husika na nature ya maadui wanaokuzunguka ,japo maboresho kwenye majeshi yte duniani japo kuwafanya wanajeshi wajue basic za anga au navy ili ukiwa uwanja wa medani usitoe macho
 
Mkuu unantoa tongotongo naona kumbe kuna mapaka 4star General na hakuwa CDF hii inawezekanaje? Ebu nipe madini kidogo.
Kaka nadhani game ya Simba ikiisha ntakuja kukufafanulia Kwa kina ,ila Kwa kifupi kuwa CDF haimaanishi lazima uwe 4star general ,Kuna nchi zingine CDF ama. Cheo cha luteni jenerali au meja jenerali ,hii inatokana na ukuaji wa jeshi husika hasa idadi ya askari

Tanzania mkuu wetu wa majeshi wa kwanza alikuwa na cheo cha brigedia jenerali wakati anaapishwa na kutumikia madaraka yKe Hadi anastaafu alikuwa meja jenerali,aliyefata twalipo alikuwa CDF na cheo cha luteni jenerali 3 star general,ila baada ya hapo waliofata wte walikuwa 4star general kwani jeshi lilijitosheleza kiidadi ya askari na mengine katika kuwa na jenerali full..

Mwaka 2002 sarakikya alipandishwa cheo kuwa 4 star general Kwa heshima yeye alikuwa ndo wa kwanza ,kumbuka kijeshi cheo kupanda au kushuka inaweza tokea ukiwa umekufa au umestaafu

Kisiwa cha Comoro mwaka 2007 mkuu wake wa majeshi alikuwa na cheo cha kanali,

Gambia wakati yahya jamej anapinduliwa mkuu wake wa majeshi alikuwa na cheo cha luteni jenerali

Marekani wakuu wa kamandi kwao ni 4 star general na pia marekani ina 4 star general 42 na ndo idadi yao inasema wAsizidi hapo ila pia ikiwa pungufu ni sawa , so haya yanatokana na ukubwa wa jeshi linavyozidi kustawi na mengineyo

Nimejibu haraka kwakuwa nataka niwai mpira na siti nzuri
 
Ntakuja kutoa majibu ngoja nitulie niulize senior officer kadhaa nipate mlingano wa majibu yao,umeuliza swali zuri sana na ambalo ni technical na siyo officer yyte anaweza kujibu mpaka awe ameenda command and staff college au national defense college ndo ataweza kujibu hili kwani Kuna vigezo vya unadhimu Huwa wanajua , ila Kwa haraka haraka Gen. Sarakikya & Gen mboma Kwa haraka ndo CDF pekee walikuwa airforce au walipiga "trade" za airforce
Hivi na huko majeshini mpo wenye kupenda masifa ya kisomo kama kule kwa kina Rweyemamu . Maana nimeona unavyojinasibu na hizo University zenu.

Anyway my mind count that, lack of security consciousness for some individuals like you is a very big challenge.
Imagine a layman like me I'm egger to know much of what you have disclosed.

I think one day you will comment and tell the strategies of your organisation before its maturity
 
Basic za infantry wanafanya wakiwa RTS ila baada ya hapo sasa level ,3,2 na kuendelea watapiga kwenye kamandi zao sasa japo Bado watu wanapiga Kwa kuchanganya ,ila kila askari unayemuona infantry lazima abobee hizo zingine ndo zinafata na hii ni kutokana na geography ya nchi husika na nature ya maadui wanaokuzunguka ,japo maboresho kwenye majeshi yte duniani japo kuwafanya wanajeshi wajue basic za anga au navy ili ukiwa uwanja wa medani usitoe macho
Hapo kwenye kuchanganya hapo, inawezekana mtu wa kikosi cha mizinga (Black Barret) akafanya level 3 ya JKT alafu akarudi kikosini kwake?
 
Kaka nadhani game ya Simba ikiisha ntakuja kukufafanulia Kwa kina ,ila Kwa kifupi kuwa CDF haimaanishi lazima uwe 4star general ,Kuna nchi zingine CDF ama. Cheo cha luteni jenerali au meja jenerali ,hii inatokana na ukuaji wa jeshi husika hasa idadi ya askari

Tanzania mkuu wetu wa majeshi wa kwanza alikuwa na cheo cha brigedia jenerali wakati anaapishwa na kutumikia madaraka yKe Hadi anastaafu alikuwa meja jenerali,aliyefata twalipo alikuwa CDF na cheo cha luteni jenerali 3 star general,ila baada ya hapo waliofata wte walikuwa 4star general kwani jeshi lilijitosheleza kiidadi ya askari na mengine katika kuwa na jenerali full..

Mwaka 2002 sarakikya alipandishwa cheo kuwa 4 star general Kwa heshima yeye alikuwa ndo wa kwanza ,kumbuka kijeshi cheo kupanda au kushuka inaweza tokea ukiwa umekufa au umestaafu

Kisiwa cha Comoro mwaka 2007 mkuu wake wa majeshi alikuwa na cheo cha kanali,

Gambia wakati yahya jamej anapinduliwa mkuu wake wa majeshi alikuwa na cheo cha luteni jenerali

Marekani wakuu wa kamandi kwao ni 4 star general na pia marekani ina 4 star general 42 na ndo idadi yao inasema wAsizidi hapo ila pia ikiwa pungufu ni sawa , so haya yanatokana na ukubwa wa jeshi linavyozidi kustawi na mengineyo

Nimejibu haraka kwakuwa nataka niwai mpira na siti nzuri
Sawa sawa Mkuu
 
Hivi na huko majeshini mpo wenye kupenda masifa ya kisomo kama kule kwa kina Rweyemamu . Maana nimeona unavyojinasibu na hizo University zenu.

Anyway my mind count that, lack of security consciousness for some individuals like you is a very big challenge.
Imagine a layman like me I'm egger to know much of what you have disclosed.

I think one day you will comment and tell the strategies of your organisation before its maturity
Usiwe mpumbavu hizi siyo Siri ni basic knowledge ambazo hata mtu mwenye passion anazijua ,jifunze kutafuta maarifa na usiwe mjinga wa kushindwa kutofautisha basic knowledge kama hizi
 
Hivi na huko majeshini mpo wenye kupenda masifa ya kisomo kama kule kwa kina Rweyemamu . Maana nimeona unavyojinasibu na hizo University zenu.

Anyway my mind count that, lack of security consciousness for some individuals like you is a very big challenge.
Imagine a layman like me I'm egger to know much of what you have disclosed.

I think one day you will comment and tell the strategies of your organisation before its maturity
Mbona hayo mambo ni ya kawaida sana ambayo ata ukitulia unayapata mtandaoni tu. Hakuna kitu cha ajabu alichosema hapo.
 
Back
Top Bottom