Hii ni dhambi gani unaweza kufafanua ? Na Je Shetani alitenda hii dhambi au ni kiburi chake yaani msamaha upo ila hautaki ?
Kwahio ni kwamba kama vile watu wanakuwa brainwashed kuridha na chochote kile..., Yaani kama enzi za utumwa ambapo kuna watu walikuwa wanafurahia sana kuwatumikia Ma-Bwana zao yaani hata ukiwapa uhuru wanaona wanapungukiwa ?
Je unaona hilo ni sahihi yaani kuridhika hata kama kuna kunyonywa sio kwa utashi wako bali kwa kuondolewa utashi ?!!!
Shirki (ushirikina) ni miongoni mwa madhambi makubwa! Na ni dhambi kubwa kuliko madhambi yote unayoyajua wewe.Kuiba,kuua,kuzini,kusema uongo,kusengenya n.k hakufikii ukubwa wa hii dhambi.
Shirki (Ushirikina) ni kitendo cha kumuwekea Mungu washirika katika masuala yote ya Ibada.
Mfano ukiamini kuwa kuna kitu,mtu au jini anaweza kukupa wewe riziki kama/Pamoja au zaidi ya Mungu. Hapa unakuwa umemuwekea Mungu mshirika. Mfano unaumwa au una matatizo ila ukaenda kumuomba babu yako aliyezikwa miaka mingi iliyopita kaburini akusaidie kukuponya au kukutatulia matatizo yako ,hapa unakuwa umemfanya babu yako kuwa nae ni Mungu pamoja na Mungu.Hivyo umemfanyia Mungu kuwa ana mshirika.
Au ukaitakidi kuwa mizimu au miti (mibuyu) ukienda kuiomba ina uwezo wa kukutatulia matatizo yako hapa unakuwa umefanya ushirikina.
Au unamatatizo ukaensa kwa mganga akupigie ramli na kuwaomba majini wakusaidie kukutatulia matatizo yako ya biashara,kupata mali au watoto....hapa unakuwa umefanya shirki. Unakuwa ni Mshirikina.
Au nafsini kwako ukiwa na itikadi kuwa kuna Mungu zaidi ya mmoja kama walivyo wahindi na mabudha.Huo unakuwa ni ushirikina.
Ina maana kuwa umeshajitoa katika imani ya Mungu mmoja apasae kuabudiwa peke yake.
Mfano mzuri ni pale Unapokuwa na biashara kisha ukamuajiri mtu akuuzie bidhaa zako...yule mtu akauza vizuri kisha pesa yako yote akaichukua na kwenda kumpa mtu mwingine ambaye huna share nae katika umiliki wa biashara yako.Na ukimuuliza why kafanya hivyo ,anakujibu kuwa hakuna ubaya kumpa mtu mwingine pesa yako kwani ww na yule wote ni sawa!...
Je unaona ubaya wa hii kitu?? Ni wazi kuwa utachukizwa na jambo hilo na ikiwezekana unaweza hata kumuadhibu huyo mfanyakazi wako kwa tendo alilolifanya.
Hii ndio SHIRKI (ushirikina)
Ni mada pana sana.Ushirikina una matawi yake mengi tu. Ila kiufupi huo ndio uhalisia wa dhambi ya SHIRKI.
Iwapo mtu atakufa akiwa na dhambi hii pasi na kutubia kwa mola wake ajue kuwa MUNGU haisamehi kamwe na amemuharamishia pepo mtu ambae atakufa hali ya kuwa ni mshirikina.