Umewahi kuona kinachotoka kwenye mwili wa mwanadamu mpaka tunaamua kusema amekufa na hivyo tunaenda kuzika?
Nyinyi wa dunia ya tatu, mkifa mnapelekwa kufukiwa na mnasema na mnaingiza imani zenu kama sababu yakufa....
Dunia ya kwanza, ukifa, ni kisheria uthibitishwe umekufaje kisayansi...hata kama ni melala nyumbani kwako, hamuendi kuzika mpaka wajue huyo mtu amekufa kwa sababu gani...
Na sayansi haidanganyi.....
Unakula mifuta imeziba matundu ya moyo, umepata shinikizo la damu au stroke usiku umelala, pia wanafanya autopsy/post mortem kuhakikisha hivyo, imetoka hiyo...
Au....
Umepata ajali na kupoteza damu nyingi au organ kama moyo, mapafu au ubongo umevurugwa, wanafanya autopsy/post mortem kuhakikisha hivyo imetoka hiyo...
Mtu anapata Arrythmia ya moyo na anakuwa katika hali ya nusu kufa na kama hamna namna ya kumukoa, ni anakufa tu baada ya muda mchache, lakini kwenye huduma bora, unarudishwa kuendelea na joto ya jiwe, mpaka kuna watu wanaweka signature inaitwa DO NOT RESUSCITATE ya kuwa akifikia hiyo hali asirudishwe duniani kuendelea na msoto...
Na ukisikia amekufa kwa natural causes, pia kuna sababu ya moyo umesimama kupiga, ubongo umeumaliza mwendo....yaani kila kufa kuna sababu yake kisayansi zaidi kuliko hizi stori za kiroho....