Kwanini Mungu na Shetani wasimalize tofauti zao?

Ngoja na wewe nikupe hili swali ili ufahamu uwepo wa reality beyond the five senses.

Bila kutumia matamshi au maandishi unaweza kuniambia mawazo yanaexist or not? Kama yanaexist, can you measure and present them in their own form
 
Shiriki hapa.

Bila kutumia matamshi au maandishi unaweza kuniambia mawazo yanaexist or not? Kama yanaexist, can you measure and present them in their own form
 
Ushahidi ni uwepo wa uhai katika mwili wako na wangu. Ile life force ndani yetu inatuhakikishia ndani yetu beyond the tangible world uwepo wa maisha beyond ulimwengu huu. Ila specifics zake ndio tunazipata katika biblia.
Kwanini uwepo wa uhai wangu na wako uwe ni uthibitisho wa kitu hicho?

Kwanini unatumia mfano wa jambo ambalo lipo kihalisia (mimi na wewe) linalothibitishika kama jaribio la kutaka kuthibitisha kitu kingine (mwili wa pili) ambacho huwezi kukithibitisha chenyewe kama chenyewe?
 
Umewahi kuona kinachotoka kwenye mwili wa mwanadamu mpaka tunaamua kusema amekufa na hivyo tunaenda kuzika?
 
Hapana, ndani ya biblia huwezi kukuta kitu chochote kinachopingana na scientific discoveries tofauti na kwenye quran.
Nenda kosome Genisis 1:9 ambapo dunia inaelezwa iliumbwa siku ya 3

Kisayansi hiyo imekaaje?

Ikiwa siku hitegemea na rotation ya dunia, tuambie unawezaje kuwa na usiku na mchana pasipo kuwa na dunia?
 
Umewahi kuona kinachotoka kwenye mwili wa mwanadamu mpaka tunaamua kusema amekufa na hivyo tunaenda kuzika?
Kinachotokea baada ya nini?

Kwa hiyo kama hatuoni hiyo ndio nafasi ya ku penetrate habari za uongo zisizopitia uthibitisho?
 
Ndio aliiweka kwasababu ni mazingira pure

Hapa ndio unatakiwa kuelewa maana ya kuzaliwa mara ya pili. Unakuwa na same spirit kama Yesu hivyo huwezi tena kuasi kwasababu utakuwa na asili ya kiungu.
Acha ujinga wewe tafuta hela.Hizo hadithi tu usikomaze shingo kufafanua ujinga
 
Ngoja na wewe nikupe hili swali ili ufahamu uwepo wa reality beyond the five senses.

Bila kutumia matamshi au maandishi unaweza kuniambia mawazo yanaexist or not? Kama yanaexist, can you measure and present them in their own form
Yana exist na yana pimika vile vile

Ubongo unaofikiria upo tofauti na ubongo ambao umelala

Unafahamu kitu kinaitwa temography scan?

Sasa kupitia hicho kifaa unaweza kupima ukajua ubongo huu una mawazo na ubongo huu hauna
 
Nenda kosome Genisis 1:9 ambapo dunia inaelezwa iliumbwa siku ya 3
Soma vizuri biblia. Mbingu na nchi ziliumbwa kwenye Mwanzo 1:1. Kutoka mstari huo wa kwanza mpaka mstari wa pili ilipita miaka zaidi ya bilioni 4.5 ndipo tukio la nchi kuwa ukiwa tena utupu likatokea.
Kisayansi hiyo imekaaje?

Ikiwa siku hitegemea na rotation ya dunia, tuambie unawezaje kuwa na usiku na mchana pasipo kuwa na dunia?
Biblia inasema the evening and the morning were the dashdash day. Swali lako hapa linaashiria haujasafiri sana. Kuwa jioni au asubuhi sio sawasawa na kuwa na giza na mwanga. Niliwahi kusafiri kwenda nchi za northern hemisphere nikashangaa usiku bado jua linawaka na mchana kuna giza.
 
Kinachotokea baada ya nini?

Kwa hiyo kama hatuoni hiyo ndio nafasi ya ku penetrate habari za uongo zisizopitia uthibitisho?
What is it that left the body for it to be dead? Biblia inatujibu kwamba ni nafsi na roho ambazo huwezi kuziona lakini zipo. Hizo ndio life force ndani yako. Ndio inayotengeneza electrical signals zinazoufanya moyo udunde.
 
Yana exist na yana pimika vile vile

Ubongo unaofikiria upo tofauti na ubongo ambao umelala

Unafahamu kitu kinaitwa temography scan?

Sasa kupitia hicho kifaa unaweza kupima ukajua ubongo huu una mawazo na ubongo huu hauna
Hicho kipimo kinapima dalili za uwepo wa mawazo na sio mawazo yenyewe.
 
Ibilisi mara baada ya kuasi amri ya Mungu .Aligoma kumsujudia Adam ,kumpa heshima yake kuwa ana elimu kumzidi yeye. Akasema kuwa yeye ni bora kuliko Adam kwakuwa ameumbwa kwa moto na Adam ameumbwa kwa udongo.

Hakuomba msamaha badala yake alikuwa na ombi lake tofauti, Alimuomba Mungu amjaalie umri ulio mrefu, apate kuishi mpaka mwisho wa ulimwengu huu. Mungu alimkubalia ombi lake na akawa ni miongoni mwa waliopewa uhai mrefu. Hili ndilo ombi lake na alifanya hivyo ikiwa ni kiburi,chuki na husda dhidi ya Adam na uzao wake. Alijua akipewa umri mrefu basi atahakikisha anaingia motoni pamoja na uzao wote wa Adam.

Suala la kuomba msamaha halipo ndani ya nafsi ya ibilisi na halitakuwepo mpaka dunia hii inatamatika
 
Kwa mujibu wa imani ya dini ya Kiislam. Mungu anasamehe madhambi yote iwapo kiumbe (mwanadamu au jini) atatubia dhambi zake kabla ya kufa kwake ila akabainisha kuwa dhambi pekee ambayo hawezi kuisamehe mara baada ya kiumbe kufa ni dhambi ya SHIRKI (kumshirikisha MUNGU) katika ibada. Dhambi ya kumfanya Mungu kuwa ana washirika katika ibada zake huwa haina msamaha mara baada ya kiumbe kufa ila ikiwa kiumbe kitatubu dhambi hii ingali hakijafa basi MUNGU anasamehe.

In hereafter (akhera) , kabla ya kuingia katika paradiso watu wote watatakaswa kutokana na marafhi yote ya nyoyo, chuki,husda,visasi,n.k vitaondolewa katika vifua na watu watakuwa safi kabisa. Kila mtu ataridhika na atakachopewa huko licha ya kuwa watu watazidiana madaraja.
 
Umewahi kuona kinachotoka kwenye mwili wa mwanadamu mpaka tunaamua kusema amekufa na hivyo tunaenda kuzika?
Nyinyi wa dunia ya tatu, mkifa mnapelekwa kufukiwa na mnasema na mnaingiza imani zenu kama sababu yakufa....

Dunia ya kwanza, ukifa, ni kisheria uthibitishwe umekufaje kisayansi...hata kama ni melala nyumbani kwako, hamuendi kuzika mpaka wajue huyo mtu amekufa kwa sababu gani...
Na sayansi haidanganyi.....
Unakula mifuta imeziba matundu ya moyo, umepata shinikizo la damu au stroke usiku umelala, pia wanafanya autopsy/post mortem kuhakikisha hivyo, imetoka hiyo...
Au....
Umepata ajali na kupoteza damu nyingi au organ kama moyo, mapafu au ubongo umevurugwa, wanafanya autopsy/post mortem kuhakikisha hivyo imetoka hiyo...

Mtu anapata Arrythmia ya moyo na anakuwa katika hali ya nusu kufa na kama hamna namna ya kumukoa, ni anakufa tu baada ya muda mchache, lakini kwenye huduma bora, unarudishwa kuendelea na joto ya jiwe, mpaka kuna watu wanaweka signature inaitwa DO NOT RESUSCITATE ya kuwa akifikia hiyo hali asirudishwe duniani kuendelea na msoto...

Na ukisikia amekufa kwa natural causes, pia kuna sababu ya moyo umesimama kupiga, ubongo umeumaliza mwendo....yaani kila kufa kuna sababu yake kisayansi zaidi kuliko hizi stori za kiroho....
 
Hawawezi kumaliza tofauti zao, kwa sababu hawapo kiuhalisia, ni wahusika wa hadithi ya kutungwa tu.

Kwa hivyo, kama unataka wamalize tofauti zao kama wahusika wa hadithi ya kutungwa, ni suala la kuandika hadithi ambayo Mungu na Sjetani wanapatana tu.

Hata wewe unaweza kuandika hiyo hadithi.
 
Nadhani watu wa wakati ule walikuwa na imani kupitiliza kiasi kwamba hata mungu alikuwa akijiamini kuwa myu fulani hawezi ingia ktk mtego wa shetani.

Embu linganisha na dunia ya sasa nani avumilie hayo mambo? Jambo dogo tu mtu ashaenda kwa mganga kuuliza /aangaliziwe nini kinaendelea😅
 
Mtume Muhammadi keshamaliza huo uhasama.

Kwa kufanikiwa kumsilimisha Shetani na kwa sasa Shetani ni Muislamu safi kabisa.

Kwa sasa Allah na Shetani ni marafiki wa kupika na kupakua.
Na wote kwa pamoja wanamswalia mtume na kumtakia rehema.

Kumbukeni Allah aliumba Mtu, Majini na Ibirisi Shetani na viumbe vyote ili vimuabudu.

Tunamshukuru sana m'bora wa mitume kwa kufanikisha hili swala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…