Kwanini Mungu na Shetani wasimalize tofauti zao?

Kwanini Mungu na Shetani wasimalize tofauti zao?

Sijui kama ujuvi wangu au ninavyodhani najua mimi ndio unavyojua wewe...

Ndio maana nikasema kwa kutumia logic na consistency nielezee maswali yangu hapo juu, Sababu ni Imani hapa sipo kusema hili ni sahihi au sio sahihi bali hili halipo consistent na halina logic (yaani the argument does not hold water)
Does not hold water,means it is so dry.
 
Huna excuse....Jua kuwa tupo hapa duniani kwa ajili ya mtihani.

Maisha yetu yapo katika mfumo huu!!

Mungu kwa hekima,utashi na mapenzi yale aliamua kutuumba ili atufanyie mtihani! Viumbe vyote vilihudhurishwa mbele yake, akauliza nani yupo tayari kufanyiwa huu mtihani wa kupewa amana!! ?

Jua,milima,wanyama,bahari,malaika,mwezi,mbingu,nyota,miti na ardhi vyote vilikataa kuibeba hiyo amana badala yake mwanadamu alikubali kubeba hiyo amana.

Amana yenyewe ni hii kuwa atafanya aliyoamrishwa na ataacha aliyokatazwa kwa maana ya kuwa mtiifu. Viumbe wengine waliogopa kubeba kutokana na uzito wa suala hili ila mwanadamu ali underestimate uzito wa jambo hili akabeba majukumu. Ila aliambiwa kuwa akifaulu kutekeleza hayo atalipwa malipo makubwa ambayo ni Pepo na akishindwa basi ataadhibiwa kwa moto.

Viumbe vingine vilistaajabu kuona kiumbe dhaifu kama binadamu kukubali kubeba mzigo mzito.

Mwandamu yeye alichagua hiyari hivyo viumbe vingine havina hiyari ya kutenda kama mwanadamu.

Nafsi inapoletwa duniani huwa ineletwa kwa ajili ya mtihani hivyo ili kuwe na fair test kila nafsi huanza ikiwa haina kitu kichwani!! Ila humu duniani Mungu tayari ameshatanguliza kuweka uongofu kupitia vitabu vyake vitukufu,mitume na manabii (wa kweli).

Hivyo ni jukumu lako mwanadamu kuutafuta ukweli kama vile unavyohangaika kila siku kuutafuta mkate wako.

Mtihani huu una muda maalumu kwa kila mtahiniwa kuna ambao wamepewa muda mrefu na wengine mfupi. Mtoto toka anapozaliwa mpk kufikia baleghe huwa hana dhambi! Ila kalamu inaanza kuandika mema na mabaya yake mara baada tu ya kuwa ameshabaleghe kwa maana sasa anaelewa lipi jema na lipi ovu.
Kwahiyo mkuu unataka kusema Mungu alikua anafanya probability juu ya nani atatii na nani hatotii. Kama vile unataka kusema Mungu alikua hajui maamuzi ambayo viumbe watayachukua hata kabla ya dakika moja
Ninadhani ungesema Mungu alionesha hekima au demokrasia kupitia viumbe wake lakini sio kwamba eti hakujua nikiumbe gani kingebeba hiyo dhamana
Suala la imani litabakia kua tete.
 
Mwanadamu hakufanya dhambi akiwa kwenye spirit realm bali alikuwa katika mwili hivyo chance anapewa.

Ukiwa kwenye spirit realm unakuwa na freewill ndio maana shetani aliasi. Sisi wanadamu kwa wale watakaokuwa ndani ya Kristo Yesu wao hawataweza kuasi kwasababu watakuwa na asili ya kiungu. Kumwasi Mungu itakuwa sawasawa na kujiasi mwenyewe kitu ambacho hakiwezekani.
Kwahiyo kila binadamu anaenda kuwa Mungu kwa mujibu wa maelezo yako haya?
 
Hili suala tulijadili kwa Logic!

Iwapo tunaambiwa kusamehe mara sabini mara saba, inakuwaje hawa wasimalize tofauti zao sababu naona hivi vita vyao sisi nyasi tunaumia.

Okay unaweza kusema kwamba Shetani hajarepent (kuomba msamaha) ndio maana hajapewa msamaha, lakini je inamaanisha Mungu anapenda kuombwa ombwa na kunyenyekewa kiasi kwamba hatoi msamaha mpaka aombwe.

Na je, Hadithi za Mwana Mpotevu, Je inamaanisha siku Shetani akirudi na kupiga magoti atasamehewa ? Au kuna Muda wa kuomba msamaha ukipita ndio basi.

Au baada ya kukaa Motoni kwa karne kadhaa huenda ukapita msamaha kama wa wafungwa na kila mtu akawa huru na sio hawa tu ambao walijinyima bata huku duniani?

NB: Kama kuna anayeweza kunielewesha haya logically kwa kanuni za imani yake naomba tujadili (na sio kutumia kanuni za multiplication kwenye paraghraph moja na ya Pili kutumia kanuni za Addition) yaani inconsistency!
Mama D, Njoo huku
 
Kuna hoja zenye mashiko kwa pande zote ila ukitulia unaweza kupata ukweli kupitia majibizano ya hoja hizi.
 
Msamaha unatolewa pale ambapo mkosaji atakiri kuwa alikosea,na kujutia kosa alilolifanya,infact ibilisi hajawahi kujutia kosa alilolifanya la kujilinganisha na Muumba wake hivyo hastahili msamaha
Additionally, Ibilisi anabuni deile mbinu na mikakati ya kuongeza wafuasi wake na pia dhambi juu ya dhambi. That's never a spirit of repentance.

Bila shaka hapo awali alipewa muda wa rehema ili kuomba msamaha na kutubu. But somehow, alidhani yuko way smarter kuliko Muumbaji wake. Grace has time limit. This privilege will not always be within the reach of a sinner.

Kuupata msamaha kutoka kwa Mungu hutegemea attitude ya mkosaji mwenyewe. Akishupaza shingo, ndiyo basi tena. Akinyenyekea na kujishusha, anakubaliwa tena. It's not that God cannot (or doesn't want to) grant him forgiveness; it's Satan who cannot receive it.

Satan has forfeited that privilege forever. Even if it were possible to grant him ^unconditional forgiveness,^ it wouldn't serve him any good--he wouldn't enjoy it--because his nature has been so identified with evil so much so that sin and wickedness are now his very second nature.

He has undergone what we may call permanent disorientation of his own nature. Forgiveness has something to do with the sinner's heart in the first place. It's not just an external, formal pronouncement such the one we normally hear in the premises of justice: ^This court declares the defendant NOT GUILTY!^

Let's not forget. Shetani alipoasi, alisababisha ^system disorder^ ulimwenguni kote. I mean, harufu ya dhambi aliyoileta duniani haiwezi kuondolewa tu hivihivi. Lazima ing'olewa ^mizizi, shina, na matawi^ yake yote.

Na, most importantly, ung'olewaji au utokomezaji huo unafanyika katika namna ambayo daima itamwonesha Mungu kwamba ni mwenye haki na upendo.

The ultimate goal now is to eventually eradicate sin completely never ever to resurface again.
 
Freewill kusema binadamu ana uhuru wa kuchagua kufanya jambo lolote bado naiona ina ukakasi.

Katika utawala wa Mungu mjuzi wa yote, aliyejua kila kitu kabla hata hakijatokea, na katika kujua kwake hakutoi chance ya kitu kwenda vinginevyo basi dhana ya free will inabaki kuwa paradox

Katika jicho la kiutu, tunaweza feel some freedon kwenye choices zetu lakini uhalisia ni kwamba tuna experiece illusion

Kwasababu freewill inatakiwa iwe na options nyingi zinazowezekana, sasa Mungu kama aliona leo waziri wa uingereza atajiuzulu maana yake hiyo ishakuwa fixed hakuna option nyingine
Foreknowledge (knowing a future event beforehand) is not the same as predestination (to predetermine, fix, decide, decree).
 
Mfano eako nashindwa kuuelewa labda pengine kwasababu siko familiar na mambo ya tech

Ila nachoweza kusema kupitia hoja ya Mungu kujua ni kuwa

Ili mtu awe na uhuru wa kuchagua basi swala la kuchagua, Mungu hapaswi kujua nini naenda kuchagua

Mungu kujua nini naend kuchagua na kujua kwake ni lazima kutokee hivyo hivyo basi hiyo ni fate mtu ameamuliwa aje apite njia hiyo

Though katika fikra zetu tunaweza hisi tuna experience uhuru lakini kiuhalisia hatukuea na namna nyingine ya kwenda vinginevyo

Kwa mfano, watabiri wa hali ya hewa wanapotuambia kuhusu hali ya anga itakavyokuwa baadaye kabla ya muda huo kuwadia, hivi wao ndio wanaratibu na kuamuru hali iwe hivyo?

Ni kwamba wana ^uwezo^ fulani wa kuona mapema jinsi hali ya hewa itakavyokuwa.

Mungu pia ana UWEZO wa kuuona mwisho tangu mwanzo.
 
Trilion of choices is just an illusion kwasababu outcome yake ishajulikana kabla hujachagua

Unacho ki experience hapo ni illusion tu kuona una machaguo mengi lakini kiukweli haukuweza kwenda kinyume na kile alichokiona umekifanya kabla

Kwasababu tayari kilishakuwa fixed
Sijawahi kuelewa kwa nini undhani kwamba ili jambo liwe na sifa ya kuwa free choice, basi ni lazima LISIFAHAMIKE kabla kwamba litatokea baadaye? Hii ni logic ya wapi?
 
Foreknowledge (knowing a future event before hand) is not the same as predestination (to predetermine, fix, decide, decree).
Hicho ndio nacho kimaanisha

Kwamba kama kuna being ambaye anajua kila kitu kitachoenda kutokea future, basi hakuna mtu ambaye anaweza ku control chochote kwenye hiyo future.

Hii theological inaweza ikamuacha dilema mtu yeyote anayedhani ni sahihi kuwa na dhana zote mbili kwa wakati mmoja

1. Mungu mjuzi wa yote anayejua yajayo

2. Na kiumbe mwenye uhuru wa kuchagua
 
Kwa mfano, watabiri wa hali ya hewa wanapotuambia kuhusu hali ya anga itakavyokuwa baadaye kabla ya muda huo kuwadia, hivi wao ndio wanaratibu na kuamuru hali iwe hivyo?

Ni kwamba wana ^uwezo^ fulani wa kuona mapema jinsi hali ya hewa itakavyokuwa.

Mungu pia ana UWEZO wa kuuona mwisho tangu mwanzo.
Utabiri wa hali ya hewa huja kwa vipimo na sio bahati nasibu

Uwezo wa Mungu kuona mwisho kabla mimi sijaufikia una violate uhuru wangu

Mungu akishaona kesho nitaiba, hiyo ni fate ambayo ishakuwa fixed na siwezi kwenda otherwise
 
Sijawahi kuelewa kwa nini undhani kwamba ili jambo liwe na sifa ya kuwa free choice, basi ni lazima LISIFAHAMIKE kabla kwamba litatokea baadaye? Hii ni logic ya wapi?
Unaweza kupata free will kwenye jambo ambalo liko fixed halikupi option zaidi?
 
Mimi nadhani kuna kitu hakipo sawa kwenye hizi habari za Mungu na shetani.

Kwanza kabisa, iliwezekana vipi kwa shetani (malaika) kumsaliti Mungu? Ni kipi hasa kilichomsukuma shetani kumsaliti Mungu?

Pili, tunaambiwa THELUTHI MOJA ya malaika mbinguni walimuunga shetani mkono!! Yaani katika kila malaika 10, zaidi ya malaika watatu walikua upande wa shetani! Ni kipi hasa ambacho malaika walikerwa na utawala wa Mungu kiasi cha kufikia theluthi yao kuunga mkono upinzani?

Tatu, tunaambiwa shetani alikua na JESHI na kwamba jeshi hilo lilienda vitani kupigana na jeshi la malaika!

a) Ina maana wakati shetani ana organize jeshi lake, wanafanya mazoezi, wananunua silaha za maangamizi, wana plan attacks nk Mungu yeye alikua amekaa tu anawaangalia? Si yeye anaona kila kitu?

b) Vita kati ya malaika wa Mungu na wa shetani ilipiganwa vipi? Wakati hao wote ni roho na tunajua roho haziumii wala hazifi? Silaha gani zilitumika? Ushindi ulipatikanaje?

Nne, tunaambiwa katika vita hiyo, shetani na jeshi lake walichakazwa vibaya sana na kutupwa duniani. Lakini hata hivyo, shetani na Mungu waliendelea kushirikiana katika "projects" mbalimbali, huku wakikutana mara kwa mara kupiga soga, kupanga majaribu nk.

Huku tena tunaambiwa shetani alipotupwa duniani, akaja kuanza kukimbizana na mwanamke gani sijui.. mara mwanamke akapewa mabawa ili shetani asimkamate!! Yaani shetani huyuhuyu ambae ametoka kupigana na Mungu, eti akashindwa kumkamata yule mwanamke 😆😆 seriously?

Kuna baadhi ya vitu ukisoma kwenye hivi vitabu yani unaona kabisa ni alfu lela ulela.

Kwahiyo mkuu unataka kusema Mungu alikua anafanya probability juu ya nani atatii na nani hatotii. Kama vile unataka kusema Mungu alikua hajui maamuzi ambayo viumbe watayachukua hata kabla ya dakika moja
Ninadhani ungesema Mungu alionesha hekima au demokrasia kupitia viumbe wake lakini sio kwamba eti hakujua nikiumbe gani kingebeba hiyo dhamana
Suala la imani litabakia kua tete.
 
Unaweza kupata free will kwenye jambo ambalo liko fixed halikupi option zaidi?

Kujua kwamba kitu fulani kitatokea baadaye, haimaanishi kwamba umeamua au umeamuru kitu hicho kiwe hivyo. Hivyo ni vipengele viwili tofauti kabisa--independent variables.

Tulia na kutafakari, utaelewa.

Utabiri wa hali ya hewa huja kwa vipimo na sio bahati nasibu

Uwezo wa Mungu kuona mwisho kabla mimi sijaufikia una violate uhuru wangu

Mungu akishaona kesho nitaiba, hiyo ni fate ambayo ishakuwa fixed na siwezi kwenda otherwise
I believe you do not know what you're talking about.

Hicho ndio nacho kimaanisha

Kwamba kama kuna being ambaye anajua kila kitu kitachoenda kutokea future, basi hakuna mtu ambaye anaweza ku control chochote kwenye hiyo future.

Hii theological inaweza ikamuacha dilema mtu yeyote anayedhani ni sahihi kuwa na dhana zote mbili kwa wakati mmoja

1. Mungu mjuzi wa yote anayejua yajayo

2. Na kiumbe mwenye uhuru wa kuchagua
 
Ndiyo maana kuna umuhimu mkubwa sana wa kuisoma Biblia na kuielewa vizuri. Maswali yako yote (na zaidi) yanajibiwa humo.

Nimecheka sana ulivyosema kwamba Shetani na jeshi lake walikuwa ^wananunua silaha za maangamizi^! (Russia au Marekani?)🙂

Mimi nadhani kuna kitu hakipo sawa kwenye hizi habari za Mungu na shetani.

Kwanza kabisa, iliwezekana vipi kwa shetani (malaika) kumsaliti Mungu? Ni kipi hasa kilichomsukuma shetani kumsaliti Mungu?

Pili, tunaambiwa THELUTHI MOJA ya malaika mbinguni walimuunga shetani mkono!! Yaani katika kila malaika 10, zaidi ya malaika watatu walikua upande wa shetani! Ni kipi hasa ambacho malaika walikerwa na utawala wa Mungu kiasi cha kufikia theluthi yao kuunga mkono upinzani?

Tatu, tunaambiwa shetani alikua na JESHI na kwamba jeshi hilo lilienda vitani kupigana na jeshi la malaika!

a) Ina maana wakati shetani ana organize jeshi lake, wanafanya mazoezi, wananunua silaha za maangamizi, wana plan attacks nk Mungu yeye alikua amekaa tu anawaangalia? Si yeye anaona kila kitu?

b) Vita kati ya malaika wa Mungu na wa shetani ilipiganwa vipi? Wakati hao wote ni roho na tunajua roho haziumii wala hazifi? Silaha gani zilitumika? Ushindi ulipatikanaje?

Nne, tunaambiwa katika vita hiyo, shetani na jeshi lake walichakazwa vibaya sana na kutupwa duniani. Lakini hata hivyo, shetani na Mungu waliendelea kushirikiana katika "projects" mbalimbali, huku wakikutana mara kwa mara kupiga soga, kupanga majaribu nk.

Huku tena tunaambiwa shetani alipotupwa duniani, akaja kuanza kukimbizana na mwanamke gani sijui.. mara mwanamke akapewa mabawa ili shetani asimkamate!! Yaani shetani huyuhuyu ambae ametoka kupigana na Mungu, eti akashindwa kumkamata yule mwanamke 😆😆 seriously?

Kuna baadhi ya vitu ukisoma kwenye hivi vitabu yani unaona kabisa ni alfu lela ulela.
 
Kwa mfano, watabiri wa hali ya hewa wanapotuambia kuhusu hali ya anga itakavyokuwa baadaye kabla ya muda huo kuwadia, hivi wao ndio wanaratibu na kuamuru hali iwe hivyo?

Ni kwamba wana ^uwezo^ fulani wa kuona mapema jinsi hali ya hewa itakavyokuwa.

Mungu pia ana UWEZO wa kuuona mwisho tangu mwanzo.
Twende pole pole....

Mtabiri anatabiri na ana uwezo wa kuona kutokana na viashiria vya sasa; (yeye sio aliyeweka hili jua liwe kali sana ili condensation itokee hence tupate mvua) hata kama mtu ana uwezo wa kuona ni tofauti na mtu aliyepanga all the moving parts yaani kama umetengeneza saa unajua kabisa nikinyonga hapa baada ya masaa ishirini na nne itasimama ila kila sekunde sitini huu mshale utasukuma huu ili huu usogee kwa nukta kadhaa na ukisogea mara sitini huu mkubwa usogee mara moja.... (huwezi kusema mshale mkubwa una free will ya kusogea au hapana) Sasa swali Mungu ni mtengenezaji wa hatua zote hizo au ni mtazamaji na anajua kutokana na hizo movement kama mimi na wewe tunavyojua kutokana na the actual design?!!!!

In short kama ulipanga / ulijua / ulitengeneza mtu ambaye atakuwa chizi na kuua wazazi wangu ili mimi nitapate kisirani maisha yangu yote na kuchukia watu na kufanya kisasi na mimi kuwa muuaji huwezi kusema my deeds hayakusababishwa na huyu ambaye aliwekwa hapo na wewe..., kwahio my destiny was determined by your design.....
 
Kuandika shida bana [emoji23]. Angalia youtube channel ya One Islam production (Satan and his army) utaelewa InShaAllah
 
Binadamu ni kiumbe wa mwisho kabisa kuumbwa na Mungu. Kabla ya mwanadamu kuletwa kuishi katika dunia hii walikuwapo majini wakiishi na wao ndio walikuwa watawala, ila walikuja kufanya ufisadi mkubwa na umwagaji wa damu.Mungu alituma jeshi la malaika kuja kuwapiga vita na wengi walikimbilia...
mapangoni,misituni,majangwani ,baharini na kwenye visiwa.
Naomba u-pause kwa sekunde chache alafu jiulize Mungu anajua kitakachotokea Kama jibu ni ndio nadhani usingeweka baadhi ya maelezo yako hapo chini kama ni hapa Okay tuendelee.
Mungu ndipo aliamua kuumba kiumbe mpya kuja kuwa mtawala/kiongozi katika dunia hii nae si mwingine bali ni mwanadamu.
Angejua haya yatafanywa na Majini si angeweza kutengeneza Mwanadamu kabla au sio kwamba aliamua kuumba kiumbe mwingine sema ule muda wa kuumba kiumbe mwingine ulifika
Malaika walistaajabu sana kwanini Mungu anataka kuumba kiumbe mwingine aje kuwa mtawala ardhini wakati majini walishafanya ufisadi na umwagaji wa damu mkubwa.? Mungu aliwajibu kuwa anayajua yale wasiyoyajua.So watulie waone ufundi wake.
Okay....
Nikijibu swali lako ni kuwa Kifo kililuwapo kabla ya Adam na Mungu alitangulia kuumba Pepo na Moto kabla ya kutuumba . Ilikuwa ikijulikana kuwa kuna siku ya mwisho (Qiyama) ila hakuna anayejua itakuwa lini.
Bali Mungu ?
 
Ndio maana wametumia watoto kwenye Household za dini na Household zisizo na dini. Mtoto wako kiranga ambaye kwako hujamfundisha kuhusu dini akionesha kuwa interested na mungu bila kufundishwa kuhusu Mungu hio haitokani na Practical realities za Maisha.

Mimi nimeleta utafiti, vyema na wewe unijibu kwa utafiti, maana ningekueleza blah blah ungesema haijakuwa proved.

Huo ni utafiti Multi country, Nchi 20 si jambo dogo. Je kuna utafiti unasema otherwise kama ndio ni upi?
Kwamba akionyesha pia interest kwenye Ipad, Video Games au Michezo Je...

Madogo wengine wanapenda sana Pipi na Chocholate na hapo tusemeje ?, Kwa uzoefu wangu madogo ni watukutu na wakiona wenzao wanakuwa favored wanawachukia na kuwafinya hapo niseme nini pia ?
 
Back
Top Bottom