Ni kwa sababu hicho kigezo chenu hakina uhalisia, ili wanawake wajitunze hadi ndoa maana yake na wanaume nao itabidi wakubali kujitunza hadi ndoa, wanawake wote wakisema wakitongozwa wakatae ili wajitunze maana yake wanaume watakosa wanawake wa kufanya nao tendo la ndoa
Sasa wanaume mkiambiwa nanyi mkubali kujitunza hadi ndoa hamtaki mnaleta visingizio vya kipuuzi eti nature, matokeo yake hata wanawake wakisema wakatae mtaendelea kuwashawishi tu, kumbuka nao ni binadamu siyo malaika kwahiyo mwisho wa siku msianze kulialia kwamba wanawake hawajitunzi ilihali nanyi hamko tayari
Lakini tukija kwenye kigezo cha pesa hicho kina uhalisia, kwa sababu mwanaume anapimwa kwa uwezo wake wa kubeba jukumu lake la kutunza na kuhudumia familia na hilo ndilo jukumu kubwa la mwanaume, sasa mwanaume usipokuwa na shughuli yoyote ya kukuingizia kipato huko ndoani unataka uende kufanya nini