Kwanini Mwanza Wanauza magari bei rahisi kuliko Dar es Salaam?

Dsm madalali wengi sana
Halafu wanaendekeza njaa,kuna mwaka niliuza gari kupitia dalali wa migo pale bila yeye kujua,baadae huko akaja kujua yule mteja aliyomleta ndie niliemuuzia alilalamika sana nimpe hata ya maji lakini ndio ikawa too late,mteja kafika bei niitakayo mimi na tena laki 7 juu,dalali hataki kuuza eti laki 7 ndogo na hapo hapo kwangu ilibidi ale kama 2 hivi,dogo wangu mmoja akachukua namba ya mteja kijanja pale pale,tukamuita docho tukafanya biashara
 
[emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419]
 
Sukubaliane nawewe zamani watu walikua wanatoka mwanza kuenda Dar kununua magari, ila sasa tredi imebadilika sasa watu wanatoka Dar kuja mwz kufuata hayo magari
 
Sukubaliane nawewe zamani watu walikua wanatoka mwanza kuenda Dar kununua magari, ila sasa tredi imebadilika sasa watu wanatoka Dar kuja mwz kufuata hayo magari
Chukua tahadhari unabishana na dalali kubwa la Dar tena muha[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Magari ya Mwanza mengi yamechoka sana ukilinganisha na ya Dar..magari yanayouzwa Mwanza yametumika Dar kisha yakauzwa huko..inasemekana 70% ya magari yanayoingizwa nchini hubaki Dar..na yanapochoka huuzwa huko mikoani
daah! Umetuonaje sisi huku mikoani tuchukue ndinga used kutoka dar kwani hatujui dar pia mnadaka ndinga 2nd hand.
 
Chukua tahadhari unabishana na dalali kubwa la Dar tena muha[emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji854]mimi nilikua dalali kwa miaka 10 nina uzoefu wa hiyo biashara trendi imebadilika kwabb kuu moja kwa 90% mkoa wa kagera Geita hununua magari yao kampala, ya kichoka kdgo kuyapeleka mwz kuyauza ndo maana bei zimeshuka sanaa ya used mwz
 
Oh kumbe sababu ni magari yao mabovu kutokana na utunzaji mbovu. Nashukuru kwa kunielewesha.

Ingawa nina watu wangu kadhaa wamenunu mwanza na zipo very clean… nitaendelea kufuatilia kwa watu wengi zaidi ili nisije kuingizwa chaka na gari zao
Uongo ni mazuri. Mi nilinunua langu huko na Nina miaka miwili wala halina shida youote
 
Wengine ni matapeli,
Anakutamanisha na Bei rahisi ila gari iko mikoani ili ukikolea anakuambia tuma hela ya mafuta uletewe Dar.
 
Magari ya mwanza ndiyo habari ya mjini. Mi nilinunua Brevis yangu huko, namba DNS, Lipo poa na Bomba kabisa.

Asante sana kwa mrejesho mkuu, tumejifunza mengi leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…