Kwanini Mwanza Wanauza magari bei rahisi kuliko Dar es Salaam?

1: watu wengi kule hawapendi kununua vitu vya mkononi...kwahyo wateja wachache..
2: Madalali wa kule huongeza pesa ndogo sana tofaut na huku Kinondoni /tegeta..
3: Mwanza sio kubwa sana..ukinunua gari ukiwa unatembea nayo unaanza kuitwa mzee X au unaulizwa ww ni dereva wa mzee X.
4: shimo likitema kwa wachimbaji...wanakuja na magari yao wanataka yabaki mwanza na wao warudi na mengine, hapa huuzwa kwa bei chee sana
 

Nashukuru sana mkuu naomba utupatie maujanja unafanyeje aiseh
 

Mkuu Shukran sana kwa maarifa haya

Mpaka sasa nimepata jawabu la swali langu
 
Nikiokota hela safari ya kwanza mwanzaaaaaaa[emoji23][emoji23]
 
Dar kuna tabia ya overpricing kila kitu sio magari tu fanya tafiti hata nguo, unaweza kukuta jeans Dar inauzwa 20000 to 30000 ila jeans yenye quality kama hiyo ukienda mkoani utaipata kwa 10000 au ukipigwa sana haizidi 15000, tatizo la Dar kila mtu anajifanya mkali.
 
Kwa mtazamo huo ni bora kununua used kagera kuliko kununua Mwanza...tupe uzoefu ndugu dalali mstaafu..[emoji119][emoji119][emoji119]
 
1.Mwanza mzunguko wa pesa si kama dsm, so ukiweka bei kubwa wengi hawanunui.

2. Dsm gari ni almost basic need but mwanza ni luxury.. uhitaji wa gari mwanza si wa lazima sana kwasababu usafiri ausumbui sana na hauna kero, pia trip za mwanza ni fupi fupi tofauti na DSm

3. Utanzaji wa gari kanda ya ziwa ni mbovu sana kulinganisha na dsm.. ukienda gereji za mwanza ukaona jinsi wanavofanya service za magari, oil wanazotumia, transmission fluid wanazotumia yaan unakuta wanaweka mi lubex kwenye transmission wakat mwingine wanaongezea na mioil eti iwe nzito dah.. nilishangaa sana..

So ukija nunua wakati mwingine you buy a time bomb so mtu anakua anatafuta namna ya ku dispose gari mapema kabla halijamfia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…