Kwanini nchi za kiarabu zinapingana na Quran kwa kufuta ndoa za wake wengi?

Kwanini nchi za kiarabu zinapingana na Quran kwa kufuta ndoa za wake wengi?

Execute

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2022
Posts
3,000
Reaction score
7,336
Nchi ya Uturuki, Tunisia na Iraq zimefuta kabisa ndoa za wake wengi huku Saudi Arabia ikiwa imeweka masharti makali kiasi kwamba hakuna watu wanaooa wake wengi.

Iran yenye watu milioni 88.5 ina ndoa za wake wengi zinazofikia laki moja tu. Algeria zinaelekea kupotea. Swali hapa ni kwanini hizi nchi zenye waislamu wengi hawataki kuoa wake wengi?
 
Ndoa za wake wengi kwa dunia ya leo mkongo lazima ahusike
Nawajua jamaa wawili maustaadhi Wandengereko wanapiga bodaboda Kariakoo mmoja ana wake wanne mwengine wawili na anasema soon ataongeza.

Jiulize mtu akimbize upepo mchana kutwa akalie tank halafu jioni amkunje mtu akunjike barrrabara hii anaweza?na zaidi ya mmoja?ni kuwatafuta watu lawama tu nadhani upo uwezekano watu hawajui dini yao inachosena wanaishia kuendekeza tamaa za miili yao.
 
Nchi ya Uturuki, Tunisia na Iraq zimefuta kabisa ndoa za wake wengi huku Saudi Arabia ikiwa imeweka masharti makali kiasi kwamba hakuna watu wanaooa wake wengi.

Iran yenye watu milioni 88.5 ina ndoa za wake wengi zinazofikia laki moja tu. Algeria zinaelekea kupotea. Swali hapa ni kwanini hizi nchi zenye waislamu wengi hawataki kuoa wake wengi?
Mkuu ni wewe uliyeandika hivi?

Elewa kwamba sharti la kuoa mke zaidi ya mmoja katika uislamu ni sharti lililokuja na uadilifu, sasa nadhan ungepata muda kujua uadilifu ni upi hasa uliozungumziwa hapa ili muislamu aongeze mke.

Unaposema wake wengi wamaanisha idadi ipi? katika Uislamu sheria imetutaka kuoa mke 1,2,3,4 hii ndio idadi ya mwisho ya kuowa wake kwa wakati mmoja katika uislamu.

Lakini pia yakupasa kujua kwamba idadi ya wanawake ulimwenguni ni mara 4 zaidi ya wanaume, hivyo unaweza kuona ndoa ni chache zilizofungwa mke zaidi ya mmoja sababu ya msingi nii hii., kama Irani population ni milioni 88.5 kwanini hukutaka kujua idadi ya wanawake na wanaume kati ya hiyo milioni 88.5 ni ngapi?? ndio uje hapa na hiyo idadi ya laki moja.

Unapotosha sana na wala hukuleta reference yoyote kwamba nchi za Uturuki na Saudia imeweka masharti makali kuongeza mke zaidi ya mmoja ni vile umepata muda tu kuwa hapa JF na kuandika chochote unachoweza kuandika
 
Lakini pia yakupasa kujua kwamba idadi ya wanawake ulimwenguni ni mara 4 zaidi ya wanaume
Kabla hata hatujafika mbali nipe ushahidi wa hili maana naona ni upotoshaji wa hali ya juu.

Kwasasa duniani wanaume ni wengi kuliko wanawake.

Screenshot_20230113-111350.png
 
Tukubaliane na ukweli tuu

Kwa Adam Kummudu Mwanamke mmoja tuu (Hawa) ilikua shughuli pevu
Kwa Ibrahimu alijaribu kwa kijakazi moto ukawaka

Kwa Isaka mke alimzidi ujanja akajikuta kampa baraka Yakobo na kumwacha Esau na wote ni watoto wa tumbo moja tena mapacha

Sembuse wa leo

Binafsi mimi sijatosheka bado ili niletewe msaada🤣🤣🤣
 
Nchi ya Uturuki, Tunisia na Iraq zimefuta kabisa ndoa za wake wengi huku Saudi Arabia ikiwa imeweka masharti makali kiasi kwamba hakuna watu wanaooa wake wengi.

Iran yenye watu milioni 88.5 ina ndoa za wake wengi zinazofikia laki moja tu. Algeria zinaelekea kupotea. Swali hapa ni kwanini hizi nchi zenye waislamu wengi hawataki kuoa wake wengi?
Wako sawa, wameona hawawezi kuwafanyia insafu!
Ilaha Allah kawapa wepesi vibubu Ruksa[emoji1376][emoji1360][emoji1676]
[emoji1370][emoji1370]
وَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تُقْسِطُوا فِي
الْيَتَامَىٰ فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَلَّا تَعُولُوا

[ AN-NISAAI - 3 ]
Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu, basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane. na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu, au wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. Kufanya hivi ndiko kutapelekea msikithirishe wana.
 
Mkuu nakuomba sana lete reference nani Saudia na Uturuki amezuia ndoa za kuoa mke zaidi ya mmoja katika Uislamu usinilitee habari za google na Wikipedia, hivi kumbe wewe umekuja na habari hizi kwa sababu ya google search, unaweza kunambia hiyo taarifa uliyosoma google imeekwa nani? Mimi sifanyii kazi kazi habari za google.

Lete reference Mfalme wa Saudia Arabia amezuia sheria ya kiislamu kutekelezeka katika nchi yake ya kuoa mke zaidi ya mmoja ama amepiga marufuku.
 
Nchi ya Uturuki, Tunisia na Iraq zimefuta kabisa ndoa za wake wengi huku Saudi Arabia ikiwa imeweka masharti makali kiasi kwamba hakuna watu wanaooa wake wengi.

Iran yenye watu milioni 88.5 ina ndoa za wake wengi zinazofikia laki moja tu. Algeria zinaelekea kupotea. Swali hapa ni kwanini hizi nchi zenye waislamu wengi hawataki kuoa wake wengi?
Wabongo sasaaa.
Wameona huo ndo ufahari wa kuacha na kuoa kila siku na ukizingatia hata mahari ya 50k unapewa mke basi ni shiiida.
Ifike mahali watu waache ulimbukeni.
 
Back
Top Bottom