Kwanini ndugu wa mwanamke mara zote hukaa kwenye familia kuliko ndugu wa mwanaume?

Kunywa soda nalipa
 
Hayakuhusu waachie wenyewe
 
Wengine ndio tabia zao tu. Huwezi kuwa na roho nzuri wakati kiuhalisia una roho mbaya. Vile vile kama nzuri unayo huwezi ficha, utaishi uzuri tu. Roho mbaya sema hata wababa tunazo sana tu, sema kwa mwanamke inakua kali sana maybe kutokana na mazingira aliyopo yeye. Lets say jikoni kule aamue kuweka chochote kibaya kwny chakula watu wadhurike. Hapo hata ww usiewajua ukiskia tu lazima useme mwanamke ana roho mbaya. Mifano tunaiona huko mitaani jamani, kwani hakuna wababa wanaopiga watoto mbaka wakaua??? Hii sio roho mbaya???(screenshots za mifano ya pande zote tu kwa roho mbaya)
 

Attachments

  • Screenshot_20230818-223100.png
    111.9 KB · Views: 2
  • Screenshot_20230818-223153.png
    139.8 KB · Views: 2
Aisee
 
Umaskini ndo chanzo cha hii migogoro kiukweli. Sioni jipya hapa. Na hapa namaanisha umaskini wa roho sio vitu. Maana ukiwa tajiri wa roho utaona mambo yote ya kupita tu. Hakuna la kudumu hapa duniani. Lakini jambo moja tunalotakiwa kulijua, neno linasema ndoa na IHESHIMIWE na watu wote. Haijabagua mtu yeyote be it parents or siblings au ndugu matembele.

Nakukaribisha kwangu kiroho sayona, ishi katika mipaka yako. Tunaamka, tutafanya kazi kwa ushirikiano, saa ya kupumzika kila mtu achague chimbo lake. Matumizi ndani ya nyumba anayeoversee ni mama. Nobody anatakiwa kumpangia kwamba wifi/shem tunataka upike hiki leo, maana yeye ndo anayejua budget. Suala la jiko la mwanamke si la kuingiliwa. Unapofika kwenye nyumba ya mtu, heshimu hilo. Lakini na sisi maza mijengo, omba utajiri katika roho yako. Sio wageni wanakuja unakumbuka choroko na maharage yalipo...it doesnt hurt kuvunja kibubu kwa timeframe ndogo ambayo umepata wageni katika malango yako. Kwani kuku nyama ni bullshit gani za kukugombanisha na watu??

Ninachoona pia mara nyingi ni watu kutaka kuishi katika mifumo yao waliyozoea kwao na kutaka kuihamishia kwa kaka/dada yao. Binafsi napenda wageni lakini nina principles za kuishi kwangu. Either uzifate kwa upendo au nionekane mkorofi. Though kugombana sio prospect yangu. Nitafanya mwenyewe nikikuona sikuelewi..dunia itakufundisha one day. All in all, tuheshimu ndoa na familia ama kila mtu abaki kwake. Nina kaka zangu wameoa na dada zangu wameolewa. In few times, pamoja na utu uzima wangu nimeshawahi kuwatembelea. Naishi kuendana na mifumo ya nyumba yao. Nikiwakuta wana utaratibu wa kusali nimo, nikiwakuta wana utaratibu wa kuamka saa kumi na moja kuokota mayai nimo.

Kwanini niwe kwazo kwenye nyumba za watu? Wifi akisema flani naomba unisaidie hiki ni sawa. Maana hata kwangu si ninafanya. Heshima heshima heshima...kama huwezi utaona wifi/shem mbaya.
 
Ujumbe umefika mama naniii, umeandika simpo but straight foward....wameskia
 
Wanawake wanaogopa siku wakitengana kusije kukawa na ndugu wa kumzidi nguvu na kumpora mali.
Afadhali wawe mbali huko kuepusha sintofahamu hii.

Pia Wanawake huw wanaamini mume atakufa atamwacha. Sijui kwanini... lakini kuna kaukweli hivi. Wanaume wengi hufa na kuwaacha wake wakiendelea na maisha na hata kuolewa tena.

Zaidi, wanawake hupata muda mwingi wa kujishughulisha na kazi za nyumbani. Watawalinda ndugu zao kuliko hao wa mume. Ndugu wa mume atajiona mgeni na hata huyo aliyekuja kwake mara nyingi hayupo nyumbani.

Poleni wanaume wenzangu.
 
Wanawake wanaogopa siku wakitengana kusije kukawa na ndugu wa kumzidi nguvu na kumpora mali.
Afadhali wawe mbali huko kuepusha sintofahamu hii.

Pia Wanawake huw wanaamini mume atakufa atamwacha. Sijui kwanini
Mnakufa mapema mno🤣🤣
 
Kweli mwastahili pole aisee
 
Ndugu wa mke wanadumu kwa sababu.
Mwanamke ambaye ndio mke yeye ndio anashinda nyumbani au anapanga taratibu zote za nyumbani. Kumbuka hao ndugu zake wameishi pamoja kabla ndugu yao hajaolewa kwahiyo wanajuana tabia vyema.

Na taratibu mke anazozipanga za nyumbani huwa hazitofautiani sana na za nyumbani kwao alipotokea hivyo basi ni rahisi sana ndugu wa upande wake kuendana nazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…