Kwanini ni lazima nioe Mwanamke wa Kaskazini?

Kwanini ni lazima nioe Mwanamke wa Kaskazini?

hujawahi kubaguliwa siyo? Subiri siku yaja halafu urudi tena huku.

Nibaguliwe mara ngapi?
Maisha ni ubaguzi halisi ndio maana tupo tofauti.
Hayo mengine ni unafiki tuu wa Mwanadamu,
Mwanadamu ni mbinafsi by nature, ukishasema MTU ni mbinafsi ujue ushazungumzia ubaguzi
 
Habari za Leo.

Kwangu ni lazima kuoa Mwanamke wa Kaskazini au jamii zinazokaribiana Mila, desturi, falsafa na mitizamo kama ya Wanawake WA Kaskazini. Kuoa Mwanamke wa Kaskazini kwangu Sio Optional, bali ni lazima. Hii itabaki kuwa hivyo ilivyo.

Sio kila mtu atakayetaka kujua sababu ya Mimi kuwa na uamuzi huo, kwani ni uamuzi binafsi unaohusu Maisha yangu mwenyewe lakini ninauhakika wapo watakaotaka kujua sababu ya Mimi kuwa na Uamuzi huo.

Wanawake WA Kaskazini ni Wanawake wote wenye tabia halisi za Mwanamke wa shoka bila kujali amezaliwa Iringa, Kigoma, mtwara, Morogoro, Mwanza, Moshi, Musoma .n.k.

Zifuatazo ni sababu za Kwa nini Taikon lazima Aoe Mwanamke wa Kaskazini;

1. Wanapenda Mali.
Kwa jamii zingine huona Jambo Hilo katika mtazamo Hasi lakini Kwa wanaume Strong tunachukulia Jambo hilo kama Motivation.
Mwanamke lazima apende Mali, ili kuzalisha Vijana wachapakazi na sio vijana wavivu na wazembe wazembe.

Ili mwanaume uheshimike Mali ni moja ya vigezo vya kumfanya mwanaume aonekane yupo serious na Maisha. Fanya kazi Kwa bidii na juhudi yenye Akili.
Ukiona eneo hilo limekushinda Hama tafuta sehemu nyingine, sio unakaa sehemu moja kama Mwanamke.
Wanawake WA Kaskazini kumwambia unaenda kutafuta Maisha nchi za mbali yeye haoni shida, au kumwambia muondoke wote muhame mwende Mikoa ya mbali kwao sio tatizo ili mradi umwambie kuna mchongo wa kutafuta Maisha.

Hii ni tofauti na Baadhi ya Wanawake WA jamii zingine, ukiwambia mhame mwende mbali watawaza sijui wazazi sijui ndugu kwamba watakuwa mbali na nyumbani.

Kupenda Mali kunazalisha Vijana wawe wachapakazi na Risk taker,

2. Wanakiu ya Maendeleo Kwa Watoto wao.
Wanawake WA Kaskazini hata umtelekezee mtoto hapo ninakuhakikishia lazima atasoma kivyovyote vile bila kutegemea Pesa yako.
Wanawake WA Kaskazini wengi wao ndio wazalishaji hasa WA hizi kazi ndogondogo Kam umachinga WA nguo, kuuza mitumba, kulima vibarua kwenye mashamba, n.k.
Vijana wengi wa Kaskazini wamesomeshwa na Mama zao.
Wababa wanasimamia shoo kubwakubwa kama ujenzi wa nyumba, ununuzi wa viwanja na utanuzi wa Ngome na miradi.

Sasa ni Mwanaume gani Strong ambaye hatataka kuoa Mwanamke wa Kaskazini ikiwa anauhakika hata asipokuwepo Watoto wake wataishi vizuri, sidhani kama kuna mwanaume wa hivyo.

3. Hawapendi wanaume Cheaters.
Ukitaka uonje joto la Jiwe basi OA Mwanamke wa Kaskazini alafu mfanyie mambo ya kiduwanzi, mcheat mara Kwa mara uone nini kitatokea.
Utawahadithia wenzako na utakuwa fundisho Kwa wengine. Kwanza lazima utoke ndani ya nyumba kivyovyote iwe Kwa Amani au Kwa Shari.
Wale wanaume Werevu wakishaona wametosheka na kukinaiwa na Wake zao huwaachia Nyumba(Mji) na kuendelea na Maisha mengine. Lakini hawapeani Talaka. Hiyo mbinu inatumiwa na wanaume wajanja.

Lakini wale wanaume wajinga hugangamala hapohapo na ndipo ubaya wa Wanawake WA Kaskazini utakapoonekana. Hakuna rangi ambayo hautaacha kuiona.

4. Huwezi kuwatapeli Mali Kama mlichuma Wote.
Kwanza hakuna kazi ngumu kama kumtoa Mwanamke wa Kaskazini ndani ya nyumba hasa kama mmejenga wote. Ni ngumu Sana. Kesi hiyo itasimamiwa vilivyo na atapata uungwaji mkono na Ndugu zake Kwa namna yoyote Ile.
Hii inamaanisha unapooa Mwanamke wa Kaskazini lazima ujue mlango wa kutokea endapo ikitokea mkiachana. Kwani wengi wao wana-backup ya Kufa mtu Kutokana na umoja waliokuwa nao.
Hivyo kama Mwanaume kwenu ukoo wenu hauna umoja kila MTU kivyake inaweza kukugharimu.

Hii inahamasisha Vijana kuunganisha nguvu na Ndugu zao. Sio kijana ukishaoa tuu unakata mawasiliano na Ndugu zako unashindwa hata kuwainua, ninakuhakikishia inaweza ikakusumbua Huko Mbele.

5. Ni Wakali na hawadekezi Watoto.
Labda ninashindwa kueleza Jambo hili vizuri. Lakini Wamama wa Kaskazini ni Wakali Kwa Watoto kuliko Wababa. Wanaume ni Wakali linapokuja suala la utafutaji na mipaka ya Ardhi lakini kwenye malezi wamama wameshindikana.

6. Ni washamba Kwa Mambo ya Kijingajinga yasiyoingiza Pesa.
Wanawake WA Kaskazini ni washamba Kwa mambo yasiyo na tija, mfano sijui udaku wa masupastaa, sijui kukata mauno au kucheza, sijui kuunganisha madanga, Kwa kweli Kwa hayo mambo NI washamba, wengi hawajui na hawafuatilii hivyo vitu.

Wao wanachojua ni Mambo ya Pesa, sijui Vikoba, Michezo, Brac, kuuza Kwa kukopeshana, ujenzi, usomeshaji wa watoto, biashara n.k. hayo ndio mambo Yao.

7. Wengi Hawana Umalaya.
Umalaya ni tabia mara nyingi inayochangiwa na Mwanamke kuwa tegemezi, utegemezi unaleta tamaa alafu Pesa hauna.
Utachunguza mwenyewe Wanawake wenye Tabia za kimalaya wengi wanatoka jamii tegemezi ambazo wao kila Pesa wanamtegemea mwanaume.
Pesa ya Kodi mwanaume,
Pesa ya chakula mwanaume,
Pesa ya kusomeshea mtoto mwanaume,
Pesa ya mavazi mwanaume
Pesa ya kila kitu mwanaume alafu kazi huna Mwanamke ataachaje kuwa Malaya.
Wanawake wengi WA Kaskazini na jamii zinazofanana NAO ni wachakarikaji, wanajua Pesa inavyotafutwa Kwa kazi ndogondogo na biashara za Kati.
Mwanaume akitafutwa ni kwaajili ya kufanya Maisha.
Weka niweke.

8. Hawana unyenyekevu Kwa Wanaume wapumbavu.
Wanawake WA Kaskazini wamefundishwa kujitambua, Haki zao. Mheshimu atakuheshimu, mpende atakupenda, mshirkishe atakushirikisha. Hawana mambo ya unafiki.
Wanawake WA Kaskazini kwenye hii nchi ndio wanaoongoza Kwa kuhonga Vijana waaminifu. Yaani ukitaka kwenda naye Sawa basi Mpe Haki zake naye akupe Haki zako.

Tabia hiyo inachukuliwa na wanaume dhaifu kama ujeuri, kiburi na kutokuwa na heshima. Jambo ambalo sio Sahihi.
Mwanamke wa Kaskazini na jamii zinazofanana nayo hawezi kukuheshimu kama Mume wake ikiwa kuna mambo unapuyanga, yaani ufanye uhuni na umalaya wa kujirudiarudia alafu utegemee heshima. Hizo ni dharau kubwa.

Sisi kama Kaka zao na Baba zao tumewafundisha wasivumilie hiyo Hali endapo ikijitokeza Kwa kujirudiarudia mara Kwa mara. Ndio maana tunawafanya wajitegemee kiuchumi zaidi ili wasinyanyasike na kunyanyaswa na wanaume wendawazimu.

Hakuna mwenye Haki ya kufanya uhalifu au uovu Kwa Mwenzake iwe Mwanamke au Mwanaume. Mimi kuwa mume wa Fulani sio kigezo cha kumpiga au kumrudia Usiku WA manane nikiwa nimelewa, hiyo hauvumiliki, na ninachowapendea Wanawake WA Kaskazini hawatakukopesha watakujibu Kwa nguvu zote.
Aidha muachane au ubadilike. Na mkiachana mtasomana kwenye mgawanyo wa Mali na kuhudumia Watoto.

Kama ni MTU mwenye Tabia za umungu mtu sikushauri ukaoe Kaskazini, kama ni Mwanaume usiyependa HAKI basi Kaskazini sio sehemu sahihi kwako.
Mnaweeza Anza vizuri hasa kama unamali au unavikazi kazi vyenye kipato lakini ninakuhakikishia Baada ya miaka 20 picha litaanza kugeuka, hapo Watoto wamekua ni muda wa kujibu mapigo.

Wanawake WA Kaskazini wengi huonekana ni Feminist Kutokana na Ile Hali wanayokabiliana na uonevu na unyanyasaji wa baadhi ya wanaume wajingawajinga.

Unapomuoa Mkeo elewa kuwa huyo ni Msaidizi wako, mnasaidizana majukumu ya kimaisha na sio mmoja kumfanya mtumwa mwingine. Mwanaume asiwe mtumwa wa Mwanamke, pia Mwanamke asiwe mtumwa wa Mwanaume. Wote muwe kitu kimoja. Mnapokabiliana na mambo yenu yawekeni bayana mjue mnayatatuaje,

Ugumu unatoka wapi?
Wengi hujikuta katika ubinafsi ndio maana migogoro haiishi.
Mfano Mwanamke anazalisha laki tano kwa mwezi, mwanaume naye laki tano.
Hiyo Pesa Kwa nini msiiweke pamoja kisha muipangie matumizi pamoja?
Au mmoja anapokea laki tatu mwingine laki Saba. Mnaona shida gani kuunganisha hizo Pesa.
Kama ni kusaidia nyumbani si msaidie, mnaona shida gani?
Semeni Kila mwezi elfu 50 itaenda familia ya MKE, elfu 50 itaenda familia ya Mme. Jumla ni laki moja itatengwa Kwa Pesa ya Wazazi.

Sasa mkishaanza kuleta mambo ya mzazi wangu, mzazi wangu sijui kanisomesha sijui kanizaa, kwani Nani hakuzaliwa? Kwani Nani hakusomeshwa, sijui Mimi nimekuoa nimekutolea Mahari hiyo Mahari ndio nimemalizana na kwenu, hivi wewe ni Kichwa? Mahari ya milioni mbili au hata milioni 10 ndio umemalizana uliambiwa hiyo ni Ng'ombe?

Alafu kuna mizazi mingine kama imelogwa, ati kisa limesomesha basi linataka mtoto wake amhudumie yeye kuliko familia yake, umelogwa wewe mzazi, kama unataka kumpangia matumizi mwanao au Binti yako ungemuoa au kuolewa naye, pumbavu.

Watu wamejaa ubinafsi Sana!

Ngoja nipumzike!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam

Robert Heriel 🔥🔥👊
 
Afadhali jamani watoto wetu wa kike wapate wachumba/waume wanaowazimia kama mleta uzi.Binti yangu anaambiwaga wewe "mpalestina" huwa kinaniuma sana na Mungu anawaona aisee.
Pole sana, wana ubabe fulani sio poa. Yaani kama wewe sio kidume ukasimama kiuwanaume hakika huwawezi. Ila mengi aliyosema mleta mada ni sahihi kabisa.

..huoni wakitaka kuwekwa hovyo yani, labda hawa wanaochipukia kwa sasa, ila wale wa marika tuliooa hawana mda na hizo mambo kivile.
 
Mwanzo kabisa nimecomment kua mwanamke unamshape wewe aweje. Wewe ndie kichwa cha familia.

Na kulingana na mkeo utajua umuweke angle ipi itayomfaa. Anawezakua mchakarikaji lakini hajali watoto, mfujaji wa mali nk.
Sio kutaka tu mchakarikaji moja kwa moja huo ni uoga, na uoga huo utadhihirika mbele ya mkeo kadri siku zinavyoyoma huko ndoani. Mwisho wa siku uonekane galasa.

Hujaona shuhuda za hao wanawake unaowaita wachakarikaji wakiwananga waume zao mitandaoni kua hawaihudumii familia, lakini deepdown jamaa anahudumia. Sababu kua ni hiyo kuwapa nafasi zetu za uanaume wazitumie badala ya sisi kusimamia nafasi zetu.

Mbwa Mzee hafundishwi kuwinda.

Sijasema kuwa Hawana Tabia Mbaya, Mimi nimeeleza mazuri Yao yanayonifanya niwaoe, sio kwamba sijui mapungufu Yao.
 
Watu wanapitia mazito sana hapo Moshi na Meru tena kwenye mzizi wenyewe kabisa na ni wao kwa wao ila mwamba hashiki rimoti.

Tuongee ukweli, hivi kuna mwanamke mkorofi hii Tanzania kama mwanamke wa kimeru?

Mdada wa kimeru anajibizana na konda kwenye gari na konda anaufyata sasa hao ukaoe si utafungiwa stoo kabisa

Na kaka zao wanajidai wakorofi kwa watu wa nje ila akiambiwa Shuuu!, anakuwa mdogo kama piritoni alafu unakuta kaambiwa na kadada ka kimeru chenye chuchu saa sita, [emoji23][emoji23]
Unakuta pisi kali inakupa mchezo wa maana usiku na inautamu balaa. Halafu ndio inakufokea dah unajikuta unakuwa mpole tu japo upate mzigo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Fanya kazi siku sita kisha yasaba pumzika, hiyo ndio Kanuni Mkuu.

Sasa kama wewe unataka mwanamke ambaye anataka uishi kivulana, mnafanya kazi siku Mbili mnapumzika siku tano huyo atakupeleka wapi Mkuu?

Ni lazima uoe Mwanamke anayetaka kukuona mumewe unatimiza ndoto na malengo ya famili. Sio unalalalala[emoji23]
Huyo mwanamke anafuata malengo yangu malengo yake au malengo yetu.

Mimi kama nimeplan baada ya miaka mitano tuwe tumeshajenga nyumba mbili, tufungue duka la biashara na kumiliki hata IST moja then hiyo ndio kitu nitasimamia, yeye kama atataka tumiliki ghorofa sita, tuwe na milioni 200 kwenye account, nje tupaki VX na BMW na December twende Marangu kwa ndege tukifika tutembeze noti na kutatua shida ndogo ndogo za ukoo wake, huyo sio mwanamke kwangu huyo ni takataka.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
Ati kufungiwa Stop nimecheka kifala Sana.

Lazima mwanaume ujifunze Martial arts Mkuu . Vinginevyo baadhi ya Wanawake wakaskazini kama Tarime watatingisha kidevu hicho[emoji23][emoji23]
Sasa umeingia kwenye mahusiano ya kimapenzi au mahusiano ya Kijeshi na mgambo wa kulinda amani congo.
 
Na ikawe ivo mkuu, tuendelee kupendana ukabila haufai
Alichokiandika ni kweli kabisa Kuna Mama ni Mchaga yaani ni Mama wa rafiki yangu nakumbuka wakati nipo std 5 mpaka form two yule Mama alinipenda kwa sababu ya Upole, Ukweli na Uaminifu kuliko Mwanae wa kumzaa niliishi naye vizuri sana mpaka nilipohama Shule kwenda Dar siku naondoka yule Mama alitoa machozi na akaniambia nitakukumbuka na ninakupenda sana Manyanza. Nilijitahidi baada ya kumaliza form four nilienda kumsalimia alifurahi sana. Na nilimkuta maisha yake yamekuwa mazuri sana na Mume wake alikuwa ni Meneja kwenye shirika Fulani lakini bahati mbaya nikaanguka dhambini na mwanaye wa Kike alinimaindi lakini akanisamehe tu. Na siku narudi Dar alinunulia na nguo na Miaka kadhaa mbele nilipopata Kazi baada ya kumaliza chuo nilimtumia 500,000 na Mapazia ya Home Shopping Centre. Alifurahi sana. Kwa kifupi yule Mama ni mtu na ana utu na ni Mpambanaji sana. Anafuga Kuku , Ng'ombe na Nguruwe na likija suala la kuchapa kazi nilikuwa nachapa kazi kweli kweli. Mtazamo wa thread ya Jana ya Cc country Wide na wa Herbert kwenye hii thread umekuwa ni tofauti. Kwa kifupi kizazi cha Mabinti wa miaka ya 1990 mpaka 2000 ndio kinachochafua legacy ya Wanawake wa Kasikazini. Maana Kuna Demu wa Kasikazini alikimbia na jembe langu na akaacha kazi yenye Mshahara wa maana kisa Jamaa wa zamani alipata kazi nzuri huko UGHAIBUNI.
 
Habari za Leo.

Kwangu ni lazima kuoa Mwanamke wa Kaskazini au jamii zinazokaribiana Mila, desturi, falsafa na mitizamo kama ya Wanawake WA Kaskazini. Kuoa Mwanamke wa Kaskazini kwangu Sio Optional, bali ni lazima. Hii itabaki kuwa hivyo ilivyo.

Sio kila mtu atakayetaka kujua sababu ya Mimi kuwa na uamuzi huo, kwani ni uamuzi binafsi unaohusu Maisha yangu mwenyewe lakini ninauhakika wapo watakaotaka kujua sababu ya Mimi kuwa na Uamuzi huo.

Wanawake WA Kaskazini ni Wanawake wote wenye tabia halisi za Mwanamke wa shoka bila kujali amezaliwa Iringa, Kigoma, mtwara, Morogoro, Mwanza, Moshi, Musoma .n.k.

Zifuatazo ni sababu za Kwa nini Taikon lazima Aoe Mwanamke wa Kaskazini;

1. Wanapenda Mali.
Kwa jamii zingine huona Jambo Hilo katika mtazamo Hasi lakini Kwa wanaume Strong tunachukulia Jambo hilo kama Motivation.
Mwanamke lazima apende Mali, ili kuzalisha Vijana wachapakazi na sio vijana wavivu na wazembe wazembe.

Ili mwanaume uheshimike Mali ni moja ya vigezo vya kumfanya mwanaume aonekane yupo serious na Maisha. Fanya kazi Kwa bidii na juhudi yenye Akili.
Ukiona eneo hilo limekushinda Hama tafuta sehemu nyingine, sio unakaa sehemu moja kama Mwanamke.
Wanawake WA Kaskazini kumwambia unaenda kutafuta Maisha nchi za mbali yeye haoni shida, au kumwambia muondoke wote muhame mwende Mikoa ya mbali kwao sio tatizo ili mradi umwambie kuna mchongo wa kutafuta Maisha.

Hii ni tofauti na Baadhi ya Wanawake WA jamii zingine, ukiwambia mhame mwende mbali watawaza sijui wazazi sijui ndugu kwamba watakuwa mbali na nyumbani.

Kupenda Mali kunazalisha Vijana wawe wachapakazi na Risk taker,

2. Wanakiu ya Maendeleo Kwa Watoto wao.
Wanawake WA Kaskazini hata umtelekezee mtoto hapo ninakuhakikishia lazima atasoma kivyovyote vile bila kutegemea Pesa yako.
Wanawake WA Kaskazini wengi wao ndio wazalishaji hasa WA hizi kazi ndogondogo Kam umachinga WA nguo, kuuza mitumba, kulima vibarua kwenye mashamba, n.k.
Vijana wengi wa Kaskazini wamesomeshwa na Mama zao.
Wababa wanasimamia shoo kubwakubwa kama ujenzi wa nyumba, ununuzi wa viwanja na utanuzi wa Ngome na miradi.

Sasa ni Mwanaume gani Strong ambaye hatataka kuoa Mwanamke wa Kaskazini ikiwa anauhakika hata asipokuwepo Watoto wake wataishi vizuri, sidhani kama kuna mwanaume wa hivyo.

3. Hawapendi wanaume Cheaters.
Ukitaka uonje joto la Jiwe basi OA Mwanamke wa Kaskazini alafu mfanyie mambo ya kiduwanzi, mcheat mara Kwa mara uone nini kitatokea.
Utawahadithia wenzako na utakuwa fundisho Kwa wengine. Kwanza lazima utoke ndani ya nyumba kivyovyote iwe Kwa Amani au Kwa Shari.
Wale wanaume Werevu wakishaona wametosheka na kukinaiwa na Wake zao huwaachia Nyumba(Mji) na kuendelea na Maisha mengine. Lakini hawapeani Talaka. Hiyo mbinu inatumiwa na wanaume wajanja.

Lakini wale wanaume wajinga hugangamala hapohapo na ndipo ubaya wa Wanawake WA Kaskazini utakapoonekana. Hakuna rangi ambayo hautaacha kuiona.

4. Huwezi kuwatapeli Mali Kama mlichuma Wote.
Kwanza hakuna kazi ngumu kama kumtoa Mwanamke wa Kaskazini ndani ya nyumba hasa kama mmejenga wote. Ni ngumu Sana. Kesi hiyo itasimamiwa vilivyo na atapata uungwaji mkono na Ndugu zake Kwa namna yoyote Ile.
Hii inamaanisha unapooa Mwanamke wa Kaskazini lazima ujue mlango wa kutokea endapo ikitokea mkiachana. Kwani wengi wao wana-backup ya Kufa mtu Kutokana na umoja waliokuwa nao.
Hivyo kama Mwanaume kwenu ukoo wenu hauna umoja kila MTU kivyake inaweza kukugharimu.

Hii inahamasisha Vijana kuunganisha nguvu na Ndugu zao. Sio kijana ukishaoa tuu unakata mawasiliano na Ndugu zako unashindwa hata kuwainua, ninakuhakikishia inaweza ikakusumbua Huko Mbele.

5. Ni Wakali na hawadekezi Watoto.
Labda ninashindwa kueleza Jambo hili vizuri. Lakini Wamama wa Kaskazini ni Wakali Kwa Watoto kuliko Wababa. Wanaume ni Wakali linapokuja suala la utafutaji na mipaka ya Ardhi lakini kwenye malezi wamama wameshindikana.

6. Ni washamba Kwa Mambo ya Kijingajinga yasiyoingiza Pesa.
Wanawake WA Kaskazini ni washamba Kwa mambo yasiyo na tija, mfano sijui udaku wa masupastaa, sijui kukata mauno au kucheza, sijui kuunganisha madanga, Kwa kweli Kwa hayo mambo NI washamba, wengi hawajui na hawafuatilii hivyo vitu.

Wao wanachojua ni Mambo ya Pesa, sijui Vikoba, Michezo, Brac, kuuza Kwa kukopeshana, ujenzi, usomeshaji wa watoto, biashara n.k. hayo ndio mambo Yao.

7. Wengi Hawana Umalaya.
Umalaya ni tabia mara nyingi inayochangiwa na Mwanamke kuwa tegemezi, utegemezi unaleta tamaa alafu Pesa hauna.
Utachunguza mwenyewe Wanawake wenye Tabia za kimalaya wengi wanatoka jamii tegemezi ambazo wao kila Pesa wanamtegemea mwanaume.
Pesa ya Kodi mwanaume,
Pesa ya chakula mwanaume,
Pesa ya kusomeshea mtoto mwanaume,
Pesa ya mavazi mwanaume
Pesa ya kila kitu mwanaume alafu kazi huna Mwanamke ataachaje kuwa Malaya.
Wanawake wengi WA Kaskazini na jamii zinazofanana NAO ni wachakarikaji, wanajua Pesa inavyotafutwa Kwa kazi ndogondogo na biashara za Kati.
Mwanaume akitafutwa ni kwaajili ya kufanya Maisha.
Weka niweke.

8. Hawana unyenyekevu Kwa Wanaume wapumbavu.
Wanawake WA Kaskazini wamefundishwa kujitambua, Haki zao. Mheshimu atakuheshimu, mpende atakupenda, mshirkishe atakushirikisha. Hawana mambo ya unafiki.
Wanawake WA Kaskazini kwenye hii nchi ndio wanaoongoza Kwa kuhonga Vijana waaminifu. Yaani ukitaka kwenda naye Sawa basi Mpe Haki zake naye akupe Haki zako.

Tabia hiyo inachukuliwa na wanaume dhaifu kama ujeuri, kiburi na kutokuwa na heshima. Jambo ambalo sio Sahihi.
Mwanamke wa Kaskazini na jamii zinazofanana nayo hawezi kukuheshimu kama Mume wake ikiwa kuna mambo unapuyanga, yaani ufanye uhuni na umalaya wa kujirudiarudia alafu utegemee heshima. Hizo ni dharau kubwa.

Sisi kama Kaka zao na Baba zao tumewafundisha wasivumilie hiyo Hali endapo ikijitokeza Kwa kujirudiarudia mara Kwa mara. Ndio maana tunawafanya wajitegemee kiuchumi zaidi ili wasinyanyasike na kunyanyaswa na wanaume wendawazimu.

Hakuna mwenye Haki ya kufanya uhalifu au uovu Kwa Mwenzake iwe Mwanamke au Mwanaume. Mimi kuwa mume wa Fulani sio kigezo cha kumpiga au kumrudia Usiku WA manane nikiwa nimelewa, hiyo hauvumiliki, na ninachowapendea Wanawake WA Kaskazini hawatakukopesha watakujibu Kwa nguvu zote.
Aidha muachane au ubadilike. Na mkiachana mtasomana kwenye mgawanyo wa Mali na kuhudumia Watoto.

Kama ni MTU mwenye Tabia za umungu mtu sikushauri ukaoe Kaskazini, kama ni Mwanaume usiyependa HAKI basi Kaskazini sio sehemu sahihi kwako.
Mnaweeza Anza vizuri hasa kama unamali au unavikazi kazi vyenye kipato lakini ninakuhakikishia Baada ya miaka 20 picha litaanza kugeuka, hapo Watoto wamekua ni muda wa kujibu mapigo.

Wanawake WA Kaskazini wengi huonekana ni Feminist Kutokana na Ile Hali wanayokabiliana na uonevu na unyanyasaji wa baadhi ya wanaume wajingawajinga.

Unapomuoa Mkeo elewa kuwa huyo ni Msaidizi wako, mnasaidizana majukumu ya kimaisha na sio mmoja kumfanya mtumwa mwingine. Mwanaume asiwe mtumwa wa Mwanamke, pia Mwanamke asiwe mtumwa wa Mwanaume. Wote muwe kitu kimoja. Mnapokabiliana na mambo yenu yawekeni bayana mjue mnayatatuaje,

Ugumu unatoka wapi?
Wengi hujikuta katika ubinafsi ndio maana migogoro haiishi.
Mfano Mwanamke anazalisha laki tano kwa mwezi, mwanaume naye laki tano.
Hiyo Pesa Kwa nini msiiweke pamoja kisha muipangie matumizi pamoja?
Au mmoja anapokea laki tatu mwingine laki Saba. Mnaona shida gani kuunganisha hizo Pesa.
Kama ni kusaidia nyumbani si msaidie, mnaona shida gani?
Semeni Kila mwezi elfu 50 itaenda familia ya MKE, elfu 50 itaenda familia ya Mme. Jumla ni laki moja itatengwa Kwa Pesa ya Wazazi.

Sasa mkishaanza kuleta mambo ya mzazi wangu, mzazi wangu sijui kanisomesha sijui kanizaa, kwani Nani hakuzaliwa? Kwani Nani hakusomeshwa, sijui Mimi nimekuoa nimekutolea Mahari hiyo Mahari ndio nimemalizana na kwenu, hivi wewe ni Kichwa? Mahari ya milioni mbili au hata milioni 10 ndio umemalizana uliambiwa hiyo ni Ng'ombe?

Alafu kuna mizazi mingine kama imelogwa, ati kisa limesomesha basi linataka mtoto wake amhudumie yeye kuliko familia yake, umelogwa wewe mzazi, kama unataka kumpangia matumizi mwanao au Binti yako ungemuoa au kuolewa naye, pumbavu.

Watu wamejaa ubinafsi Sana!

Ngoja nipumzike!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
sijasoma yote, ila hongera sana hutajutia mkuu
 
Hapa hakuna ukabila, hata hivyo humu wengi tumezaliwa makabila chotara.
Ila ninachokuambia Wanawake WA Kaskazini (sio wote) Ila ni wengi ukilinganisha na jamii zingine, wapo very strong kwenye ishu za hustling
So unataka kusema wanaume tunaovutiwa na wanawake wa maeneo hayo ni kwasababu tunatafuta hustlers au tunakweda kwasababu ni wanawake wenye features nzuri za muonekano ambao unatupa stimu za kuwalala na kufurahia ujana huku tukitengeneza nao maisha?
 
Kila siku mada za wanawake wa Kaskazini
Mnawahusudu ndio maana mnawaongelea
Igweeeeee to Chagga Ladies out there[emoji7]
 
Wewe ni Mkristo?
Nikupe Aya zinazomtaja Mwanamke ambaye ni wife material au wewe ni muislam nikuonyeshe Wanawake ambao ni wife material kwenye Quran alafu uone Kati ya hao ni Mwanamke gani hakuwa na Pesa
Kwa sababu Moja ya vigezo vikuu vya wife material ni uchapakazi na uzalishaji Mali.

Sio hizo kazi za kufua na kuosha vyombo, tunazungumzia kazi za uzalishaji.

Sasa nijibu wewe ni Mkristo au muislam ili tuende Kwa reference uelewe vizuri, maan kwenye Mila na tamaduni zetu panakushinda.

Angali Wanawake wa Iringa, Mbeya, Kigoma, Moshi,Arusha uone jinsi walivyo heavy weight katik uchapakazi. Hiyo ni Sifa namba tatu Kati ya zile 10 za Mwanamke Strong
Wanioneshe.kwenye biblia kaka, ila wakati ukiwatafuta tuanze na Bikira Maria mama wa Yesu mke wa Yusufu fundi seremala.

Kwakuwa kuna wakati ulisema mama na mke wana wajibu sawa, basi ni wapi Bikira Maria alifanyakazi? tunafahamu Yusufu alikuwa akifanya kazi ya useremala na hata alisaidiwa na Yesu kazi hizo.

Usije ukasema tu wayahudi hawakuruhusu wanawake kufanyakazi. Bila kuadhiri imani za wadau humu, twende kwenye mjadala kaka, karibu
 
Unamanisha Mkoa gani sasa,Mikoa 3 IPO Kaskazini mwa Tanzania
1.Kaskazini upo Mkoa wa Mara pekee
2.Kaskazini mashariki-Arusha
3.Kaskazini Magharibi kuna Mkoa wa Kagera.
 
Unazungumzia hustling ila hamna tajiri pale top ten ...

Hamna mwanamke hustler hapa Tz wengi ni back ya wanaume zao na mali za urithi..

ukitaka hustling nenda vijijini kuanzia kutafuta kuni .

Halafu vibiashara za kupost vinguo online na kava za simu wengi wamefanya mwaka washarudi makwao sio biashara bali ni uchuuzi..
Inauzwa nguo na mwili uliovaa hiyo nguo. Ndio biashara za dada zetu huko Instagram na whatsApp status.

Anakufuata mdada inbox anakuambia umsave namba yake kwa ajili ya urafiki na kuview status. Ukiwa serious kidogo unakula kimasihara maisha yanaendelea.
 
Unazungumzia hustling ila hamna tajiri pale top ten ...

Hamna mwanamke hustler hapa Tz wengi ni back ya wanaume zao na mali za urithi..

ukitaka hustling nenda vijijini kuanzia kutafuta kuni .

Halafu vibiashara za kupost vinguo online na kava za simu wengi wamefanya mwaka washarudi makwao sio biashara bali ni uchuuzi..
Na hii ndio huwa inanifanya nihoji kwann wanakuwa wajuaji na kujifanya wanajua kutafuta ila ukija kupima maendeleo na mafanikio mwaka mzima unakuta efforts na fujo zote outcome yake ni equal to Zero yaani hakuna kitu katengeneza zaidi ya kupoteza muda tu.

Kuna binti hapo Moshi, alikuwa na fala wake m'moja hivi wakatiana mimba wakashindwana. Huyu binti akapitia wakati mgumu sana kuishi na yule jamaa sababu hakuwa mtu makini na familia so akawa anafikiria kutengana nae ila hajui aanzie wapi.

Akapata kakazi somewhere akaamua kusanuka apate sehemu ya kuishi mwenyewe, mtoto akampeleka kwa ndugu yake wa kike amsaidie kumlea.

Sasa baada ya kuanza haya maisha ya kuishi mwenyewe ndio akaanza yale matabia sasa ya wadada wa kichagga kujifanya wamezaliwa Smart kuliko wanawake wote Africa.

Demu alikuwa ana mambo mengi halafu akaanza kuwa muongo muongo mixer mtu wa matukio, WhatsApp yake haina last seen, ukimtext hujui kama amepata text au la.

Kuna siku aliniomba hela nikachelewa kumtumia akanimind balaa. Nikasema anyway ahadi ni deni wacha nimtumie tu. Kilichokuja kunizima kwa yule bi dada ni siku moja nimempigia simu, nikaona yupo dry sana namna anavyojibu, nikamuuliza mbona kama haupo sawa, akanambia yaani hata hapa hata tunavyoongea sikuelewi maana gesi, nikamtumia pesa anunue gesi apike.

Alipotea hakunicheki tena baada ya pale, nikaja wasiliana nae keshokutwa yake nikamwambia kwahiyo uliposhiba ukazimia, akanambia nilikuwa sina vocha nikamuunganisha kifurushi cha sms cha mwezi na kifurushi cha wiki cha data na muda wa maongezi, akajibu tu asante kisha akawa kimya.

Sikumtafuta, tena hadi siku mbili baadae nikampigia nipige nae story ananiambia kichwa hakipo sawa kabisa nikaona hiki ni kirungu kinafuata, nikaona ila wacha nimuulize. Akanambia sijui anashida ya 100,000 ila akipata hata 60,000 tu ataweza kusolve tatizo linalompa mawazo.

Nikamwambia ngoja nikupigie tena kuna jambo namalizia hapa. Nilipokata simu nikasema "matako yako kama ukiona simu yangu tena inaita kwako sijui iwaje" nikampotezea mazima.

Recently ananitafuta kwa sms ananiuliza mbona nipo kimya nimempotezea simtafuti. Namkwepa tu maana namuona ni wale wale wanawake wa kanda hiyo wao muda wote mazungumzo yao ni hela tu hakuna la maana lingine mtaongea as if hela zinachumwa kwenye miti.

Ufala ufala tu yaani.
 
Tatizo huwezi nipata.
Nimesema unaendesha Maisha yako, Sawa. Assume umekufa au umefukuzwa kazi, angalia Nani atawajibika na watoto wako 100% kama sio Mkeo.

Tatizo vijana WA siku hizi mnayachukulia mambo kibinafsi pasipokuangalia Watoto wenu na wajukuu wenu. Na ukishagusa Watoto na wajukuu jua tayari umeshataja Mwanamke.
Sasa Kama hukuchagua mwanamke Strong unategemea nini kitatokea Kwa Watoto au wajukuu wako.

Kaskazini Wanawake wabibi wanasomesha mpaka wajukuu zao wakiwapiga tough Watoto wao.
Bado hujaelewa Nini nazungumzia
Kwann katika hizi assumptions ni mwanaume tu ndie anakutwa na majanga kwan mwanamke hawezi kufa ghafla, hawezi patwa na magonjwa ambayo yatampa ulemavu wa kudumu ashindwe hata kunyanyua kidole.

Why ni wanaume tu ndio ambao huwa ni target ya hizi assumptions mbaya ambazo si lazima zitokee?
 
Back
Top Bottom