Kwanini ni lazima nioe Mwanamke wa Kaskazini?

hujawahi kubaguliwa siyo? Subiri siku yaja halafu urudi tena huku.

Nibaguliwe mara ngapi?
Maisha ni ubaguzi halisi ndio maana tupo tofauti.
Hayo mengine ni unafiki tuu wa Mwanadamu,
Mwanadamu ni mbinafsi by nature, ukishasema MTU ni mbinafsi ujue ushazungumzia ubaguzi
 

Robert Heriel 🔥🔥👊
 
Afadhali jamani watoto wetu wa kike wapate wachumba/waume wanaowazimia kama mleta uzi.Binti yangu anaambiwaga wewe "mpalestina" huwa kinaniuma sana na Mungu anawaona aisee.
Pole sana, wana ubabe fulani sio poa. Yaani kama wewe sio kidume ukasimama kiuwanaume hakika huwawezi. Ila mengi aliyosema mleta mada ni sahihi kabisa.

..huoni wakitaka kuwekwa hovyo yani, labda hawa wanaochipukia kwa sasa, ila wale wa marika tuliooa hawana mda na hizo mambo kivile.
 

Mbwa Mzee hafundishwi kuwinda.

Sijasema kuwa Hawana Tabia Mbaya, Mimi nimeeleza mazuri Yao yanayonifanya niwaoe, sio kwamba sijui mapungufu Yao.
 
Unakuta pisi kali inakupa mchezo wa maana usiku na inautamu balaa. Halafu ndio inakufokea dah unajikuta unakuwa mpole tu japo upate mzigo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huyo mwanamke anafuata malengo yangu malengo yake au malengo yetu.

Mimi kama nimeplan baada ya miaka mitano tuwe tumeshajenga nyumba mbili, tufungue duka la biashara na kumiliki hata IST moja then hiyo ndio kitu nitasimamia, yeye kama atataka tumiliki ghorofa sita, tuwe na milioni 200 kwenye account, nje tupaki VX na BMW na December twende Marangu kwa ndege tukifika tutembeze noti na kutatua shida ndogo ndogo za ukoo wake, huyo sio mwanamke kwangu huyo ni takataka.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
Ati kufungiwa Stop nimecheka kifala Sana.

Lazima mwanaume ujifunze Martial arts Mkuu . Vinginevyo baadhi ya Wanawake wakaskazini kama Tarime watatingisha kidevu hicho[emoji23][emoji23]
Sasa umeingia kwenye mahusiano ya kimapenzi au mahusiano ya Kijeshi na mgambo wa kulinda amani congo.
 
Na ikawe ivo mkuu, tuendelee kupendana ukabila haufai
Alichokiandika ni kweli kabisa Kuna Mama ni Mchaga yaani ni Mama wa rafiki yangu nakumbuka wakati nipo std 5 mpaka form two yule Mama alinipenda kwa sababu ya Upole, Ukweli na Uaminifu kuliko Mwanae wa kumzaa niliishi naye vizuri sana mpaka nilipohama Shule kwenda Dar siku naondoka yule Mama alitoa machozi na akaniambia nitakukumbuka na ninakupenda sana Manyanza. Nilijitahidi baada ya kumaliza form four nilienda kumsalimia alifurahi sana. Na nilimkuta maisha yake yamekuwa mazuri sana na Mume wake alikuwa ni Meneja kwenye shirika Fulani lakini bahati mbaya nikaanguka dhambini na mwanaye wa Kike alinimaindi lakini akanisamehe tu. Na siku narudi Dar alinunulia na nguo na Miaka kadhaa mbele nilipopata Kazi baada ya kumaliza chuo nilimtumia 500,000 na Mapazia ya Home Shopping Centre. Alifurahi sana. Kwa kifupi yule Mama ni mtu na ana utu na ni Mpambanaji sana. Anafuga Kuku , Ng'ombe na Nguruwe na likija suala la kuchapa kazi nilikuwa nachapa kazi kweli kweli. Mtazamo wa thread ya Jana ya Cc country Wide na wa Herbert kwenye hii thread umekuwa ni tofauti. Kwa kifupi kizazi cha Mabinti wa miaka ya 1990 mpaka 2000 ndio kinachochafua legacy ya Wanawake wa Kasikazini. Maana Kuna Demu wa Kasikazini alikimbia na jembe langu na akaacha kazi yenye Mshahara wa maana kisa Jamaa wa zamani alipata kazi nzuri huko UGHAIBUNI.
 
sijasoma yote, ila hongera sana hutajutia mkuu
 
Hapa hakuna ukabila, hata hivyo humu wengi tumezaliwa makabila chotara.
Ila ninachokuambia Wanawake WA Kaskazini (sio wote) Ila ni wengi ukilinganisha na jamii zingine, wapo very strong kwenye ishu za hustling
So unataka kusema wanaume tunaovutiwa na wanawake wa maeneo hayo ni kwasababu tunatafuta hustlers au tunakweda kwasababu ni wanawake wenye features nzuri za muonekano ambao unatupa stimu za kuwalala na kufurahia ujana huku tukitengeneza nao maisha?
 
Kila siku mada za wanawake wa Kaskazini
Mnawahusudu ndio maana mnawaongelea
Igweeeeee to Chagga Ladies out there[emoji7]
 
Wanioneshe.kwenye biblia kaka, ila wakati ukiwatafuta tuanze na Bikira Maria mama wa Yesu mke wa Yusufu fundi seremala.

Kwakuwa kuna wakati ulisema mama na mke wana wajibu sawa, basi ni wapi Bikira Maria alifanyakazi? tunafahamu Yusufu alikuwa akifanya kazi ya useremala na hata alisaidiwa na Yesu kazi hizo.

Usije ukasema tu wayahudi hawakuruhusu wanawake kufanyakazi. Bila kuadhiri imani za wadau humu, twende kwenye mjadala kaka, karibu
 
Unamanisha Mkoa gani sasa,Mikoa 3 IPO Kaskazini mwa Tanzania
1.Kaskazini upo Mkoa wa Mara pekee
2.Kaskazini mashariki-Arusha
3.Kaskazini Magharibi kuna Mkoa wa Kagera.
 
Inauzwa nguo na mwili uliovaa hiyo nguo. Ndio biashara za dada zetu huko Instagram na whatsApp status.

Anakufuata mdada inbox anakuambia umsave namba yake kwa ajili ya urafiki na kuview status. Ukiwa serious kidogo unakula kimasihara maisha yanaendelea.
 
Na hii ndio huwa inanifanya nihoji kwann wanakuwa wajuaji na kujifanya wanajua kutafuta ila ukija kupima maendeleo na mafanikio mwaka mzima unakuta efforts na fujo zote outcome yake ni equal to Zero yaani hakuna kitu katengeneza zaidi ya kupoteza muda tu.

Kuna binti hapo Moshi, alikuwa na fala wake m'moja hivi wakatiana mimba wakashindwana. Huyu binti akapitia wakati mgumu sana kuishi na yule jamaa sababu hakuwa mtu makini na familia so akawa anafikiria kutengana nae ila hajui aanzie wapi.

Akapata kakazi somewhere akaamua kusanuka apate sehemu ya kuishi mwenyewe, mtoto akampeleka kwa ndugu yake wa kike amsaidie kumlea.

Sasa baada ya kuanza haya maisha ya kuishi mwenyewe ndio akaanza yale matabia sasa ya wadada wa kichagga kujifanya wamezaliwa Smart kuliko wanawake wote Africa.

Demu alikuwa ana mambo mengi halafu akaanza kuwa muongo muongo mixer mtu wa matukio, WhatsApp yake haina last seen, ukimtext hujui kama amepata text au la.

Kuna siku aliniomba hela nikachelewa kumtumia akanimind balaa. Nikasema anyway ahadi ni deni wacha nimtumie tu. Kilichokuja kunizima kwa yule bi dada ni siku moja nimempigia simu, nikaona yupo dry sana namna anavyojibu, nikamuuliza mbona kama haupo sawa, akanambia yaani hata hapa hata tunavyoongea sikuelewi maana gesi, nikamtumia pesa anunue gesi apike.

Alipotea hakunicheki tena baada ya pale, nikaja wasiliana nae keshokutwa yake nikamwambia kwahiyo uliposhiba ukazimia, akanambia nilikuwa sina vocha nikamuunganisha kifurushi cha sms cha mwezi na kifurushi cha wiki cha data na muda wa maongezi, akajibu tu asante kisha akawa kimya.

Sikumtafuta, tena hadi siku mbili baadae nikampigia nipige nae story ananiambia kichwa hakipo sawa kabisa nikaona hiki ni kirungu kinafuata, nikaona ila wacha nimuulize. Akanambia sijui anashida ya 100,000 ila akipata hata 60,000 tu ataweza kusolve tatizo linalompa mawazo.

Nikamwambia ngoja nikupigie tena kuna jambo namalizia hapa. Nilipokata simu nikasema "matako yako kama ukiona simu yangu tena inaita kwako sijui iwaje" nikampotezea mazima.

Recently ananitafuta kwa sms ananiuliza mbona nipo kimya nimempotezea simtafuti. Namkwepa tu maana namuona ni wale wale wanawake wa kanda hiyo wao muda wote mazungumzo yao ni hela tu hakuna la maana lingine mtaongea as if hela zinachumwa kwenye miti.

Ufala ufala tu yaani.
 
Kwann katika hizi assumptions ni mwanaume tu ndie anakutwa na majanga kwan mwanamke hawezi kufa ghafla, hawezi patwa na magonjwa ambayo yatampa ulemavu wa kudumu ashindwe hata kunyanyua kidole.

Why ni wanaume tu ndio ambao huwa ni target ya hizi assumptions mbaya ambazo si lazima zitokee?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…