Kwanini ni lazima nioe Mwanamke wa Kaskazini?

Kwanini ni lazima nioe Mwanamke wa Kaskazini?

Shida karne hii unakuta tayari kuna muingiliano....labda sijui uende huko interior
 
Na hii ndio huwa inanifanya nihoji kwann wanakuwa wajuaji na kujifanya wanajua kutafuta ila ukija kupima maendeleo na mafanikio mwaka mzima unakuta efforts na fujo zote outcome yake ni equal to Zero yaani hakuna kitu katengeneza zaidi ya kupoteza muda tu.

Kuna binti hapo Moshi, alikuwa na fala wake m'moja hivi wakatiana mimba wakashindwana. Huyu binti akapitia wakati mgumu sana kuishi na yule jamaa sababu hakuwa mtu makini na familia so akawa anafikiria kutengana nae ila hajui aanzie wapi.

Akapata kakazi somewhere akaamua kusanuka apate sehemu ya kuishi mwenyewe, mtoto akampeleka kwa ndugu yake wa kike amsaidie kumlea.

Sasa baada ya kuanza haya maisha ya kuishi mwenyewe ndio akaanza yale matabia sasa ya wadada wa kichagga kujifanya wamezaliwa Smart kuliko wanawake wote Africa.

Demu alikuwa ana mambo mengi halafu akaanza kuwa muongo muongo mixer mtu wa matukio, WhatsApp yake haina last seen, ukimtext hujui kama amepata text au la.

Kuna siku aliniomba hela nikachelewa kumtumia akanimind balaa. Nikasema anyway ahadi ni deni wacha nimtumie tu. Kilichokuja kunizima kwa yule bi dada ni siku moja nimempigia simu, nikaona yupo dry sana namna anavyojibu, nikamuuliza mbona kama haupo sawa, akanambia yaani hata hapa hata tunavyoongea sikuelewi maana gesi, nikamtumia pesa anunue gesi apike.

Alipotea hakunicheki tena baada ya pale, nikaja wasiliana nae keshokutwa yake nikamwambia kwahiyo uliposhiba ukazimia, akanambia nilikuwa sina vocha nikamuunganisha kifurushi cha sms cha mwezi na kifurushi cha wiki cha data na muda wa maongezi, akajibu tu asante kisha akawa kimya.

Sikumtafuta, tena hadi siku mbili baadae nikampigia nipige nae story ananiambia kichwa hakipo sawa kabisa nikaona hiki ni kirungu kinafuata, nikaona ila wacha nimuulize. Akanambia sijui anashida ya 100,000 ila akipata hata 60,000 tu ataweza kusolve tatizo linalompa mawazo.

Nikamwambia ngoja nikupigie tena kuna jambo namalizia hapa. Nilipokata simu nikasema "matako yako kama ukiona simu yangu tena inaita kwako sijui iwaje" nikampotezea mazima.

Recently ananitafuta kwa sms ananiuliza mbona nipo kimya nimempotezea simtafuti. Namkwepa tu maana namuona ni wale wale wanawake wa kanda hiyo wao muda wote mazungumzo yao ni hela tu hakuna la maana lingine mtaongea as if hela zinachumwa kwenye miti.

Ufala ufala tu yaani.
Wabongo wengi wanapenda mbwembwe hapa ofisi kwangu wapo baadhi wanakelele sana eti mi mchaga bhana😂😂 Biashara kweny damu ila nakuambia kuna watu wapo kimya wanapiga business...

Kuna janja mmoja nilimshtukia mara anapost magari mara duka la vinjwaji ila kuna siku eti anataka kunikopa laki 4 ni pesa ndogo na mshahara ni mkubwa sana kwa pesa hiyo na ni siku chache tu baada ya kupokea mshahara sasa kama sio utapeli ni nn? kelele kibao then unakosa akiba au anataka kunitapeli.


Eti hustling ni zaidi ya utoto wa wanawake tu kwa vile hata awe 35 years still ana utoto ila wanaume wanahustling ile real na wapo kimya .
 
Inauzwa nguo na mwili uliovaa hiyo nguo. Ndio biashara za dada zetu huko Instagram na whatsApp status.

Anakufuata mdada inbox anakuambia umsave namba yake kwa ajili ya urafiki na kuview status. Ukiwa serious kidogo unakula kimasihara maisha yanaendelea.
😂😂😂
 
Unajua maisha ni mifumo. Na mifumo huwa ina watu maalumu ambao hutegemea kushika nafasi zao kikamilifu.

Unaweza kuwa na house girl ila akayafanya vema sana majukumu ya mkeo kiasi kwamba ndani ya moyo wako unaona kabisa hapa hata huyu mwanamke aondoke hapa ndani maisha still yataenda tu bila shida.

Hiki ndicho ambacho sisi tunaongelea, mwanamke kufit profile ya mwanaume anaeishi nae sio kuishi anavyoona yeye anataka au kwa kufuata mila na desturi za jamii yake.

Sasa wanawake wakanda hizo wengi wanaklemisha sana maisha na kuhisi kuwa mfumo wa kutafuta hela masaa 24 kila mtu anaupokea kama wao. Pesa haitafutwi hivyo hadi ikupe ukichaa.
Hapa una hoja nzuri. Inshu mwanaume anatakiwa akae ktk nafasi yake kama kichwa cha familia. Kila siku tunaona matukio ya wanandoa kufumaniana, kuuuana, kujeruhiana etc.
Haya matukio hutokea sehemu mbalimbali ktk nchi yetu. Haimanishi kwakuwa kaskazini ndo mnapasema basi hayo matukio yangeongoza kutokea huko.

Mwaka jana wilaya ya Temeke ilitoa ripoti ya talaka kuwa kulikuwa na ndoa 3000+ zimevunjika. Lakini hapa hatujadili suala la kabila. Sitetei kuwa kaskazini hakuna matukio hapana ila nataka mfanye haki na kwa makabila mengine pia isije ikaleta kutengwa kwa wanawake wa jamii za kaskazini kumbuka mitandao ni sehemu ya kubadilisha mtazamo wa jamii. Hofu tusitumie vibaya tuje kujilaumu baadaye.
 
Habari za Leo.

Kwangu ni lazima kuoa Mwanamke wa Kaskazini au jamii zinazokaribiana Mila, desturi, falsafa na mitizamo kama ya Wanawake WA Kaskazini. Kuoa Mwanamke wa Kaskazini kwangu Sio Optional, bali ni lazima. Hii itabaki kuwa hivyo ilivyo.

Sio kila mtu atakayetaka kujua sababu ya Mimi kuwa na uamuzi huo, kwani ni uamuzi binafsi unaohusu Maisha yangu mwenyewe lakini ninauhakika wapo watakaotaka kujua sababu ya Mimi kuwa na Uamuzi huo.

Wanawake WA Kaskazini ni Wanawake wote wenye tabia halisi za Mwanamke wa shoka bila kujali amezaliwa Iringa, Kigoma, mtwara, Morogoro, Mwanza, Moshi, Musoma .n.k.

Zifuatazo ni sababu za Kwa nini Taikon lazima Aoe Mwanamke wa Kaskazini;

1. Wanapenda Mali.
Kwa jamii zingine huona Jambo Hilo katika mtazamo Hasi lakini Kwa wanaume Strong tunachukulia Jambo hilo kama Motivation.
Mwanamke lazima apende Mali, ili kuzalisha Vijana wachapakazi na sio vijana wavivu na wazembe wazembe.

Ili mwanaume uheshimike Mali ni moja ya vigezo vya kumfanya mwanaume aonekane yupo serious na Maisha. Fanya kazi Kwa bidii na juhudi yenye Akili.
Ukiona eneo hilo limekushinda Hama tafuta sehemu nyingine, sio unakaa sehemu moja kama Mwanamke.
Wanawake WA Kaskazini kumwambia unaenda kutafuta Maisha nchi za mbali yeye haoni shida, au kumwambia muondoke wote muhame mwende Mikoa ya mbali kwao sio tatizo ili mradi umwambie kuna mchongo wa kutafuta Maisha.

Hii ni tofauti na Baadhi ya Wanawake WA jamii zingine, ukiwambia mhame mwende mbali watawaza sijui wazazi sijui ndugu kwamba watakuwa mbali na nyumbani.

Kupenda Mali kunazalisha Vijana wawe wachapakazi na Risk taker,

2. Wanakiu ya Maendeleo Kwa Watoto wao.
Wanawake WA Kaskazini hata umtelekezee mtoto hapo ninakuhakikishia lazima atasoma kivyovyote vile bila kutegemea Pesa yako.
Wanawake WA Kaskazini wengi wao ndio wazalishaji hasa WA hizi kazi ndogondogo Kam umachinga WA nguo, kuuza mitumba, kulima vibarua kwenye mashamba, n.k.
Vijana wengi wa Kaskazini wamesomeshwa na Mama zao.
Wababa wanasimamia shoo kubwakubwa kama ujenzi wa nyumba, ununuzi wa viwanja na utanuzi wa Ngome na miradi.

Sasa ni Mwanaume gani Strong ambaye hatataka kuoa Mwanamke wa Kaskazini ikiwa anauhakika hata asipokuwepo Watoto wake wataishi vizuri, sidhani kama kuna mwanaume wa hivyo.

3. Hawapendi wanaume Cheaters.
Ukitaka uonje joto la Jiwe basi OA Mwanamke wa Kaskazini alafu mfanyie mambo ya kiduwanzi, mcheat mara Kwa mara uone nini kitatokea.
Utawahadithia wenzako na utakuwa fundisho Kwa wengine. Kwanza lazima utoke ndani ya nyumba kivyovyote iwe Kwa Amani au Kwa Shari.
Wale wanaume Werevu wakishaona wametosheka na kukinaiwa na Wake zao huwaachia Nyumba(Mji) na kuendelea na Maisha mengine. Lakini hawapeani Talaka. Hiyo mbinu inatumiwa na wanaume wajanja.

Lakini wale wanaume wajinga hugangamala hapohapo na ndipo ubaya wa Wanawake WA Kaskazini utakapoonekana. Hakuna rangi ambayo hautaacha kuiona.

4. Huwezi kuwatapeli Mali Kama mlichuma Wote.
Kwanza hakuna kazi ngumu kama kumtoa Mwanamke wa Kaskazini ndani ya nyumba hasa kama mmejenga wote. Ni ngumu Sana. Kesi hiyo itasimamiwa vilivyo na atapata uungwaji mkono na Ndugu zake Kwa namna yoyote Ile.
Hii inamaanisha unapooa Mwanamke wa Kaskazini lazima ujue mlango wa kutokea endapo ikitokea mkiachana. Kwani wengi wao wana-backup ya Kufa mtu Kutokana na umoja waliokuwa nao.
Hivyo kama Mwanaume kwenu ukoo wenu hauna umoja kila MTU kivyake inaweza kukugharimu.

Hii inahamasisha Vijana kuunganisha nguvu na Ndugu zao. Sio kijana ukishaoa tuu unakata mawasiliano na Ndugu zako unashindwa hata kuwainua, ninakuhakikishia inaweza ikakusumbua Huko Mbele.

5. Ni Wakali na hawadekezi Watoto.
Labda ninashindwa kueleza Jambo hili vizuri. Lakini Wamama wa Kaskazini ni Wakali Kwa Watoto kuliko Wababa. Wanaume ni Wakali linapokuja suala la utafutaji na mipaka ya Ardhi lakini kwenye malezi wamama wameshindikana.

6. Ni washamba Kwa Mambo ya Kijingajinga yasiyoingiza Pesa.
Wanawake WA Kaskazini ni washamba Kwa mambo yasiyo na tija, mfano sijui udaku wa masupastaa, sijui kukata mauno au kucheza, sijui kuunganisha madanga, Kwa kweli Kwa hayo mambo NI washamba, wengi hawajui na hawafuatilii hivyo vitu.

Wao wanachojua ni Mambo ya Pesa, sijui Vikoba, Michezo, Brac, kuuza Kwa kukopeshana, ujenzi, usomeshaji wa watoto, biashara n.k. hayo ndio mambo Yao.

7. Wengi Hawana Umalaya.
Umalaya ni tabia mara nyingi inayochangiwa na Mwanamke kuwa tegemezi, utegemezi unaleta tamaa alafu Pesa hauna.
Utachunguza mwenyewe Wanawake wenye Tabia za kimalaya wengi wanatoka jamii tegemezi ambazo wao kila Pesa wanamtegemea mwanaume.
Pesa ya Kodi mwanaume,
Pesa ya chakula mwanaume,
Pesa ya kusomeshea mtoto mwanaume,
Pesa ya mavazi mwanaume
Pesa ya kila kitu mwanaume alafu kazi huna Mwanamke ataachaje kuwa Malaya.
Wanawake wengi WA Kaskazini na jamii zinazofanana NAO ni wachakarikaji, wanajua Pesa inavyotafutwa Kwa kazi ndogondogo na biashara za Kati.
Mwanaume akitafutwa ni kwaajili ya kufanya Maisha.
Weka niweke.

8. Hawana unyenyekevu Kwa Wanaume wapumbavu.
Wanawake WA Kaskazini wamefundishwa kujitambua, Haki zao. Mheshimu atakuheshimu, mpende atakupenda, mshirkishe atakushirikisha. Hawana mambo ya unafiki.
Wanawake WA Kaskazini kwenye hii nchi ndio wanaoongoza Kwa kuhonga Vijana waaminifu. Yaani ukitaka kwenda naye Sawa basi Mpe Haki zake naye akupe Haki zako.

Tabia hiyo inachukuliwa na wanaume dhaifu kama ujeuri, kiburi na kutokuwa na heshima. Jambo ambalo sio Sahihi.
Mwanamke wa Kaskazini na jamii zinazofanana nayo hawezi kukuheshimu kama Mume wake ikiwa kuna mambo unapuyanga, yaani ufanye uhuni na umalaya wa kujirudiarudia alafu utegemee heshima. Hizo ni dharau kubwa.

Sisi kama Kaka zao na Baba zao tumewafundisha wasivumilie hiyo Hali endapo ikijitokeza Kwa kujirudiarudia mara Kwa mara. Ndio maana tunawafanya wajitegemee kiuchumi zaidi ili wasinyanyasike na kunyanyaswa na wanaume wendawazimu.

Hakuna mwenye Haki ya kufanya uhalifu au uovu Kwa Mwenzake iwe Mwanamke au Mwanaume. Mimi kuwa mume wa Fulani sio kigezo cha kumpiga au kumrudia Usiku WA manane nikiwa nimelewa, hiyo hauvumiliki, na ninachowapendea Wanawake WA Kaskazini hawatakukopesha watakujibu Kwa nguvu zote.
Aidha muachane au ubadilike. Na mkiachana mtasomana kwenye mgawanyo wa Mali na kuhudumia Watoto.

Kama ni MTU mwenye Tabia za umungu mtu sikushauri ukaoe Kaskazini, kama ni Mwanaume usiyependa HAKI basi Kaskazini sio sehemu sahihi kwako.
Mnaweeza Anza vizuri hasa kama unamali au unavikazi kazi vyenye kipato lakini ninakuhakikishia Baada ya miaka 20 picha litaanza kugeuka, hapo Watoto wamekua ni muda wa kujibu mapigo.

Wanawake WA Kaskazini wengi huonekana ni Feminist Kutokana na Ile Hali wanayokabiliana na uonevu na unyanyasaji wa baadhi ya wanaume wajingawajinga.

Unapomuoa Mkeo elewa kuwa huyo ni Msaidizi wako, mnasaidizana majukumu ya kimaisha na sio mmoja kumfanya mtumwa mwingine. Mwanaume asiwe mtumwa wa Mwanamke, pia Mwanamke asiwe mtumwa wa Mwanaume. Wote muwe kitu kimoja. Mnapokabiliana na mambo yenu yawekeni bayana mjue mnayatatuaje,

Ugumu unatoka wapi?
Wengi hujikuta katika ubinafsi ndio maana migogoro haiishi.
Mfano Mwanamke anazalisha laki tano kwa mwezi, mwanaume naye laki tano.
Hiyo Pesa Kwa nini msiiweke pamoja kisha muipangie matumizi pamoja?
Au mmoja anapokea laki tatu mwingine laki Saba. Mnaona shida gani kuunganisha hizo Pesa.
Kama ni kusaidia nyumbani si msaidie, mnaona shida gani?
Semeni Kila mwezi elfu 50 itaenda familia ya MKE, elfu 50 itaenda familia ya Mme. Jumla ni laki moja itatengwa Kwa Pesa ya Wazazi.

Sasa mkishaanza kuleta mambo ya mzazi wangu, mzazi wangu sijui kanisomesha sijui kanizaa, kwani Nani hakuzaliwa? Kwani Nani hakusomeshwa, sijui Mimi nimekuoa nimekutolea Mahari hiyo Mahari ndio nimemalizana na kwenu, hivi wewe ni Kichwa? Mahari ya milioni mbili au hata milioni 10 ndio umemalizana uliambiwa hiyo ni Ng'ombe?

Alafu kuna mizazi mingine kama imelogwa, ati kisa limesomesha basi linataka mtoto wake amhudumie yeye kuliko familia yake, umelogwa wewe mzazi, kama unataka kumpangia matumizi mwanao au Binti yako ungemuoa au kuolewa naye, pumbavu.

Watu wamejaa ubinafsi Sana!

Ngoja nipumzike!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kumbe taikon hujaoa, ?
 
Wanawake wa kaskazini? Bora ninyamaze tu. Hasa Wameru.

Nimekaa kwenye mahusiano na Mwanamke wa Kimeru kwa Mda wa Miaka mi tano. Ila Itoshe tu kusema nilijifunza mengi, na sitokuja kurudia kua na Mwanamke wa huko hata aweje.
 
Yote kwa yote!
Wanaume WEAK hawapendi
Kuoa ladies ambao wana challenge, wanahoji, wanaleta arguments na mawazo mbadala!

Sema kila mtu ashinde mechi zake!
 
Na hii ndio huwa inanifanya nihoji kwann wanakuwa wajuaji na kujifanya wanajua kutafuta ila ukija kupima maendeleo na mafanikio mwaka mzima unakuta efforts na fujo zote outcome yake ni equal to Zero yaani hakuna kitu katengeneza zaidi ya kupoteza muda tu.

Kuna binti hapo Moshi, alikuwa na fala wake m'moja hivi wakatiana mimba wakashindwana. Huyu binti akapitia wakati mgumu sana kuishi na yule jamaa sababu hakuwa mtu makini na familia so akawa anafikiria kutengana nae ila hajui aanzie wapi.

Akapata kakazi somewhere akaamua kusanuka apate sehemu ya kuishi mwenyewe, mtoto akampeleka kwa ndugu yake wa kike amsaidie kumlea.

Sasa baada ya kuanza haya maisha ya kuishi mwenyewe ndio akaanza yale matabia sasa ya wadada wa kichagga kujifanya wamezaliwa Smart kuliko wanawake wote Africa.

Demu alikuwa ana mambo mengi halafu akaanza kuwa muongo muongo mixer mtu wa matukio, WhatsApp yake haina last seen, ukimtext hujui kama amepata text au la.

Kuna siku aliniomba hela nikachelewa kumtumia akanimind balaa. Nikasema anyway ahadi ni deni wacha nimtumie tu. Kilichokuja kunizima kwa yule bi dada ni siku moja nimempigia simu, nikaona yupo dry sana namna anavyojibu, nikamuuliza mbona kama haupo sawa, akanambia yaani hata hapa hata tunavyoongea sikuelewi maana gesi, nikamtumia pesa anunue gesi apike.

Alipotea hakunicheki tena baada ya pale, nikaja wasiliana nae keshokutwa yake nikamwambia kwahiyo uliposhiba ukazimia, akanambia nilikuwa sina vocha nikamuunganisha kifurushi cha sms cha mwezi na kifurushi cha wiki cha data na muda wa maongezi, akajibu tu asante kisha akawa kimya.

Sikumtafuta, tena hadi siku mbili baadae nikampigia nipige nae story ananiambia kichwa hakipo sawa kabisa nikaona hiki ni kirungu kinafuata, nikaona ila wacha nimuulize. Akanambia sijui anashida ya 100,000 ila akipata hata 60,000 tu ataweza kusolve tatizo linalompa mawazo.

Nikamwambia ngoja nikupigie tena kuna jambo namalizia hapa. Nilipokata simu nikasema "matako yako kama ukiona simu yangu tena inaita kwako sijui iwaje" nikampotezea mazima.

Recently ananitafuta kwa sms ananiuliza mbona nipo kimya nimempotezea simtafuti. Namkwepa tu maana namuona ni wale wale wanawake wa kanda hiyo wao muda wote mazungumzo yao ni hela tu hakuna la maana lingine mtaongea as if hela zinachumwa kwenye miti.

Ufala ufala tu yaani.
Aisee sasa nimeelewa. Pole sana. Ndiyo maana tunasema siyo wote wako hivyo unaweza ukampata wa huko kaskazini na ukaenjoy maisha. Huyo alikuwa ana element za umalaya.

Na kwa wanawake nafkiri akiwa hakutaki Cha kwanza anachofikiria ni kukupiga virugu ili umuache.
 
Yote kwa yote!
Wanaume WEAK hawapendi
Kuoa ladies ambao wana challenge, wanahoji, wanaleta arguments na mawazo mbadala!

Sema kila mtu ashinde mechi zake!
Kati ya madem 6 ambao nilikua nao kwenye mahusiano kwa nyakati tofauti kabla sijaoa 4 ni wachaga na wote wamelelewa na single maza baba zao walishakufaga. Jiulize!
 
Wanawake wa kaskazini? Bora ninyamaze tu. Hasa Wameru.

Nimekaa kwenye mahusiano na Mwanamke wa Kimeru kwa Mda wa Miaka mi tano. Ila Itoshe tu kusema nilijifunza mengi, na sitokuja kurudia kua na Mwanamke wa huko hata aweje.

Tupe short story Mkuu
 
Alichokiandika ni kweli kabisa Kuna Mama ni Mchaga yaani ni Mama wa rafiki yangu nakumbuka wakati nipo std 5 mpaka form two yule Mama alinipenda kwa sababu ya Upole, Ukweli na Uaminifu kuliko Mwanae wa kumzaa niliishi naye vizuri sana mpaka nilipohama Shule kwenda Dar siku naondoka yule Mama alitoa machozi na akaniambia nitakukumbuka na ninakupenda sana Manyanza. Nilijitahidi baada ya kumaliza form four nilienda kumsalimia alifurahi sana. Na nilimkuta maisha yake yamekuwa mazuri sana na Mume wake alikuwa ni Meneja kwenye shirika Fulani lakini bahati mbaya nikaanguka dhambini na mwanaye wa Kike alinimaindi lakini akanisamehe tu. Na siku narudi Dar alinunulia na nguo na Miaka kadhaa mbele nilipopata Kazi baada ya kumaliza chuo nilimtumia 500,000 na Mapazia ya Home Shopping Centre. Alifurahi sana. Kwa kifupi yule Mama ni mtu na ana utu na ni Mpambanaji sana. Anafuga Kuku , Ng'ombe na Nguruwe na likija suala la kuchapa kazi nilikuwa nachapa kazi kweli kweli. Mtazamo wa thread ya Jana ya Cc country Wide na wa Herbert kwenye hii thread umekuwa ni tofauti. Kwa kifupi kizazi cha Mabinti wa miaka ya 1990 mpaka 2000 ndio kinachochafua legacy ya Wanawake wa Kasikazini. Maana Kuna Demu wa Kasikazini alikimbia na jembe langu na akaacha kazi yenye Mshahara wa maana kisa Jamaa wa zamani alipata kazi nzuri huko UGHAIBUNI.
Yeah sure
 
nothing else to contribute in this thread.
Just sit in back stage have some nice weed, 🚬🚬. listen to amapiano 🎵


.......Kush master......
 
Maana Kuna Demu wa Kasikazini alikimbia na jembe langu na akaacha kazi yenye Mshahara wa maana kisa Jamaa wa zamani alipata kazi nzuri huko UGHAIBUNI.
Hapo hapo unang'ata hapo hapo inapuliza, sawa mkuu Manyanza nimekupata hio ni ipo kwenye damu sio maigizo
 
Back
Top Bottom