Kwanini nyumba yako unaiita "kakibanda kangu"? Mungu hapendi kujishusha sana. Having too much humility is self destructive

Kwanini nyumba yako unaiita "kakibanda kangu"? Mungu hapendi kujishusha sana. Having too much humility is self destructive

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Sio kila siku tunapaswa kuandika, kusoma na kujadili makala zinazohusiana na masuala ya kizungu kama Cold War, jeshi na ujasusi wa KGB, CIA na Mossad. Leo ngoja tujadili kidogo masuala ya kimaisha katika jamii zetu hizi tunamoishi.

Ndugu zangu watanzania jifunzeni kujishusha lakini isiwe too much. Mungu hapendi mjishushe sana. Having too much humility is self destructive;

Unakuta mtu alikuwa anaishi katika nyumba ya kupanga vyumba viwili chumba na sebule, lakini kwa bahati nzuri akajinyima kisha kwa uwezo wa Mungu akajenga nyumba yake self-contained ya vyumba vitatu vya kulala.

Siku ama weeks kadhaa baada ya kuhamia unasema ngoja niende nikamtembelee ndugu, jamaa au rafiki yangu nifahamu anapokaa. Baada ya kufika na kusalimiana anakukaribisha ndani kisha anakwambia "karibu, haka ndio kakibanda kangu najifichamo na kafamilia kangu, si unajua tena ujenzi wa kimasikini"

Kwanini nyumba yako nzuri Mungu aliyokubariki uiite kakibanda? Au baadhi ya watu wanafikiri huko ndio kujishusha kwenyewe na ndio uungwana? Why don't you feel proud of what God blessed you with? Au haujui kuwa hata vinyonge havitaenda Mbinguni. Mtu amekuja kukutembelea mwambie kwa kujiamini kwamba, "hii ndio nyumba yangu. Nimeijenga mpaka stage hii ila Mungu akinijalia nitaimalizia taratibu tarabitu kwa maana pesa ngumu sana siku hizi"

Au unakutana na dada classmate wako wa secondary school na ulisikia aliolewa punde tu baada ya kumaliza shule. Unamuuliza "hongera Fatuma ninasikia uliolewa na fulani na umebarikiwa mtoto mmoja" utamsikia atakavyokujibu kwa kinyonge "kuolewa wapi kaka yangu, nipo tu ninasogeza naye maisha, si unajua tena mambo ya sogea tukae"

What the hell is "Sogea tukae"? Hiyo ndio ndoa yako ndugu yangu ambayo Mungu ameona inafaa uwepo mpaka wakati huo. Kuwa na shukrani kwa mume/mke uliyenaye na usimuite tena SOGEA TUKAE. Kwani kuna akina dada/kaka wangapi wanatamani wangekuwa katika ndoa ila wameshindwa kwa sababu mbalimbali?

A thankful heart is one that is grateful and appreciative of who God is and the life He has given them despite the storms of life. I have learned that cultivating a thankful heart is a choice and it requires our intentional effort in achieving it.

Having too much humility is self destructive. Humility has to be practiced with care. Humility requires boundaries.

Watanzania msipende kujiweka kinyongenyonge na kujishusha saana. Jivunie kile ambacho Mungu amekubariki kwa wakati huo huku ukizidi kupambana ili usonge mbele zaidi.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Wewe na familia yako kura zenu mkimpa msaliti wa Nchi haitaathiri kitu kwa sababu Dr Magufuli ni kipenzi cha Watanzania na tutampigia kura kwa 98% Vijana wachache wa Chadema mwaka huu mtajiua sana.
 
Watu wanasema kibada ili kukidhi haja ya walimwengu, kwani akisema nyumba yangu atashabuliwa kwa maneno na kejeli utasikia dah si kwamajivuno hayo kijumba chenyewe chumba kimoja ila utasikia nyumba yangu n.k hivo hatuna jince lazima tujishushe ili watu walidhike
 
Watu wanasema kibada ili kukidhi haja ya walimwengu, kwani akisema nyumba yangu atashabuliwa kwa maneno na kejeli utasikia dah si kwamajivuno hayo kijumba chenyewe chumba kimoja ila utasikia nyumba yangu n.k
Sawa mkuu...
 
Cha msingi mtu aite nyumba yake kadri apendavyo maana ni yake. Na kusema anenavyo mtu ndivyo atakavyokuwa ni uongo, ukitaka kuamini jinenee kuwa wewe ni tajiri wa Afrika then baada ya miaka kumi utajiona
Sawa mkuu
 
Shida sio kujishusha maana kuna watu wana midomo michafu sana isitoshe hatulingani uwezo.
Hivi ni mara ngapi watu wamekuja kuposti wanauza nyumba zao humu wakaishia kupata response za kejeli kama "We unauza nyumba au kibanda kwenye shamba?"...."Hapo sijaona nyumba zaidi ya kiwanja kitupu"...."Kuwa serious ukiongelea nyumba, hilo kwangu ni banda la mbwa tu" hizi ndio aina za member humu ambao ndio wabongo hao.

Kuepukana na dharau hizi mtu anai undervalue nyumba yake ili kuwafunga midomo kijanja hawa walimwengu.
 
Shida sio kujishusha maana kuna watu wana midomo michafu sana isitoshe hatulingani uwezo.
Hivi ni mara ngapi watu wamekuja kuposti wanauza nyumba zao humu wakaishia kupata response za kejeli kama "We unauza nyumba au kibanda kwenye shamba?"...."Hapo sijaona nyumba zaidi ya kiwanja kitupu"...."Kuwa serious ukiongelea nyumba, hilo kwangu ni banda la mbwa tu" hizi ndio aina za member humu ambao ndio wabongo hao.
Ninadhani kusimamia kilicho sahihi ndio suala la msingi zaidi badala ya kufuata wakisemacho watu...
 
Back
Top Bottom