Kwanini Serikali inawabagua walimu wenye shahada kwenye ajira?

Kwanini Serikali inawabagua walimu wenye shahada kwenye ajira?

Kuna kitu hakipo sawa kwenye ajira za walimu.

Kwenye kila kibali cha ajira kinachotoka idadi ya walimu wenye shahada wapatao fursa ya kuajiriwa serikalini huwa ni ndogo sana kulinganisha na walimu wa ngazi zingine za kielimu kama vile cheti na diploma.

Kielelezo kizuri ni ajira zilizotoka juzi ukizichunguza kwa makini utakubaliana na hiki ninachokisema.

Kwani katika hizo ajira, wenye shahada walioajiriwa hawafiki hata robo ya waajiriwa wote(wapo chini ya 1500 kati ya 8000).

Tukumbuke asilimia kubwa ya walimu hawa wamesomeshwa na serikali hivyo wanadaiwa na bodi ya mikopo(HESLB). Lakini cha kushangaza serikali ni kama inatoa kipaumbele kidogo kwa wao kuajiriwa.

Je, ni kipi hasa kinafanya walimu hao waajiriwe kwa uchache kuliko walimu wengine?

Je, watalipaje madeni yao ya mikopo kama serikali itaendelea kuwaacha mitaani?
Nafikiri itakuwa no issue ya mishahara.Nafikiri nimeeleweka,kuhusu mikopo watalipaje Hilo tuliachie watoa ajira.
 
Wenye degree mna uwezo mkubwa wa kujiajiri...(in Ndugai's voice)

Nasema uwongo ndugu zangu?
Umesema uwongo kabisa, hebu angalia pale mjengoni karibia asilimia 80 wana degree na wamegoma kujiajiri na kuamua kufukuzia milioni 12 kwa mwezi. Kiufupi wasomi ni waoga sana wa maisha...
 
Sahiz nasikia wanasema wenye Masters ndio wanafaa kufundisha advance
Siyo unavyosikia, ndivyo dunia inavyotaka. Primary ifundishwe na diploma na some degree holders. Sekondari degree wachache na master's wengi. University Dr na Profs.... Enzi zetu tukisoma Old Moshi kulikuwa na walimu wa kujitolea wazungu from Urusi na Marekani, walikuwa wakifundisha hasa masomo ya sayansi, yaani wote walikuwa na degree ya kwanza na Masters, enzi hizo....
 
Usilaumu sana, serikali
inaajiri kulingana na;

1. Uhitaji.
2. Bajeti iliyopo.
Hakuna uhitaji wa walimu?? Bajeti mbona tunanunua ndege na kujenga miradi kwa cash money? Sema elimu haijapewa priority coz viongozi na wapanga hiyo mipango watoto wao hawasomi kwenye hizo shule so they don't care....
 
HAPPY NEW YEAR 2021
 
Tatzo hela, sio serikalini tu hata private wanapendelea watu wa stashahada
 
Hakuna uhitaji wa walimu?? Bajeti mbona tunanunua ndege na kujenga miradi kwa cash money? Sema elimu haijapewa priority coz viongozi na wapanga hiyo mipango watoto wao hawasomi kwenye hizo shule so they don't care....
Unaelewa maana ya uhitaji&bajeti?
Je,mambo mengine yasimame,ili serikali iajiri tu?
Niliwahi kumshauri mtu 2014
asisome ualimu kwa 7bu kuna uhakika wa ajira,kwani ifikapo miaka ya 2016 kuendelea hakutakuwa
na demand kubwa ya walimu
hasa Sekondari.
Huyo ndugu amenishukuru.
 
Fanya uchunguzi.
Nimefanya nimegundua walimu wa cheti na diploma wanaandaliwa/wana fundishwa kuwa waoga na walimu wa shahada wanaandaliwa/ wana fundishwa ujasiri na kujiamini. Kama niko wrong nisahihishe mkuu
 
Nimefanya nimegundua walimu wa cheti na diploma wanaandaliwa/wana fundishwa kuwa waoga na walimu wa shahada wanaandaliwa/ wana fundishwa ujasiri na kujiamini. Kama niko wrong nisahihishe mkuu
Imekaa sawa sawa.
 
Tofauti ipo umeambiwa.
Madeni ni ya mtu binafsi.
Ndio sikatai tofauti ipo lakini ni kidogo wewe ambacho huelewi ni nini mkuu?

Nyie ndio mnafanya walimu waendelee kulipwa maslahi duni kwasababu ya kutaka kuaminisha jamii kwamba walimu wenye shahada wanalipwa mishahara mikubwa wakati sivyo.
 
Hapana mkuu sio kweli

mwalimu mpya mwenye shahada anaanza na ngazi ya mshahara ya daraja D sawa na 716,000(basic). Baada ya deductions zote kuanzia CWT, NHIF, HESLB nakadhalika karibia nusu ya mshahara wote hurudi serikalini na hivyo kufanya mishahara yao kukaribiana kabisa na mishahara ya walimu wenye diploma. Kama ni kutofautiana wanatofautiana kwa kiasi kidogo sana kisichozidi 50,000.
Sasa huo mshahara mkubwa unaosema ni upi mkuu?
  • TGTS B1 = 419,000/-
  • TGTS C1 = 530,000/-
  • TGTS D1 = 716,000/-
  • TGTS E1 = 940,000/-
  • TGTS F1 = 1,235,000/-
  • TGTS G1 = 1,600,000/-
  • TGTS H1 = 2,091,000/-
  • TGTS I = 2,810,000/-
Daraja b cheti, c diploma , d degree , DARAJA E 'na kuendelea ni upandaji wa madaraja
 
Haya hayana maana. Lete figures za take home tuthaminishe tuone kama viwango vinatofautiana kwa kiasi mnachotaka kutuaminisha.
 
Unaelewa maana ya uhitaji&bajeti?
Je,mambo mengine yasimame,ili serikali iajiri tu?
Niliwahi kumshauri mtu 2014
asisome ualimu kwa 7bu kuna uhakika wa ajira,kwani ifikapo miaka ya 2016 kuendelea hakutakuwa
na demand kubwa ya walimu
hasa Sekondari.
Huyo ndugu amenishukuru.
So unataka kutuambia demand ya walimu nchini kulingana na idadi ya shule zilizopo na wanafunzi imekuwa met siyo? Unafahamu darasa linatakiwa kuwa na wanafunzi wangapi and hence idadi ya walikuwa ili kupata elimu bora? Sasa madarasa na madawati kwa wanaoenda form one this January hakuna, unalijua hilo? Unafahamu kwamba kuna shule darasa moja lina wanafunzi 80 mpaka mia?

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom