Kwanini Tanzania hakuna daily briefing juu ya Corona virus pandemic?

Mkuu Mystery, kwanza naunga mkono hoja.
Pili kwa ruhusa yako, naomba kutumia hoja za bandiko lako hili kama mbegu ya kuoteshea bandiko langu fulani.

Enzi za zamani, mambo ya kutoa habari kwa upande wa serikali ilikuwa iko huru kutoa habari au kutotoa, ikijisikia kutoa habari, inatoa, ikijisikia kutotoa habari, haitoi na hakuna yoyote mwenye mamlaka ya kuiuliza.

Lakini kuanzia mwaka 2016, Tanzania tumepitisha sheria ya haki ya kupata habari, the right to information act, ambapo sasa kupata habari ni haki, sio favours, serikali inawajibika kutoa habari za kweli kwa wananchi, hiki kinachoendelea sasa kwenye utoaji wa habari za maendeleo ya ugonjwa wa Corona, ni kinyume cha sheria. Watanzania wana haki ya kupata habari, unless rais atangaze hali ya hatari, sheria zote na haki zote zinasimama!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…