Kwanini Tanzania hakuna daily briefing juu ya Corona virus pandemic?

Kwanini Tanzania hakuna daily briefing juu ya Corona virus pandemic?

Jamaa akiongoza nchi kwa rimoti from Jamhuri ya watu wa chato
 
Siri ni sehemu ya maisha kwa binadamu So, hata wewe Kuna vitu vyako vya siri na kimoja ninachokijua Mimi kwako ni "About ID"

Go ahead
Tofautisa siri ya mtu mmoja na maslahi mapana ya nchi ni vitu viwili tofauti sana.
Yamkini kama wangetoa takwimu sahihi watu wangeogopa na kuchukua tahadhari zaidi kwa kila mtu
 
Hivi watu wa humu mnaishi mitaa gani, mbona izi habar za watu kufa hovyo sijui nyumba kuzungushiwa utepe huku mtaan tupoishi hazipo,, acheni uchawi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tofautisa siri ya mtu mmoja na maslahi mapana ya nchi ni vitu viwili tofauti sana.
Yamkini kama wangetoa takwimu sahihi watu wangeogopa na kuchukua tahadhari zaidi kwa kila mtu
Mbona hupo Smart lakini Kama unajaribu ku-pretend mzee

Kwahiyo taifa litumie mamlaka kuogopesha wananchi kaka ?

Qn
 
Kuficha uso kwa kufunika hakumuondoi Simba aliye mbele yako. Ukimuomba Mungu akuokoe na adui Simba katika mazingira hayo, kumbuka Simba naye atakuwa anamshukuru Mungu kwa chakula kilichombele yake!

Tunawashangaa Wamarekani na Waitaliano kwasababu wanatoa data kamili na inakiwa rahisi kwa wao kujua ugonjwa huu umefikia wapi na wakabiliane nao vipi, mbaya zaidi inaweza kwenda namna hii ukaja sikia "kama huko Ulaya umeisha bhasi hata hapa kwetu umeisha pia"

Mr mkiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tokea tarehe 22/04/2020 Rais wetu, John Magufuli, alipofanya kikao maalum kule Chato na viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, kuhusiana na ugonjwa wa COVID 19, tumeshuhudia kimya kizito kwa upande wa mamlaka za utoaji taarifa wa Tanzania Bara ya maambukizi mapya na vifo vinavyotokana na ugonjwa huo

Tukumbuke pia katika kikao hicho tulimsikia Rais wetu, akipiga "mkwara" mzito, kuwa haridhishwi na namna taarifa zinazotolewa na wizara ya Afya, kuhusu maambukizi mapya na vifo vinavyotokana na ugonjwa huo wa corona

Tulishuhudia pia akifanya "mini reshuffle" kwa kumwondoa aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara ya Afya na kumteua mwingine

Tumeshuhudia waziri wa Afya, Ummy Mawalimu ambaye amekuwa akitupa "updates" za ugonjwa huo, akipata ghafla "kigugumizi" baada ya kikao hicho cha Mheshimiwa Rais kwa kutoweza tena kutupa taarifa zinazohusiana na ugonjwa huo

Ndipo hapo tunapomuuliza waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, nini kimekutokea hadi usitishe kutupa "updates" za maendeleo ya ugonjwa huo nchini?

Tunashuhudua kwenye nchi jirani za Zanzibar, Kenya na nchi nyingine za mbali za Uingereza na Marekani wakitoa "updates" za ugonjwa huo kila siku.

Tunafahamu pia kuwa Taifa la Tanzania limetoka kwenye maombi mazito ya kumlilia Mungu wetu atuepeshie na janga hili la corona.

Ikiwa hakuna maambukizi mapya wala vifo kutokana na maombi tuliyoyafanya kwa Mungu, basi ni vyema waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, akawa anatupatia "daily briefing" na sisi wananchi turejeshe utukufu kwa Mungu wetu, kwa kutuondolea janga hili la corona

Kwa kuendelea kukaa kimya kwa serikali, kunatoa mwanya kwa wananchi wasiolitakia mema Taifa letu, kwa kutangaza wao taarifa wanazozijua wao za maambukizi mapya na vifo vinavyotokea nchini kutokana na ugonjwa huo wa corona

Naziomba mamlaka zinazohusika za wizara ya Afya zitujibie utata huu wa suala nyeti sana la ugonjwa wa corona hapa nchini, ili sisi wananchi zituondolee hofu kubwa inayotukabili hivi sasa kuwa wananchi wa Taifa hili, hususani wa Jiji la Dar, kuwa wanapukutika kwa wingi sana

Ni lazima pia tuwajulishe watawala wetu kuwa kupewa taarifa za maendeleo ya ugonjwa huu wa corona siyo hisani kwa watawala wetu, bali ni kitu cha LAZIMA kwa wananchi wake
 
Kama tulimshuhuhudia RC wa Dar, Paul Makonda, katika mahojiano na kituo kimoja cha luninga hapa nchini cha Clouds TV akikiri wazi kuwa wakazi wake wa Dar hivi sasa wanapukutika!

Iweje sasa mamlaka ya wizara ya Afya nchini, zisiweze kutoa "updates" za ugonjwa huo wa corona ili kuwatoa hofu wananchi?
 
Tokea tarehe 22/04/2020 Rais wetu, John Magufuli, alipofanya kikao maalum na viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, kuhusiana na ugonjwa wa COVID 19, tumeshuhudia kimya kizito kwa upande wa mamlaka za utoaji taarifa wa Tanzania Bara ya maambukizi mapya na vifo vinavyotokana na ugonjwa huo

Tukumbuke pia katika kikao hicho tulimsikia Rais wetu, akipiga "mkwara" mzito, kuwa haridhishwi na namna taarifa zinazotolewa na wizara ya Afya, kuhusu maambukizi mapya na vifo vinavyotokana na ugonjwa huo wa corona

Tulishuhudia pia akifanya "mini reshuffle" kwa kumwondoa aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara ya Afya na kumteua mwingine

Tumeshuhudia waziri wa Afya, Ummy Mawalimuambaye amekuwa akitupa "updates" za ugonjwa huo, akipata ghafla "kigugumizi" baada ya kikao hicho cha Mheshimiwa Rais kwa kutoweza tena kutupa taarifa zinazohusiana na ugonjwa huo

Ndipo hapo tunapomuuliza waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, nini kimekutokea hadi usitishe kutupa "updates" za maendeleo ya ugonjwa huo nchini?

Tunashuhudua kwenye nchi jirani za Zanzibar, Kenya na nchi nyingine za mbali za Uingereza na Marekani wakitoa "updates" za ugonjwa huo kila siku.

Tunafahamu pia kuwa Taifa la Tanzania limetoka kwenye maombi mazito ya kumlilia Mungu wetu atuepeshie na janga hili la corona.

Tunadhani ni muhimu sana kwa wananchi kuendelea kupewa "updates" za ugonjwa huo za kila siku, kama yafanyavyo mataifa mengine.

Ikiwa hakuna maambukizi mapya wala vifo, basi ni vyema waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, akawa anatipatia "daily briefing" na sisi wananchi turejeshe utukufu kwa Mungu wetu, kwa kutuondolea janga hili la corona

Kwa kuendelea kukaa kimya kwa serikali, kunatoa mwanya kwa wananchi wasilitakia mema Taifa letu, kwa kutangaza wao taarifa wanazozijua wao za maambukizi mapya na vifo vinavyotokea nchini kutokana na ugonjwa huo wa corona

Naziomba mamlaka zinazohusika za wizara ya Afya zitujibie utata huu wa suala nyeti sana la ugonjwa wa corona hapa nchini, ili sisi wananchi zituondolee hofu kubwa inayotukabili hivi sasa kuwa wananchi wa Taifa hili, hususani wa Jiji la Dar, wanapukutika kwa wingi sana

Ni lazima pia tuwajulishe watawala wetu kuwa kupewa taarifa za maendeleo ya ugonjwa huu wa corona siyo hisani kwa watawala wetu, bali ni kitu cha LAZIMA kwa wananchi wake
Data za nini? Zikotolewa mnasema sio za kweli! Hamueleweki mnataka nini.
 
ili uzifanyie nini hizo taarifa.?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni wajibu wetu wananchi kuzipata taarifa hizo, kwa kuwa wanaoambukizwa na ugonjwa huo wa corona ni ndugu na jamaa zetu

Vile vile ni sharti na takwa mojawapo la WHO kuwa ni lazima kuwepo na "transparency" katika kutangaza ugonjwa huo kwa wananchi wote

Tukumbuke pia ule msemo unaosema mficha ficha maradhi mwisho kilio kitamwumbua.........
 
Back
Top Bottom