Kwanini Tanzania hakuna daily briefing juu ya Corona virus pandemic?

Mkuu Mystery,
Naunga mkono hoja, enzi za zamani, mambo ya kutoa habari kwa upande wa serikali ilikuwa iko huru kutoa habari au kutotoa, ikijisikia kutoa habari, inatoa, ikijisikia kutotoa habari, haitoi na hakuna yoyote mwenye mamlaka ya kuiuliza.

Lakini kuanzia mwaka 2016, Tanzania tumepitisha sheria ya haki ya kupata habari, the right to information act, ambapo sasa kupata habari ni haki, sio favours, serikali inawajibika kutoa habari za kweli kwa wananchi, hiki kinachoendelea sasa kwenye utoaji wa habari za maendeleo ya ugonjwa wa Corona, ni kinyume cha sheria. Watanzania wana haki ya kupata habari, unless rais atangaze hali ya hatari, sheria zote na haki zote zinasimama!.
P
Kama kutotoa habari ni kinyume cha sheria, je kupitia mahakama wadau wana uwezo wa kuilazimisha serikali kutekeleza wajibu wake?
 
Wanajifanya wanamuheshimu jiwe, natengeneza website ikusanye report toka kwa wananchi directly anonymously hakuna kuweka namba yako ya simu wala email, ngoja watu watutumie report na picha tuweke wenyewe.

Tako moja linafanya nchi nzima tuonekane machizi
 
Tokea tarehe 22/04/2020 Rais wetu, John Magufuli, alipofanya kikao maalum kule Chato na viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, kuhusiana na ugonjwa wa COVID 19, tumeshuhudia kimya kizito kwa upande wa mamlaka za utoaji taarifa wa Tanzania Bara ya maambukizi mapya na vifo vinavyotokana na ugonjwa huo

Tukumbuke pia katika kikao hicho tulimsikia Rais wetu, akipiga "mkwara" mzito, kuwa haridhishwi na namna taarifa zinazotolewa na wizara ya Afya, kuhusu maambukizi mapya na vifo vinavyotokana na ugonjwa huo wa corona

Tulishuhudia pia akifanya "mini reshuffle" kwa kumwondoa aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara ya Afya na kumteua mwingine

Tumeshuhudia waziri wa Afya, Ummy Mawalimu ambaye amekuwa akitupa "updates" za ugonjwa huo, akipata ghafla "kigugumizi" baada ya kikao hicho cha Mheshimiwa Rais kwa kutoweza tena kutupa taarifa zinazohusiana na ugonjwa huo

Ndipo hapo tunapomuuliza waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, nini kimekutokea hadi usitishe kutupa "updates" za maendeleo ya ugonjwa huo nchini?

Tunashuhudua kwenye nchi jirani za Zanzibar, Kenya na nchi nyingine za mbali za Uingereza na Marekani wakitoa "updates" za ugonjwa huo kila siku.

Tunafahamu pia kuwa Taifa la Tanzania limetoka kwenye maombi mazito ya kumlilia Mungu wetu atuepeshie na janga hili la corona.

Ikiwa hakuna maambukizi mapya wala vifo kutokana na maombi tuliyoyafaya kwa Mungu, basi ni vyema waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, akawa anatupatia "daily briefing" na sisi wananchi turejeshe utukufu kwa Mungu wetu, kwa kutuondolea janga hili la corona

Kwa kuendelea kukaa kimya kwa serikali, kunatoa mwanya kwa wananchi wasiolitakia mema Taifa letu, kwa kutangaza wao taarifa wanazozijua wao za maambukizi mapya na vifo vinavyotokea nchini kutokana na ugonjwa huo wa corona

Naziomba mamlaka zinazohusika za wizara ya Afya zitujibie utata huu wa suala nyeti sana la ugonjwa wa corona hapa nchini, ili sisi wananchi zituondolee hofu kubwa inayotukabili hivi sasa kuwa wananchi wa Taifa hili, hususani wa Jiji la Dar, wanapukutika kwa wingi sana

Ni lazima pia tuwajulishe watawala wetu kuwa kupewa taarifa za maendeleo ya ugonjwa huu wa corona siyo hisani kwa watawala wetu, bali ni kitu cha LAZIMA kwa wananchi wake

Mkuu. Wewe tupe tu data Zote hapa Hakuna Shida. Kwanini ungoje Serikali ambayo hata huna trust nayo. Mwaga mkuu Acha majungu. Na corona Hii tuna bundle la kutosha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanajifanya wanamuheshimu jiwe, natengeneza website ikusanye report toka kwa wananchi directly anonymously hakuna kuweka namba yako ya simu wala email, ngoja watu watutumie report na picha tuweke wenyewe.

Tako moja linafanya nchi nzima tuonekane machizi
Tuko pamoja...........
 
Naisubiri kiongozi lini itakuwa tayari mkuu...?
 
Kama kutotoa habari ni kinyume cha sheria, je kupitia mahakama wadau wana uwezo wa kuilazimisha serikali kutekeleza wajibu wake?
Proved
Kama Katiba inasema kuwa ni lazima mwananchi apewe habari, basi hata likipelekwa mahakamani suala hilo, mahakama itaiamuru serikali itekekeze takwa hilo la kisheria.

Lakini kwa mazingira ya nchi yetu ambapo Jiwe aliwahi kutamba kuwa mhimili wake ndiyo uliojichimbia zaidi chini, basi tutarajie mahakama nayo ifanye uamuzi huo kisiasa......

Usije shangaa mahakama ikaamua "kukwepa" mamlaka yake na kudai kuwa inaogopa kugonganisha mihimili!
 
Tokea tarehe 22/04/2020 Rais wetu, John Magufuli, alipofanya kikao maalum kule Chato na viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, kuhusiana na ugonjwa wa COVID 19, tumeshuhudia kimya kizito kwa upande wa mamlaka za utoaji taarifa wa Tanzania Bara ya maambukizi mapya na vifo vinavyotokana na ugonjwa huo

Tukumbuke pia katika kikao hicho tulimsikia Rais wetu, akipiga "mkwara" mzito, kuwa haridhishwi na namna taarifa zinazotolewa na wizara ya Afya, kuhusu maambukizi mapya na vifo vinavyotokana na ugonjwa huo wa corona

Tulishuhudia pia akifanya "mini reshuffle" kwa kumwondoa aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara ya Afya na kumteua mwingine

Tumeshuhudia waziri wa Afya, Ummy Mawalimu ambaye amekuwa akitupa "updates" za ugonjwa huo, akipata ghafla "kigugumizi" baada ya kikao hicho cha Mheshimiwa Rais kwa kutoweza tena kutupa taarifa zinazohusiana na ugonjwa huo

Ndipo hapo tunapomuuliza waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, nini kimekutokea hadi usitishe kutupa "updates" za maendeleo ya ugonjwa huo nchini?

Tunashuhudua kwenye nchi jirani za Zanzibar, Kenya na nchi nyingine za mbali za Uingereza na Marekani wakitoa "updates" za ugonjwa huo kila siku.

Tunafahamu pia kuwa Taifa la Tanzania limetoka kwenye maombi mazito ya kumlilia Mungu wetu atuepeshie na janga hili la corona.

Ikiwa hakuna maambukizi mapya wala vifo kutokana na maombi tuliyoyafaya kwa Mungu, basi ni vyema waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, akawa anatupatia "daily briefing" na sisi wananchi turejeshe utukufu kwa Mungu wetu, kwa kutuondolea janga hili la corona

Kwa kuendelea kukaa kimya kwa serikali, kunatoa mwanya kwa wananchi wasiolitakia mema Taifa letu, kwa kutangaza wao taarifa wanazozijua wao za maambukizi mapya na vifo vinavyotokea nchini kutokana na ugonjwa huo wa corona

Naziomba mamlaka zinazohusika za wizara ya Afya zitujibie utata huu wa suala nyeti sana la ugonjwa wa corona hapa nchini, ili sisi wananchi zituondolee hofu kubwa inayotukabili hivi sasa kuwa wananchi wa Taifa hili, hususani wa Jiji la Dar, wanapukutika kwa wingi sana

Ni lazima pia tuwajulishe watawala wetu kuwa kupewa taarifa za maendeleo ya ugonjwa huu wa corona siyo hisani kwa watawala wetu, bali ni kitu cha LAZIMA kwa wananchi wake
Hakuna kitu kilichokuwa kina kera kama waziri Ummy kujitokeza kututisha. Angalau sasa kaacha mioyo imetulia. Sasa bora aje na mkakati wa kupunguza maambukizi.
 
Hivi mtasemaje kuwa waziri Ummy Mwalimu alikuwa anatutisha, wakati alikuwa anatimiza wajibu wake wa kutupa habari za ukweli?
 
Ipo tayari hadi sasa nafanyia marekebisho kidogo tu. Sa hivi natafuta hosting ambaye atapokea malipo kwa kutumia bitcoin kila kitu nafanya kwa bitcoin so hata wakisema watafute aliyetengeneza nani watatafuta mno hawashiki mtu

Much respect kiongozi usisahau kuiweka hapa jamvini ili watu waweze kupata access kiurahisi na kuweza kupata watu wengi zaidi watakaoweza kutoa taarifa sahihi mkuu.

Ubarikiwe sana katika bwana mkuu.
 
Hivi mtasemaje kuwa waziri Ummy Mwalimu alikuwa anatutisha, wakati alikuwa anatimiza wajibu wake wa kutupa habari za ukweli?
Alishindwa kutumia akili. Mbona wagonjwa wa malaria hawatangazwi??? Huwezi kukopy kila kitu
 
Back
Top Bottom