Drone Camera
JF-Expert Member
- Jul 25, 2017
- 14,041
- 13,907
Watazitoa subir
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tofautisa siri ya mtu mmoja na maslahi mapana ya nchi ni vitu viwili tofauti sana.Siri ni sehemu ya maisha kwa binadamu So, hata wewe Kuna vitu vyako vya siri na kimoja ninachokijua Mimi kwako ni "About ID"
Go ahead
Uliweka uzi wenye mantiki kubwa, hivi bado upo, nautafuta siuoni. Nilijua watautoa maana ulikuwa hatari kidogoSijawai kuona nchi duniani inayopika takwimu kama Tanzania
Mbona hupo Smart lakini Kama unajaribu ku-pretend mzeeTofautisa siri ya mtu mmoja na maslahi mapana ya nchi ni vitu viwili tofauti sana.
Yamkini kama wangetoa takwimu sahihi watu wangeogopa na kuchukua tahadhari zaidi kwa kila mtu
Mungu hadhihakiwi [emoji40]Hivi watu wa humu mnaishi mitaa gani, mbona izi habar za watu kufa hovyo sijui nyumba kuzungushiwa utepe huku mtaan tupoishi hazipo,, acheni uchawi
Sent using Jamii Forums mobile app
Data za nini? Zikotolewa mnasema sio za kweli! Hamueleweki mnataka nini.Tokea tarehe 22/04/2020 Rais wetu, John Magufuli, alipofanya kikao maalum na viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, kuhusiana na ugonjwa wa COVID 19, tumeshuhudia kimya kizito kwa upande wa mamlaka za utoaji taarifa wa Tanzania Bara ya maambukizi mapya na vifo vinavyotokana na ugonjwa huo
Tukumbuke pia katika kikao hicho tulimsikia Rais wetu, akipiga "mkwara" mzito, kuwa haridhishwi na namna taarifa zinazotolewa na wizara ya Afya, kuhusu maambukizi mapya na vifo vinavyotokana na ugonjwa huo wa corona
Tulishuhudia pia akifanya "mini reshuffle" kwa kumwondoa aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara ya Afya na kumteua mwingine
Tumeshuhudia waziri wa Afya, Ummy Mawalimuambaye amekuwa akitupa "updates" za ugonjwa huo, akipata ghafla "kigugumizi" baada ya kikao hicho cha Mheshimiwa Rais kwa kutoweza tena kutupa taarifa zinazohusiana na ugonjwa huo
Ndipo hapo tunapomuuliza waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, nini kimekutokea hadi usitishe kutupa "updates" za maendeleo ya ugonjwa huo nchini?
Tunashuhudua kwenye nchi jirani za Zanzibar, Kenya na nchi nyingine za mbali za Uingereza na Marekani wakitoa "updates" za ugonjwa huo kila siku.
Tunafahamu pia kuwa Taifa la Tanzania limetoka kwenye maombi mazito ya kumlilia Mungu wetu atuepeshie na janga hili la corona.
Tunadhani ni muhimu sana kwa wananchi kuendelea kupewa "updates" za ugonjwa huo za kila siku, kama yafanyavyo mataifa mengine.
Ikiwa hakuna maambukizi mapya wala vifo, basi ni vyema waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, akawa anatipatia "daily briefing" na sisi wananchi turejeshe utukufu kwa Mungu wetu, kwa kutuondolea janga hili la corona
Kwa kuendelea kukaa kimya kwa serikali, kunatoa mwanya kwa wananchi wasilitakia mema Taifa letu, kwa kutangaza wao taarifa wanazozijua wao za maambukizi mapya na vifo vinavyotokea nchini kutokana na ugonjwa huo wa corona
Naziomba mamlaka zinazohusika za wizara ya Afya zitujibie utata huu wa suala nyeti sana la ugonjwa wa corona hapa nchini, ili sisi wananchi zituondolee hofu kubwa inayotukabili hivi sasa kuwa wananchi wa Taifa hili, hususani wa Jiji la Dar, wanapukutika kwa wingi sana
Ni lazima pia tuwajulishe watawala wetu kuwa kupewa taarifa za maendeleo ya ugonjwa huu wa corona siyo hisani kwa watawala wetu, bali ni kitu cha LAZIMA kwa wananchi wake
Ni wajibu wetu wananchi kuzipata taarifa hizo, kwa kuwa wanaoambukizwa na ugonjwa huo wa corona ni ndugu na jamaa zetu